Na Ripota wa Globu ya Jamii

Hukumu ya kwenda gerezani na kutumikia kifuncho cha miaka miwili jela ndiyo adhabu anayoanza kuitumikia aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania BoT Amatus Liyumba, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo wakati akiwa kazini, hususana wakati wa ujenzi wa maghorofa pacha ya BOT jijini Dar.

Hata hivyo leo hii katika mahakama hiyo, mahakimu watatu wanaounda jopo la mahakimu linalosikiliza kesi hiyo, walitofautiana huku wawaili kati yao wakiwa na mtazamo mmoja wakati wa uandikaji na usomwaji wa hukumu yao.

Wawili hao ambao ni hakimu Benedict Mwingwa pamoja na Lameck Mlacha, waliandika na kusoma hukumu iliyofanana ambayo kimsingi ndiyo iliyomtia hatiani Liyumba na kumsababishia kupata adhabu hiyo.

Kwa upande wa Hakimu Mkasimongwa ambaya ndiye aliyekuwa kiongozi wa jopo hilo la mahakimu, ndiye aliyeandika hukumu yake tofauti hukumu ambayo ilionesha kumuachia huru mshatakiwa kwa kuwa hana hatia.

Lakini kutokana na nafasi kubwa na kuungwa mkono iliyoonekana na mahakimu wawili, ilisababisha mahakama hiyo kuichukua kiutekelezaji hukumu ya mahakimu hao Mlacha na Mwingwa na kumuhukumu Liyumba kifungo hicho.


Akisoma hukumu hiyo iliyomtia hatiani Liyumba, Hakimu Mlacha alisema kuwa ushahidi wa mashahidi nane wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, ndivyo vilivyopelekea mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo.


Mlacha alisema kuwa, alisema kuwa Liyumba alisahini barua za mahidhinisho ya ufanyikaji wa mabadiliko ya ujenzi wa jengo la BoT, wakati hakiwa hana mamlaka ya kufanya hivyo.

Aliongeza kuwa barua hizo zilikuwa na sahihi yake Liyumba jambo ambalo ni kinyume kwani ilitakiwa ziidhinishwe na bodi ya benki na si kurugenzi kama ambavyo alikuwa akifanya Liyumba.

Pia mahakama hiyo iliukataa ushahidi wa utetezi uliotolewa mahakamani hapo na Liyumba, ushahidi ambao ulidai kuwa mammlaka ya kusahini barua hizo, alipewa na aliyekuwa Gavana wa benki hiyo Daud Balali kwa njia ya mdomo.

Mlacha alisema kuwa mahakama imeingia mashaka juu ya kuamini hilo, kutokana na ukweli kuwa BoT ni taasisi ambayo kulingana na ukubwa wake na uzito wake hisingeweza kutoa maamuzi au kuumpa mtu madaraka makubwa pasipo kutumia maandishi hili kutunza kumbukumbu.


Aliongeza kuwa Mahakama hiyo inauchukulia ushahidi wa utetezi uliotoewa mahakamani hapo, si wa kweli kwani hata mmoja wa mashahidi wa upande wa mashtaka aliithibitishia mahakama hiyo kuwa maelekezo ya Gavana yalikuwa yakitoka kwa barua.


"Hata shahidi wa nne wa upande wa mashtaka bwana Michale Shirima, ambaye alikuwa mjumbe wa bodi ya benki, aliithibitishia mahakama hii kuwa maamuzi ya Gavana yalikuwa yakitolewa kwa maandishi na si kwa mdomo kama Liyumba alivyotuambia"alisema Mlacha.

Mbali na hilo, mahakama pia iliukataa ushahidi wa shahidi wa pili wa utetezi ambaye ni aliyekuwa Katibu wa Benki bwana Bosco Kimela, kwa kuita ushahidi huo kuwa ulikuwa wa kutungwa na mstakiwa pamoja na shahidi huyo.


Mlacha alisema kifungu namba 96 (1) cha Kanuni ya adhabu, kinasema kwamba iwapo mtu aliyeajiriwa katika taasisi ya umma, akielekeza kufanyika kwa jambo kinyume na sheria na taratibu za ofisi na hivyo kusababisha madhara kwa mtu mwingine, atakuwa ametenda kosa.

