Profesa J
Juma Nature
Mwana FA
Joe Makini
Dully Sykes
Belle 9 (shoto) na Diamond
CPwaa
Mwasiti (shoto) na Chidi Benz
wana THT









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 49 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2010

    nyie mmechangia au nyie mmelipwa kuwekwa kwenye tangazo?


    umaskini wa akili ni kitu kibaya sana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2010

    Unachangia ndoo ya maji baharini? CCM wamebana pesa za wanachama wa Desi sasa wanajifanya kuchangisha ili kujustfy matumizi manono wakati wa uchaguzi.
    Wasanii mnachangia au mnajiandaa kula tenda wakati wa kampeni? Nature mzigo huo unakuja changia changia si zitarudi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2010

    CCM WANGEFANYA KUSAIDIA JAMII KAMA KUSOMESHA WATOTO YATIMA, KUJANEGA MASHULE NA ETC TUNGEKUWA MBALI SANA, SO I WONT TOA MCHANGO WANGU NOT FOR THIS CHAMA ANYWAY! TUMETESEKA VYA KUTOSHA, NA TUNAENDELEA KUTESEKA. GOD BLEE TANZANIA

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2010

    hivi hii michango ni kwa ajili ya nini hasa???
    1.yani kutunisha mfuko
    2.kuendeleza miradi....
    3.kulipia safari zao
    4.uchaguzi mkuu october
    5.........

    ni zoezi endelevu????au

    nielimishwe

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2010

    Nyie mmechangiwa T-shirt kuwauza wabongo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2010

    Mimi nawaunga mkono 100% wasanii hawa. Mwaka jana na juzi nilikuwa Kenya nikaona mwenyewe athari ya jinamizi la ukabila. Nikaweka nadhiri kuwa nikirudi nyumbani nitaiunga mkono CCM kwa sababu, licha ya mapungufu yake, CCM NDICHO CHAMA PEKEE TANZANIA NZIMA KINACHOTUUNGANISHA WATANZANIA WA MAKABILA, DINI NA RANGI ZOTE. Period. Hivyo vyama vingine vina harufu ya ukabila. Tumeona vingine vimekwishaanza udikteta kabla hata havijaingia madarakani, je, vikiwa serekalini si itakuwa disaster! Wewe anon wa kwanza kabisa, wewe umeanika chupi yako yenye kinyesi hadharani kwa kuwatukana hawa vijana. Just accept it!!! You'll never get everybody to follow your whims simply because your uppity comeuppance makes your twisted ego think so!!! (Ama kweli wahenga walisema "Ulimi hauna mfupa" na "aliyeamua kukutukana hachagui tusi"). Wewe anzisha chama chako au jiunge na vyama vya upinzani, si kutukana watu ovyo kwa sababu hawakufuati wewe "mfalme" kalumekenge. Sitakutukana kwa sababu mindset yangu haifanani na yako hata kidogo. By the way, nimesoma zaidi yako, sifanyi kazi serikalini na...NITACHANGIA!!!!Ngowi7

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2010

    kuna picha ya ajabu naipata, hivi wasanii wako bongo flava tu? na aliyebuni Tangazo hili ni wazi kasomea marketing ulaya na hajakaa aangalie mazingira ya Tanzania na kujua kama aliyowatundika hapa watahamasisha kuchangia. Kazi ya vijana wawili moja mjanja anatengeneza pesa kwa ajili ya kampuni yake mwingine mtoto wa mwanasiasa anaetaka kugombea ubunge.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 19, 2010

    Jamani njaa mbaya!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 19, 2010

    wewe profesa uchwala ni wewe uliyeimba ndio mzee au kivuli chako?wapi nakaaya sumari?simple because hayupo kundini,
    NAUUNGANA NA ANONI WA KWANZA HAPO JUU KUWA UMASKINI WA AKILI NI KITU KIBAYA SANA.
    MUNGU TUONGOZE WATANZANIA

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 19, 2010

    Mchangiaji wa kwanza; ungeliishia sentensi ya kwanza tu ingelikuwa o.k.; lakini ulipoamua tu kutukana nikahisi kuwa ni wewe ndiye mwenye umaskin wa akili mpaka ukafikia hatua ya kutukana. Nadhani tukiongea kuhusu akili, mwenye akili timamu hatukani hivyo.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2010

