Wananchi wa Uingereza jana tarehe 6 mwezi tano wamepiga kura kuchagua viongozi watakaoiongoza nchi kwa muda wa miaka mitano. Wananchi walianza kupiga kura tangu saa 07:00 Asubuhi mpaka saa 22:00 usiku.
Ijapokuwa kuna baadhi ya sehemu nyingine wananchi walishindwa kupiga kura kutokana na kuchelewa kufika katika sehemu za kupigia kura.Viti 650 ndiyo vilikuwa vinagombaniwa na mshndi wa viti vingi ndiye atakayeiweza kuongoza nchi.

Ili uweze kushinda inabidi upate viti 326 kuweza kuongoza nchi lakini vyama vyote vimeshindwa kufikia viti hivyo.

Matokeo ya uchaguzi yalianza kutangazwa kwa mshindi wa kiti cha Houghton & Sunderland baada ya Labour Party kushinda kiti hicho kwa kura 19137 kwa kupitia mgombea wao Bridget Philipson mwenye umri wa miaka 26. Mpaka kufikia mchana walimaliza kuhisabu kura katika majimbo yote ya uchaguzi.

Mpaka hivi sasa chama cha Conservative kinataka kuungana na Chama cha Lib Democrat Party ili kuweza kuongoza nchini.

Chama cha Conservative kimepata kura 305, Labour Party kura 258, Lib Democrat Party kura 57 na vyama vingine vimepata kura 28.

Uchaguzi umefanyika lakini hakuna chama chochote chenye nguvu ya kuongoza kutokana na kushindwa kufikia kiwango cha viti vya wabunge. Kwahiyo madaraka ya kuongoza yamebakia kwa Labour Party mpaka mshindi atakapopatikana.

Viti vya Wabunge vikifikia 326 ndivyo yinavyoweza kukipa chama nguvu ya kuweza kuongoza nchi na isiwe pungufu ya viti hivyo.
Ally Muhdin wa
http://www.tz-one.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2010

    CCM wameponza labour party. Kwa kuhamishia matawi yake (CCM) huko

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 07, 2010

    tz na sisi tufanye mapinduzi kama hayo basi. too long for CCM

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2010

    Mbona Waziri Mkuu aliyeshindwa uchaguzi hataki kutoka ofisi ya namba 10! au amepata maelekezo toka kwa Maraisi madikteta wa Afrika na latini-Amerika?
    Maana 258+57= 315 ; wakati za mshindi 305+57= 362 yaani zaidi ya 326 kutengeneza 'majority'.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2010

    wabongo wa Uk mnaotegemea benefits kaeni mkao wa kula Torry wanakuja kwenye manifesto yao waliweka bayana kuwa utolewaji wa benefits utasitishwa pindi utakaposhindwa fanya kazi waliokupa.
    Ukisikia la mgambo..............

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2010

    TORY WANATAKA WAAMIAJI WARUDI KWAKO, WAMATUMBI RUDINI NYUMBANI NYIE, MTAPIGWA NA NJAA ILE MBAYA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...