Aliongeza kuwa baada ya kupitia kwa makini kifungu hicho, mahakama imeona kuwa kosa alilotenda Liyumba lilikuwa ni kinyume na sheria na kwamba lilileta madhara kwakuwa gharama za ujenzi wa jengo hilo zilipanda kulinganishwa na zile zilizopangwa kwenye mkataba uliopitishwa na bodi hapo awali.


Kwa upande wa Wakili wa utetezi Majura Magafu, kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo aliiomba mahakama hiyo kupanga adhabu kwa kuangalia kifungu cha 38 (1) 16 ambacho kinairuhusu mahakam kutoa adhabu ya faini, ama kifungo cha nje kwa mashtakiwa.


“Muheshimiwa tunaiomba mahakama iweza kukiangalia kifungu hicho na kumpa mshatakiwa adhabu ya kulipa faini, au kifungo cha nje hasa ikizingatiwa umri wa mshtakiwa ni wa miaka 62 na vilevile anamaatatizo ya kiafya.

Magafua alidai kuwa mahakama izingatie kwamba Liyumba nategemewa na familia yake.

Lakini mambo yalikuwa tofauti wakati wa upangaji wa adhabu hiyo, ambapo Hakimu Mlacha na Mwingwa walipingana na maombi hayo ya magafu.

Pamoja na maombi hayo kwa mahakama, Hakimu Mlacha alitoa adhabu ya kifungo hicho baada ya kusema kuwa mshtakiwa hasingeweza kulipa faini hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa kuna mapambano ya vitendo vya rushwa.

Kwa upande wa Hakimu Edson Mkasimongwa, alisoma huku yake aliyoiandaa ambayo ilipingana na hukumu ya awali, ambapo pia ilisomwa hili kutunza kumbukumbu za mahakama.

Mkasimongwa alisema kuwa upande wa mashataka umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya Liyumba, hivyo anatakiwa awe huru kutokana na hilo.

Mkasimongwa alipingana na hoja ya kuwa mshtakiwa alisahini barua za kuhidhinisha kufanyika kwa mabadiliko wakati akiwa hana mamlaka hayo, kwasababu haikuwa na msingi.

Aliongeza kuwa kwa upande wa hilo, yeye haoni kama ni kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwani Liyumba kama mkuu wa kurugenzi iliyokuwa ikisimamia ujenzi huo alikuwa na na mamlaka ya kusahini barua hizo kama aliona kuwa hazikuwa na ubishani.

Hukumu hizo zilipomalizika kusomwa , Liyumba aliondoka mahakamani hapo huku akilindwa na askari kuelekea kwenye gari la magereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    Michuz sio Jijini Dar Bwana Wewe ni Mtu wa Habari Sema Jijini La Dar-es-salaam. Dar ndio Mji Gani?.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    Bez comentariv "No comment"

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    miaka miwili ya jela ni miezi. uchaguzi umefika hili ni changa la macho hamna lolote

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    michuzi kwenye video yako nimekusikia ukisema"POLE"
    unampoza au una'mnafiki...
    *halafu usibane hii comment

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2010

    Tanzania kuna uonevu sijaona,mtu anaiba kuku tu jela miaka mitatu na kazi nzito,huyu kaiba mihela eti miaka miwili tena bila faini wala kazi nzito.haki haipo kabisa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 24, 2010

    jamani huu ni uonevu wa hali ya juu jamaa katia hasara taifa ma milioni ya pesa anaenda jela miaka 2 kasusura kaiba vijisenti ambavyo hata robo ya robo ya hela ya liumba amekwenda jela miaka 35...nchi hii inataka rais mwendawazimu kidogo..sikubaliani hata kidogo na hukumu hii,na michuzi usiibane maana kila mtu ana haki ya kutoa maoni........ninavyoona mimi watanzania watachoka huu ujinga soon tu,nyie subirini tu,tuone hukumu zenu zisizo za haki ndizo zitakazo wapeleka kaburini.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 24, 2010

    SCAPEGOAT

    MBUZI WA KAFARA

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 24, 2010

    ...2yrs? haya maigizo kwa kweli hayaishi... tusubiri december atolewe kwa msamaha wa raisi...
    Bongo tambarare...!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 24, 2010