    Daah kweli nimeamini msemo usemao kila kitu huenda hatua kwa hatua ama ule msemo wa ngazi kwa ngazi sasa baada ya hawa jamaa kusema nguvu mpya hari mpya kasi mpya na maisha bora kwa kila mtanzania ndo nagundua apa....tumepewa maisha bora tunashukuru sasa kirungu ndo hiki kinatugeukia ili maisha yaendelee kua bora zaidi kama hao jamaa apo juu wamepewa na matisheti poa kabisa ya GO GREEN sasa niwakati na msimu mwengine kama wamavvuno tunaambiwa tuchangie chama apa poa tutachangia na watavuna kura zetu kama kawaa maisha yataendelea hapa hakuna maubishi kabisa.......Mi nawatakia kila laheri na nangoja kwa hamu kauli mbiu yao ya mwaka huu sina lingine
    Mdau
    Babuu

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 19, 2010

    Mchangiaji wa kwanza; ungeliishia sentensi ya kwanza tu ingelikuwa o.k.; lakini ulipoamua tu kutukana nikahisi kuwa ni wewe ndiye mwenye umaskin wa akili mpaka ukafikia hatua ya kutukana. Nadhani tukiongea kuhusu akili, mwenye akili timamu hatukani hivyo.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 19, 2010

    kwanza nimefurahi kuikuta hii sehemu ya POST A COMMENT maana mapema asubuhi haikuwepo!!! halafu sielewi hii kitu, HIVI NI KWA NINI TUWACHANGIE HAWA SISIEM? HIYO PESA WAIFANYIE NINI? KWA MANUFAA YA NANI? WARUDI MADARAKANI KUFANYA KAZI (ya kutuletea maendeleo) AMBAYO WAMESHINDWA KUIFANYA KWA MIAKA 33?? Lakini HONGERENI VIJANA (wasanii wa 'bongo fleva') KWA KUPATA HIYO DILI. HIVI WAMEWALIPA SH. NGAPI KUWAWEKA KWENYE HAYO MATANGAZO??!!! EEH MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE WAPIGA KURA WA NCHI HII SIKU MOJA TUAMKE...

    chiggs

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 19, 2010

    mdau wa Wed May 19, 10:13:00 AM kula tano, nilikuwa nawaza hayo hayo.

    Pia kusema kweli hao jamaa ni kuwa wamelipwa kutangaza tangazo hili, ili wanyonge wenye ari na ccm wawanyime watoto wao tonge ya siku ili viongozi wa ccm wanufaike, wasafiri, wawapeleke watoto wao nje kusoma n.k.

    HIMA HIMA TANZANIA!!!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 19, 2010

    ........Sitakutukana kwa sababu mindset yangu haifanani na yako hata kidogo. By the way, nimesoma zaidi yako,........ MUHESHIMIWA MSOMI SANA NGOWI7, MBONA UNAKULA MATAPISHI YAKO MWANA?? hiyo quote nimeitoa kwenye mistari yako ambayo, kabla imetanguliwa na maneno kama (ashakum si matusi) KINYESI, kumwita mwenzio kalumeKENGE na huoni kama hayo ni matusi!!! NDO TUNACHOSEMA DAILY KUHUSU NYIE 'WASOMI' WETU KWAMBA KAMA AKILI ZENU ZIKO HIVI, HATUWEZI ENDELEA NCHI HII.......MDAU KATOA MAONI YAKE,NI HAKI YAKE, NA WEWE TOA YAKO......

    chiggs

    ReplyDelete
  16. ccm supporterMay 19, 2010

    Juhudi za CCM ni nyingi sana hata kwenye kusoomesha watoto yatima hawako nyuma. je wajua wanafunzi wenye mahitaji maaluma wamepatiwa elimu katika vituo 251 za msingi zenye jumla ya wanafunzi 20,027?

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 19, 2010

    jaman..jaman...hebu tuache kaujanja,inakupa kwel akilin kutafuta pesa ya kampen kwa njia hii...hapa tunazugwa tu,pesa za kampen miaka yote ccm huchota kwenye mashirika ya umma,imekuwaje wachangishe hivyo..hv kwa kiongozi anae jiamin kwa nini umshawishi mpiga kula kwa pesa?..hv kwa nn utaratibu huu ungefanywa kuchagia kujenga vyuo vya waalim hapa nchini ili kukidhi mahitaji..au ndio wanaona tukiwa na mfumo bora wa elimu tutakuwa waelewa na tutawabania kula zetu?..sawa bwana tumezaliwa wajinga na tutaendelea kuwa wajinga.....kuleni mmetuwahi...!..matobholwa..

