Mh. Balozi Mwanaidi Maajar akiongea katika sherehe za Muungano usiku wa kuamkia leo jijini London ambapo pia Jumuiya ya Watanzania uingereza walitumia nafasi hiyo kumuaga rasmi Mh. Balozi ambaye kwa sasa kapangiwa kituo cha Washington DC, Marekani
Mwanachama wa New Deal Africa Ally Muhdin akimkabidhi zawadi Balozi Maajar
Uongozi wa New Deal Africa chini ya mwenyekiti wake Ayoub Mzee (kulia) na Shaaban Kawawa (koti bluu) wakimuaga Balozi Maajar


Mwenyekiti wa watanzania waishio Uingereza Bw. John Lusingo na Balozi Maajar wakiongea katika meza kuu ya mnuso huu
Bendi ya African Jambo ikitumbuiza.

Na Ripota wetu, London
Watanzania waishio nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo walifanya sherehe za kusheherekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Kumuaga Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Bi. Mwanaidi Sinare Maajar ambaye amehamishiwa Marekani.

Katika Sherehe hizo zilifanyika katika Ukumbi wa LA Royale Bonqueting Suites, Tottenham jijini London, Mgeni wa heshima Bi. Mwanaidi Maajar aliwashukuru watanzania kwa kuanzisha vyama na jumuiya ambazo zimewakutanisha na kudumisha umoja, upendo na kuwasaidia Watanzania waishio nyumbani na ughaibuni.

Balozi Maajar aliwausia Watanzania kutokata tamaa katika kujishighulisha na kufanya biashara na kujiendeleza katika maisha yao kwani serikali ipo tayari kuwasaidia endapo wataonyesha moyo wa maendeleo.

"Nitapita kuwatembelea kuangalia maendeleo yenu yamefikia wapi" aliongezea Balozi Maajar ambaye amemaliza muda wake wa kikazi nchini Uingereza.

Naye Mwenyekiti wa chama cha Watanzania nchini Uingereza Bw. John Lusingo alitoa hutuba fupi ya kumuaga Bi. Maajar, "Tunakushukuru kwa kutuunganisha Watanzania na kutufanya kuwa kitu kimoja" Bw. Lusingo alisema.

Bw. Lusingo aliendelea kusema kuwa Balozi Maajar ametupa changamoto ya kuweza kuwa na umoja, uzalendo na imani katika mambo mbali mbali.

Jumuiya ya New Deal Africa ilitoa pongezi na shukrani kwa Balozi Maajar kwa mchango wake mkubwa wa kuiwezesha jumuiya hiyo kuweza kuanzishwa na kufikia hapo ilipo. Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya mwenyekiti wa New Deal Africa Bw. Ayoub Mzee, mwasisi wa Blog ya TZ-ONE Bw. Ally Muhdin alisema tusingeweza kuwa na mawazo ya kuanzisha jumuiya hii endapo tusingepata changamoto na ushauri kutoka kwa Balozi Maaajar.

Watanzania wengi walijitokeza katika sherehe hizo akiwemo mwimbaji maarufu wa Taarabu Bi. Sabaha Salum Mchacho ambaye aliwatumbuiza washabiki wake kwa kuwaimbia nyimbo ya "FIMBO YA MUNGU"

African Baand haikuwa nyuma illipata fursa ya kuwatumbuiza na kuwaburudisha Watanzania kwa kuwapigia nyimbo za kizamani ambazo zilitamba enzi hizo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2010

    sasa sherehe hizo zilikuwa zinasherehekewa na upande mmoja tu sura za wazenji hazikuoneka nilijisikia vibaya hawa wezetu kufikia mamuzi yakuto fika

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2010

    It is our sincere belief that she enjoyed her time at WESTMINSTER! Or was it?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 02, 2010

    DUH FINALLY! ALL THE BEST

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2010

    HAWA WENZETU WAPEMBA WANA MATATIZO MAKUBWA.ANGEKUWA MAALIM SEIF KAJA UNGEWAONA WAKUMWAGA.
    CHA AJABU WAMETUMIWA SALAM NA MAALIM SEIF KUWA WAIPIGIE LIB.DEMOCTTRATIC KWENYE UCHAGUZI WA UINGEREZA WIKI.HII.
    NAO WANATAKA KUTEKELEZA WAKATI SERIKALI YA CHAMA CHA LABOUR CHINI YA GORDON BROWN IMEWAFANYIA MENGI SANA.

