Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akitilia maji mti wa kivulia alioupanda katika eneo la Shule ya Sekondari Maghang Wilayani Mbulu baada ya kufunguwa baadhi ya madarasa ya Shule hiyo leo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Manyara kwa ziara ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendele. Mmoja kati ya Viongozi wa Wazee wa kabila la IRAQW Wilayani Mbulu Mzee Stakislaus Sabida, akimkabidhi mkongonjo na kumkabidhi Uongozi wa kabila la IRAQW Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, mara baada ya kumvalisha Mgolole wa Vazi la asili ya IRAQW wakati alipowasili katika Uwanja wa Mbulu mjini kwa ajili ya kuhutubia Wananchi mkutano wa Hadhara leo, alipokuwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo ya Wananchi Mkoani Manyara leo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 30, 2010

    hivi kweli hawa viongozi wa nchi yetu akili zao ni nzuri kweli?viongozi walikuwa wanajua makamo wa rais, lini ataingia kwenye mkoa au wilaya yao,matayarisho ya kila shughuli yalikwisha fanywa kabla,hivyo walishindwa kutafuta kifaa muafaka cha kumwangilia huo mti, isipokuwa hilo bakuli kubwa?je makamo nae amewezaje kukubali kuchukuwa kifaa kama hicho na hakuna hatua zilizochukuliwa kwa wahusika?kweli tanzania tambarare....kaiz ipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...