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 19, 2010

    wajinga kweli njie, CCm ndio iliyowafanya muwe walala hoi, msiweze kupata elimu ya kutosha mpaka mkawa wasanii, leo hii eti mnachangia vipesa vyenu ili kuididimiza nchi zaidi. Yaani akili zenu haziwaelekezi kuwa, mabilioni ya pesa yanaibiwa kila siku na hao hao wana CCM, halafu eti kuchangia kampeni zao pia tutoe pesa mifukoni mwenu. Endelee kulala, na kweli msiamshwe mpala kesho!

    ReplyDelete
  19. CCM supporterMay 19, 2010

    Mpango wa uchangiaji kupitia njia hii ya wazi ya simu za mikononi sio tu unatokana na msukumo wa zama na mazingira, bali pia ni hatua muhimu ya utekelezaji wa dhamira ya rais alyoieleza katika hotuba yake ya kuzindua Bunge tarehe 30 Desemba, 2005, ya kuwa na “utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutafuta fedha za uchaguzi; na utaratibu halali ulio wazi, wa chama au mgombea kutumia fedha hizo.”

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 19, 2010

    Hatutataki! msifanye watu wajinga kwa hiyo danganya toto, tunajua hela zenu za kampeni mnatoa wapi, tuelezeni meremete ni ya nani, na hela zilizoibwa kwenye account ya EPA zilienda wapi ndio tutachanga.... nashangaa wasanii kama wakina proffesor J kutumiwa kwenye uozo kama huo, wamekununua kwa kiasi gani kaka... HATUCHANGII NG'O CHAMA CHA MAFISADI(CCM)

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 19, 2010

    Muheshimiwa mkuu wa blogi hi ya jamii, wachangiaji wenzangu...mimi nalitazama hili kwa mtazamo tofauti...."Ni kwamba kampeni ime anza rasmi kwa chama kiongozi cha nchi" au wenzangu mnasemaje? Wapinzani wasubiri tarehe yao itangazwe!!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 19, 2010

    Umasikini wa akili anaomaanisha mchangiaji wa kwanza siyo tusi hata kidogo, bali ni tafsiri zenu hapo zisizo sahihi. Kuwa na umasikini wa akili ina maana umepungukiwa uwezo fulani wa kuyachambua mambo kwa mapana yake na kufanya maamuzi sahihi. Mfano, Prof J na ndiyo mzee akilaani uongozi mbovu wa CCM, Mwana FA na usije mjini, akimaanisha kuwa ufukara umekithiri Tanzania vijijini na mijini n.k. Hivyo hawa watu wasingeunga mkono hizi kampeni kama kweli wanamaanisha wanayoimba. Hawawezi kuwa mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 19, 2010

    HAHAHA HABARI NDIYO CCM JUU!!! KAMA UNAPATA KERO SANA JINYONGE. HIYO NDO HABARI MDAU UKITAKA CHANGA UKITAKA ACHA.... ASANTE WASANII NIMECHANGIA PIA...

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 19, 2010

    no aducation is really bad things

    ccm wanachangiwa ili wazidi kuvimba matumbo na wazidi kujenga mijumba mikubwa

    turudi kwa wana jamii wenye njaa magonjwa no aducation kila balaa wanalipata wao wana jamii

    nani mpiga kura?
    mpiga kura wa ccm ni yule mlala hoi aliekosa chakula aliekosa elimu bora anaesumbuliwa kwa magonjwa

    kwanini anapigia ccm?
    sababu hana elimu ni mwenye njaa anahitaji hizo kilo 2 za mcehele na sukari wanazopewa kupigia kura ccm

    kwanini hawataki kushtuka?
    sababu hawajaenda shule na ni wazee sana wanaona maisha bora kwa vizazi vijavyo hazina maana kwao

    je ankal ni ccm?
    jibu yes ni mwana ccm na kada mkubwa wa chama cha mafisadi ccm

    je ankal atafikisha huu ujumbe?
    yes atafikisha ikiwa atakuwa ni mwana jamii mwenye kujali wana jamii wenzake

    je mimi mtoa mada naipenda ccm?
    no no no no ni bora kuwa jambazi wa kutumia bunduki kuliko kuwa jambazi wa siasa wa chama hicho cha mafisadi

    asante ankal
    nimimi mwenyeji wako wa ukerewe.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 19, 2010

    shule shule shule inasaidia sana. Masikini wasanii hawajui the implication of what they are doing. shule shule inasaidia kuelewa mambo,.....nchi ya politics

