kutoka kushoto ni Mhe. Balozi Fatuma Ndangiza, Mzee Quoro, Mhe. Waziri Louise Mushikiwabo, Mhe. Balozi Christopher Liundi, Mzee Mwaheleja na Advocate Safari.
Godfrey Semwaiko, Mhe. Balozi Christopher Liundi (mwenyekiti TARAFA), Mzee Quoro (Makamu TARAFA), Mhe. Waziri Louise Mushikiwabo, Advocate Safari (Katibu TARAFA), Mzee Mwaheleja (Mweka hazina TARAFA), na Mhe. Balozi Fatuma Ndangiza.

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Mhe. Louise Mushikiwabo, alikutana na kamati ya chama cha uhusiano wa Tanzania na Rwanda (TARAFA) kwa maongezi mafupi.

Kamati hiyo ilialikwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Fatuma Ndangiza, nyumbani kwake kwa chakula cha mchana, ambapo waziri huyo alitaka kuonana na kamati hii ya TARAFA (Tanzania Rwanda Friendship Association) mara baada ya kumaliza kuhudhuria mkutano wa World Economic Forum.

Waziri alitaka kujua mipango endelevu ya TARAFA na RWATAFA (Chama mwenza cha Rwanda) kwa kuongeza uhusiano kati ya wananchi wa kawaida wa nchi hizi mbili. Alishauri wananchi washirikiane kwa karibu zaidi, na kwa kupitia taasisi za kijamii kama TARAFA, iwe rahisi kuendesha program mbalimbali ambazo zitasaidia serikali na viongozi katika kuleta mahusiano ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.

Pia Mheshimiwa waziri alitoa ahadi ya kusaidia mipango endelevu katika kuwakutanisha na kuwaunganisha wananchi wa nchi hizi mbili, na kwamba atashauriana na viongozi wenzake nchini Rwanda katika kuhakikisha lolote linawezekana katika kuleta uhusiano wa karibu kati ya wananchi wa nchi hizi, hasa kwa kuanzia wale walioko katika mikoa ya mpakani mwa Tanzania na Rwanda.

Mpaka sasa TARAFA imepanga kuwa na program za utamaduni katika kuwaelimisha watanzania kuhusu Rwanda na kuiomba Bodi ya Utalii nchini kutoa mikanda ya video kwa nia ya kubadilishana na RWATAFA katika kuitangaza Tanzania nchini Rwanda.

Katibu Mwenezi, TARAFA.
Godfrey Semwaiko

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 07, 2010

    udumu ushirikiano wa nchi zote mbiri rwanda na tanzania,maana zote ni jirani.oyeee EAC

    mdau kigali makazi boksini kusaka chake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...