Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T.833.BEF lliilokutwa limesheheni mizigo na abiria mkoani Singida licha ya juhudi mbalimbali zinazofanywa na vyombo vya usalama kupunguza ajari za barabarani kwa kupiga marufuku malori ya mizigo kusafirisha abiria kutokana na baadhi ya madereva kuendelea kukiuka sheria za barabarani. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2010

    Watu wanalazimika kupanda malori kwa kuwa hakuna usafiri mbadala. Mtu hawezi kupeleka magari ya abiria sehemu ambako hakuna barabara. Sertikali iboreshe barabara hadi vijijini na haya mambo ya kusafiri kwa malori yatapungua.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2010

    muwapelekee mabasi sio mnalalama tu au mkae kimya kama hamuwezi kupeleka usafiri mnaoutaka ninyi

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2010

    Duu! Bado kuna Scania 81 barabarani!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 24, 2010

    Aisee, hilo Scania 81 liko bomba sana. Hiyo ni collector's item na mmiliki wake anaweza kupata pesa nyingi sana akiliuza Ulaya kuliko kulitumia kubebea watu vijijini Bongo. Sitashangaa kama Wazungu wataanza kulifuatilia lori hilo kupitia blog hii.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2010

    Kwako ANONY: 09:54:00 PM

    Ndani ya bongo hiyo inaweza kuwa cabin ya Scania, chassis ya Leyland DAF na injini ya Volvo.

    Kwa hiyo kimsingi, ili mradi inatembea, usisome nembo ambao unaweza kuwa urembo tu.

    Shida ndiyo inafanya watu wakubali kupanda gari kwa mtindo kama huu wa kwenda mnadani.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2010

    Hii ni advertisement nzuri sana kwa SCANIA, wewe unaezungumzia malori kupigwa marufuku kubeba abiria umezaliwa Manzese nini? Hivi hujui Tanzania hii kuna sehemu mabasi au whatever magari ya abiria mnayoyatumia mijini hayaendi? Malori haya ndio option pekee ya usafiri, tena huko kuzuri kuna barabara, kuna ambako hata mashine kubwa kama hizo hazifiki. Umeshakusikia Lyamba lya Mfipa wewe? Na Makongorosi je...!? Acha bwana, Tanzania sio Dar Es Salaam tu, tembea uone.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2010

    Kwa kumjibu Anony wa Tue May 25, 12:39:00 AM, nina hakika hili ni Scania 81 baada ya kuchunguza ‘axle’ ya mbele. Hata hivyo, lori hili nyuma limefungwa ‘axle’ ya Liaz. Hapa hakuna cha kushangaza kwani aina hii ya usafiri ndio inayotumika sehemu nyingi za Bongo. Kupiga marufuku malori kubeba abiria ni agizo lisilotekelezeka Tanzania kwa sasa na hata wakubwa wanatambua ukweli huu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2010

    Hawa ni wauza nguo wakielekea au kutoka kwenye minada ya vijijini, huko Singida ndo usafiri wa wauza nguo minadani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...