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 19, 2010

    Kuanzia leo nafuta nyimbo zote za wasanii waliopo kwenye matangazo hayo...du inauma sana, Njaa Mbaya Kula Ugali...yaani mmenunuliwa kwa mashati tuuu, bora wale wa sahani ya pilau...

    ReplyDelete
  27. Hizi kelele na jazba hazitatufikisha popote pale. Kama hatuungi mkono tunachoona, hatuna budi kutoa mawazo mbadala.

    Kupiga kelele kusema ukweli ni kupoteza muda; ndio hasira zitapungua lakini ukiamka kesho utakuwa pale pale!

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 19, 2010

    naungana mkono na mchangiaji hapo juu aliyesema kuwa CCM wameshaanza kampeni kiujanjajanja na wenzao wa upinzani wanasubiri tarehe ya kampeni itangazwe , duhh kaazi kweli kweli
    na hao wasanii wanajipendekeza wanajua kuwa ccm lazima washinde siku zote (kwa kuiba kura) ndo maana wanajipendekeza,WANAFIKI TU....

    ReplyDelete
  29. mtzwadarMay 19, 2010

    Hakuna kuchangia wala nini, kwani hawa CCM lazima wachangiwe na walalahoi wao kurudi madarakani?
    JK mwenyewe kasema, hata KURA zetu sie wafanyakazi hazitaki, je anataka za wakulima? kwa mradi gani?
    Miaka 33 ya CCM hakuna maji, umeme, kazi, huduma za jamii, elimu na afya.
    Wa akina Lowassa, Rostam, Chenge, Mramba, Yona, Mkapa, EPA, rICHMOND, Rada, Meremeta, Kagoda, Kiwira, Tanroad, Ubungo, NBC nk.
    Halafu eti tuwachangie wazidi kutafuna mali za umma??
    Ntakua mjinga basi kuwapigia kura achilia mbali kuwachangia!

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 19, 2010

    Jamani hawa CCM ni wezi. Nyie wasanii mnawachangishia pesa wao wanakula, wanatoa rushwa, wananunua kura, wanajenga maghorofa, n.k. Lakini na nyie pia labda wanawanunua, wanawapa vipesa kidogo vya matangazo.

    ReplyDelete
  31. Mpalang'ombeMay 19, 2010

    Ili kuwa na uwazi na ukweli, Tendwa anatakiwa kuwa na kitabu chenye namba na pesa zilizochangiwa ili kiwe public maana kuna uwezekano wachangiaji wakawa ni foreigners na kuinunua nchi. Pia mchango uwe na kiwango, mtu mmoja asitoe zaidi ya laki moja.

    Nijuavyo mimi hii gelesha ya kujustify EPA ingine in making kwa ajili ya 2010.

    Simba kashika fungua za Zoo halafu unamwambia njaa ikiuma nenda porini kawinde LOL!, wakati kuna miradi kibao inayoweza kuongezewa 10% each na kupatikana full mziki

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 19, 2010

    WIZI MTUPU HUYO LUGE ANAWATUMIA KWA NTREST ZAKE NYIE MABWEGE, MNAVALISHWA MANGUO YA CHAMA ALAFU MAISHA YENU YANAKUWA DUNI KAZI KUPIGA MIZINGA YA KUINGIA STUDIO TU... KUANZIA LEO SISIKILIZI MIZIKI YENU MAANA MMEONYESHA THE WAY MLIVYOWEPESI KUNUNULIWA EBOOOOO.

    KWA HILI MMECHEMSHA MIJITU IMEIBA RASILIMALI ZA NCHI HII ALAFU MNAJIDAI KUJINADI MMECHANGIA EBO HEBU NENDENI VIJIJINI MKAONE HALI HALISI ALAFU MUONE KAMA KUNA HAJA YA KUCHANGIA HAO CCM MWEH.