    KWANI HAWAWEZI KUPIMA KWA AKILI ZAO HADI WAMSIKILIZE MTU AMBAYE YUKO MAILI NA MAILI HUKO MBALI NA ASIYEJUA MAZINGIRA YA UINGEREZA.NAWAULIZA HATA TIMU YA MPIRA HAWAWEZI KUSHANGILIA HADI WACHAGULIWE NA MAALIM SEIF?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2010

    Karibu NY mama uniamshe kwenye usingizi mzito.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2010

    mdau wa kwanza hapo juu sio hivyo nyinyi watu mna majungu sana mmearibu london mna midomo mirefuuuuuuu kutwa umbea tuu mlivyofanyiwa sawasawa walalamishi sana nyinyi

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2010

    Haya sasa Wa-TZ wa Marekani hasa Washington-Dc mjiandae kuwa kitu kimoja. Kuna siku nilikuwa DC M-TZ mmoja akaalalamika kuwa Wa-TZ wa huk Marekani siyo kama wa Uingereza. Sababu Wat-TZ wa huko hawakuwahi kupata balozi kama Maajar ambaye huwa anafikiria kuwa Wa-TZ walioko Ughaibuni ni kitu kimoja. Jamani nawaomba mjikusanye na muwe na umoja wa nguvu kama mataifa mengine ya Kiafrika huk Marekani.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2010

    kweli mama tutakukumbuka huna makuu kanisani yupo msikitini yupo popo mkimualika kama ana muda lazima atie timu mcheshi na mkalimu huyu mama kweli usa mmepata barozi

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2010

    Wewe hapo juu . Uk is a sociolist country na USA capitalist . Hapa hufungui fungui matawi kama huko . Na tupo buisy sana na schedule ,tunafanya kazi hapa . Mimi Baada ya kwenda kwenye matawi ya CCM niheri nikatengeneze 120 kwa siku nilipie wanangu ada ya shule . Hatuhitaji balozi tukifiwa hawana pesa . Hapa marekani ni tofauti sana na huko kwa hiyo we are sorry we won't be able to come

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2010

    asituletee tu UCCM otherwise karibu sana mama yetu

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2010

    Anon wa 03:00:00, Wacha ulimbukeni wako... oh...sisi tunafanya kazi...oh sijui nini...Listen!!! --- Mimi nimekaa huko na kupata digrii moja na diploma mbili professionals na kuchapa kazi nzuri. Lakini mambo hayo hayakunifanya nijitenge na WA-TZ wenzangu. Tumeshirikiana katika raha na shida (DC area na NY/NJ) as wana-TZ for years bila kujali huyu anatoka wilaya gani au anasali wapi. Mama Sinare-Majar tangu alipokuwa UDSM (mimi nilikuwa mwaka mmoja mbele yake) mpaka leo ni mtu wa watu. Wewe kama unataka ujitenge from wa WA-TZ you are free to do so, usitafute visingizio visivyo na kichwa wala mguu...

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2010

    Ha ha ha, anon wa 03.00.00, huko kazini uliko "buisy" na ambako "mnafata schedule" ambako si "sociolist" unatumia lugha gani??? Kihispania...Free advice: nenda shule za usiku zitakusaidia kujua Ki-english, muhimu saaana USA...nyinyi ndiye mlikuwa mnatoroka shule...ennnnhhh!!!!????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...