    MTU GANI ANAKUWA JELA YA TANZANIA ANAKWIVA KAMA LIYUMBAA,YUKO JELA LAKINI KANAWIRIRIIIIII

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 24, 2010

    KAMA SHERIA ZA TANZANIA ZINARUHUSU CAMERA NDANI YA MAHAKAMA BASI HUO NI UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU ZA KIMSINGI. HUWEZI KUMPIGA MTUHUMIWA WA KESI MAHAKANI TENA NDANI NA UKAANZA KUIONYESHA DUNIA HATA KAMA ANAKWENDA JELA NI UDHALLILISHAJI HUO, ANAYO HAKI KABISHA YA KUWASHITAKI. HEBU SHERIA YA TANZANIA ILITAZAME HILO-CAMERA NDANI YA MAHAKAMA!!!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 24, 2010

    Watanzania sijui wakoje...mwanzo mlisema hafungwi hii kesi ni danganya toto.

    Sasa amefungwa mnasema, mnasema ohh miaka miwili sio kitu atakaa jela miezi tu.

    Mlitaka afungwe kinyume na sheria ili iweje.

    Sisi aliyeturoga walahi alishakufa miaka nyingi sana. Ujinga huu hauna mfano

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2010

    Hii Case imetumika kama warning ya walio madarakani kuwa ukitumia vibaya madaraka unaweza kwenda jela miaka miwili.

    Zaidi ya hapo sioni kitu ni kama vile Ze comedi tu ya kuwarubuni wahisani waendelee kututupia change zinazobaki kwao.

    Hali ni ngumu jamani, tusiposimama kwa miguu yetu bongo tutarajie kuoneana kwa sana tu hata kama mtu hana kosa mnamtoa kafara.

    wafadhili wao wanabana matumini, Cameron anataka £6.2b kwa maana kuwa wanakata baadhi benefit kama child trust na kuondoa quangos. pia wanasitisha ajira serikalini, sisi ndiyo kwanza tunaongeza majimbo ya uchaguzi na wizara kibao. Matokeo yake tunalazimishana kufanya mambo ya kuoneana ili kuwaridhisha wafadhili.

    Pole Amatus, usijali, jela yako ni kwa faida ya nchi yako. Ila angalia miaka miwili mingi ukitaka kuwaridhisha askari jela utamaliza fungu lako halafu ukitoka yale mambo yetu ushindwe tena.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 25, 2010

    MIAKA MIWILI TUUUUU???!!!!.....

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 25, 2010

    JAMANI MIMI SIELEWI KABISA HII. KUTUMIA MADARAKA VIBAYA NI KOSA LA JINAI AU LA KINIDHAMU?? HUYU BWANA AMESHITAKIWA KWA KOSA GANI LINALOSITAHILI AENDE JELA??? KWA NINI BASI WASIMSHITAKI KWA KUIIBIA UMMA?? MIMI NAAMINI HIVI NI VIINI MACHO TU VYA CCM NAS SISI KAMA ILIVYO ADA TUTASHANGILIA BILA KUJIULIZA KULIKONI?
    NA HUYU MWISHONI ATASHINDA ALAFU ATATUANGUSHIA MADAI YA MABILIONI KWA KUMUONEA WEWE FUNGUA MACHO.
    MZAWA

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 25, 2010

    hivi bila wafadhiri serikali hata ingeziona hizo pacha???????nakumbuka zilianza kupigiwa kelele miaka kama minne imepita leo ndo uchunguzi umekamilika au?????

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 25, 2010

    hamna wa kumpiga na kiatu ?

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 25, 2010

    Miaka miwili akitoka ni millioner. Angefilisiwa ndio tujue kweli haki imetendeka. i am sure alivyosign hiyo kitu alipata na commission sio bure kulikua na ulaji hapo. Leo familia yake inamuhitaji. Unajua ni wanafunzi wangapi wanakosa elimu kwa upumbavu wao?

    Tanzania jamani mwenzi wa kumi muamke .....

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 25, 2010

    uwiiii my Liyumbaaa!!
    usijali najua una-access ya room yako nzuri hapo jelani kila kitu kipo

    ntakuja tu usijali mupenzi

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 25, 2010

    Wanasheria wako wanajua miaka miwili lazima utumikie, na wanajua una mapesa mengi, ili kuendelea kula nawe wanataka kukukatia rufaa ili mambo yasiishie hapo leo mahakamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...