    NA MWENYE HOJA NA AJIBU HUJA HII KAMA HUNA HOJA KAA CHONJO

    ReplyDelete
  33. CCM MSITRUFANYE WAJINGA HELA MMEISHA , HIVI VIMICHANGO MICHANGO NI KWA AJILI YA KUSAFISHA MACHO ILI TUSEME NA NYINYI MMECHANGIWA , 2010 HAKUNA MMBAVU HATA MMOJA ,

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 19, 2010

    Unajua watu wengi walioandika hizi habari hata Kenya hawajafika! Tembea uone then u will appreciate CCM. Nenda Afrika Magharibi kama Nigeria na nchi zingine hakuna umeme wala maji. Kila mtu ana generato na anatengeneza umeme wake. Kila mtu ana tank na wananunua maji. Elimu kama huna pesa ya kwenda private schools umekwisha. NYIE WATU MNASEMA NIN? ELIMU, ZAHANATI, MAJI YAPO MPAKA VIJIJINI! MIMI NIMESOMA TANZANIA HADI CHUO KIKUU KWA GHARAMA YA SERIKALI WAZAZI WANGU HAWAKULIPA SUMNI MIMI KUSOMA NILICHOJUA NI KUSOMA NA KUPATA MISONGE NA SERIKALI ILINICHAGUA KWENDA SEKONDARI HADI NIKAMALIZA DEGREE HAPO MLIMANI WAPI KATIKA BARA LA AFRIKA UTAKUTA HAYA. KAMA ULICHEZA NA KUFELI DARASA LA SABA AU SEFONDARI HAKUNA WA KUMLAUMU. NYERERE (CCM) ILISEMA WATOTO WOTE WA KITANZANIA WANA HAKI SAWA YA KUPATA ELIMI IWE NI MKULIMA AU MFANYABIASHARA. SISI TULIOJAALIWA KUTEMBEA DUNIA HII NA KUONA KWA MACHO YETU HALI DUNI ZA MAISHA ZA WATU HATA MAJI NA UMEME INAKUWA NI ISSUE UNASHUKURU MUNGU KWAMBA HUKUWAHI KUONA TABU HII. MPAKA LEO VIJIJI VYOTE VINA MAJI SAFI YAWE YA BOMBA AU VISIMA. IAM PROUD TO BE A LIFETIME MEMBER OF CCM AND IAM PROUD TO TELL THE HISTORY OF THE WONDERFUL COUNTRY TANZANIA TO ANYBODY I MEET AND SO FAR KILA ANAYESIKIA HISTORY YA TANZANIA HAWAAMINI KUWA HOW COULD CCM build such a strong nation???? I wish the whole continent of Africa wangefata mfumo wa siasa wa CCM FROM 7 HOUSES, SHINA, TAWI, KATA,WILAYA, MKOA HADI TAIFA. CCM IS IN MY BLOOD AND I WILL NOT STOP TO THANK THE FOUNDER LEADERS OF CCM MAY GOD REST THEIR SOUL IN PEACE!!! WE MISS YOU FATHER OF OUR NATION NYERERE. Nisingeweza kufika hapa nilipofika bila CCM.
    MDAU IN STATES!!!

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 19, 2010

    Anyway kila mwenye akili ya kupambanua mambo anaelewa vizuri nini kinachoendelea katika siasa Tanzania.
    Wapiga kura wa CCM kwa asilimia kubwa hawana uelewa huu na ndio sababu chochote watakachofanyiwa kwao CCM DAMU.
    Marehemu bibi yangu aliwahi kulima pamba miaka ya tisini bila ya kulipwa chochote lakini hadi anaingia kaburiri alikuwa anasema CCM DAMU.
    Wanachama wa CCM wanaofahamu haya ni wale wanaofaidika na CCM kwa kufanya kila aina ya uchafu ambao sihitaji hata kuuelezea maana kila mmoja anaufahamu. Wako tayari kutumia akili yao na uwezo wao wote kupotesha jamii kama wanavyofanya.
    Kadri navyozidi kuongea naona machozi yanazidi kumwagika, bora niishie hapa.
    CHA MSINGI WATANZANIA WENZANGU TUKAZANIE ELIMU ILI KIZAZI KIJACHO KISIBURUZWE KAMA SISI WATUFANYAVYO.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  36. Prof Jei wa kunyumba, kumbe wewe ni kasuku? Nilifikiri u tajiri kiakili kumbe yale uyaimbayo hata huwa huyasikilizi wakati ukiimba? Sina cha kukuambia zaidi ya pole!

    Pole na wasanii wengine mliomo kundini. Duh, kweli nimeamini kuwa ckio la kufa halickii dawa.

    Nami pia nazifuta nyimbo zako na za hao wengineo kama muAnony wa Wed May 19, 02:35:00 PM Alivyosema. Kumbe ni madangi mtupu kadoda weee ...

    Dayasipora

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 19, 2010

    acheni maneno , uchaguzi waja ongeeni kwa vitendo......hiyo biashara tu, mbona hamna upeo? Mbona wako katika nyanja mbali mbali na hamsemi?
    Wanakubalika ndo maana wako hapo, kama unaipinga CCM fanya hivyo kwa kura yako sio maneno hadharani...mnapingana na hali halisi, watachangia wengi tu

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 19, 2010

    Wahenga hawakukosea "PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA". Kila anayenufaika na mfumo uliopo hana budi kuchangia CCM. Kila anayeteseka na mfumo uliopo hana budi kulaani kampeni hii. Upeo mdogo na kutofikiria kesho ndio unaofanya wasanii kutumiwa katika kampeni hii ya uchangiaji fedha kwa ajili ya CCM. Kwa kuwa wasanii wanahangaikia mkate wa leo hawaoni shida kutekeleza matakwa ya chama tawala. Kwao leo ni leo, kesho itajijua yenyewe! Mola ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 19, 2010

    WTF!Profesa Jay si ametoa mwimbo majuzi tu unaitwa MSILIE akimaananisha wananchi wanaoteseka walisie siku ya ukombozi inakuja!

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 20, 2010

    Huyu Barnaba wanajitahidi kumbeba lakini habebeki, hehehe ..

    CCM wanaweza kua wezi ila angalau chama kina dumisha umoja ingawa unapotea pole pole na ndio hivyo kiuchumi ndio tuna dorora , hawa Upinzani Chadema sijui CUF wakiingia ni Ukabila na udini , bora tubaki na hao hao CCM kidogo bado kina utaifa zaidi , sababu waTZ wengi unaingai siasa ili kujitafutia maisha mazuri na sio kutumikia Nchi, wote ni wale wale tuu.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 20, 2010

    HUYU ANONY ALOANZA NA HAYA MANENO HAPO CHINI NAHISI SHULE YAKE NA HIYO MISONGE NI NOTHING BUT NAIVE AND A BRAINED WASHED MINDSET.

    Unajua watu wengi walioandika hizi habari hata Kenya hawajafika! Tembea uone then u will appreciate CCM. Nenda Afrika Magharibi kama Nigeria na nchi zingine hakuna umeme wala maji..........

    MJOMBA SHULE YAKO INAWALAKINI.UNASEMA CCM NDO IMEKUSOMESHA SIVYO?INA MAANA CCM WANA KIWANDA CHA KUTENGENEZA PESA?UNGEKUWA NA SHULE MAKINI AS YOU HAVE BRAGGED YOU WOULD HAVE BEEN A THINKER WHO UNDERSTANDS HOW MONEY IS GENERATED,PESA NI ZA WALIPA KODI(WANANCHI) NA SIO MALI YA CCM.WANANCHI WANATOA KODI NA NDIO HAO CCM WAKO WANAZITUMIA,PROBABLY ONLY 20% OF THE MONEY GOES TO WHAT YOU CLAIM COMMUNITY SERVICES,80% ZINAIBWA KUJENGEA MAJUMBA MIKOCHENI B,MASAKI NA KWINGINEKO NA ZINGINE ZINAPELEKWA KUFICHWA KWENYE MABANK YA NJE,WEWE UACHE KUDANGANYA WATU KWA HUO UPOTOSHAJI WAKO WA KITOTO WADANGANYE HAO WANA CCM WENZIO,OK.WATU KAMA NINYI NDO MTAFANYA TANZANIA IEENDELEE KUWA MASIKINI MPAKA END OF THE DAY,MNAJIFANYA MMESOMA BUT VERY EMPTY,MMEJAA UBINAFSI TU,AND THATS IT.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA AFRICA

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 20, 2010

    Guys if it hurts so much....you have a simple solution....VOTE against CCM...but I doubt cause most of waTZ ni wapiga domo na kulalama tu zero action....losers!

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 20, 2010

    Mdau Chiggs, rejea posting yako ya May 19, 11:06:00. Sikuwa na nia ya kukutukana. Ni kweli nimetumia lugha Kali. kwa hilo, samahani. Mimi kitu kilichoninifanya ni-react hivyo ni wewe kuwatusi hao vijana kwa kuwaita maskini wa akili. Hilo ni tusi kubwa sana. Otherwise, sote tuna uhuru wa kutoa maoni yetu kidemokrasia na kuanzisha vyama vyetu bila kuwaita watu tusiokubaliana nao maskini wa akili. That was my point dude!!! Ngowi7.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 20, 2010

    KUMANINA ZENU

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 20, 2010

    Habari za leo wachangiaji wenzangu?
    Tangu jana nimekua nikifuatilia kwa makini Mjadala huu,,,! Mimi niliona kama ni mwanzo wa kampeni za chinichini!! na nabaki kua kwenye mtazamo huo....Ila kuna watu kwa kweli nina wasiwasi na upeo wao. Mfano huyu; (MDAU IN STATES!!!Wed May 19, 06:15:00 PM)...Unajua kuna mambo ambayo ni haki yako kufanyiwa, na wala sio bahati au privilege! kusoma kwako ni kodi za wavuja jasho na ukifikia na wewe kukatwa kodi watu watalazimika kusoma kwa kodi yako. Kuna watu wenye akili zao, wanaotoa misaada ili msome pia,,,kwa hiyo hilo la kusoma ni haki na wala usijione kua umejaaliwa saana. Sikupenda ulipotoa mifano ya nchi zenye matatizo kama nchi yako, kwa nini usitoe mfano wa nchi zilizo endelea? We kwenda kenya na Nigeria ndio unatoa shamirisho? Lazima uwe na matatizo kidogo, ulisoma nini kwani wewe? Kumbuka, mtu, chama au serikali inapokosea, ni wajibu wa kila anayeona kosa kukosoa!! sasa usifiche makosa eti kisa ulisomeshwa na huyo aliyekosea. Hebu fananisha ubora wa elimu uliyosoma wewe, waliosoma waliopita na wanayosoma wa sasa? Angalia vyuo mnavyosoma, vina nafasi ipi kidunia? vina wataalam kiasi gani? vitendea kazi je? Sihitaji kusema kitu kwenye shule za msingi na sekondari,,,Usibaki kusema tu, nilisoma shule ya msingi mpaka university! angalia maisha ya watu wa mijini na vijijini! usiangalie kijiji kimoja ulichotoka wewe,,,hii nchi ina vijiji zaidi ya 500, hivi unajua hali ikoje huko? Kuna vijiji hata kufikika ni shida, we unazungumzia uwepo wa Zahanati na maji! una uhakika? Na wewe usijitolee kauli zako za kisiasa, kama vile unatafuta nafasi ya kuchukua jimbo. Tembea Tanzania uijue vizuri, kisha ndo uje na hizo kauli zako. Halafu kumbuka, uwepo wa kiwanja kilichotengwa au jengo, hakumaanishi uwepo wa huduma. Na kuepo kwa mashimo ya visima vilivyo kauka,,,sio uwepo wa maji.
    Madau, De

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 20, 2010

    Ankal, tunashukuru unatoa fursa ya watu kujadiliana barabara. Watu wameeleza jazba na kero zao na kufikisha hoja zao. Hata hivyo, kuna mtu mmoja amevuka mpaka na kutumia tusi kubwa sana la nguoni. Huyo ni anon wa May 20, 10:18:00 a.m. aliyewatukania watu mama zao. Hili halikubaliki. Tunaomba mtu akitumia tusi la neno k.....(au kuwatukania watu mama zao) basi comments hizo zisichapishwe. Watu kama hao wamehamia hapa baada ya blog yao ya kishetani zeutamu kufa. Usiapprove comments za matusi ya nguoni. Wakitaka matusi hayo wanaweza kwenda katika blogu zao kama vile gayuniverse n.k.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 20, 2010

    Nimekupenda Ngowi7. Ubarikiwe!

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 20, 2010

    JUDAS! THIRTY PIECES OF SILVER ...

    YUDAH! VIPANDE THELATHINI VYA PESA ...

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 20, 2010

    Umaskini wa akili hawajua wanalolitangaza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...