Ni kawaida kwa siku za weekend wakazi wa jiji kuvuka kwenda Kigamboni kupunga upepo. Ni muda sasa kumekuwa na malalamiko ya matukio ya ukabaji katika kiunga hiki cha jiji la Dar bila ya polisi kufanya jitihada za ziada kudhibiti hali hii.
Inawezekana labda polisi wanazidiwa lakini matukio yamekuwa ya kawaida kiasi hadi ukabaji unafanyika mchana kweupe huku raia wa kigeni wakiongoza kuvamiwa wakati mwingine hata wakiwa ndani ya magari yao basi kunatokea kundi la vijana na visu, mapanga na hata bisibisi na kuwatishia kisha kuwapora. Wanapenda sana raia wa kigeni kwani wanauhakika wa kupata Camera, lap top ama pesa toka kwao.
Maeneo korofi ni eneo la Petrol Station ya Gapco hapo Ferry unapovuka tuu kutoka kwenye pantoni mkono wa kushoto, hili eneo ni hatari kwani wakabaji hujifanya wapita njia na huwa kwenye kundi kuanzia watatu hadi kumi na hufanya kazi zao kwa ushirikiano mkubwa.
Eneo jingine ni uwanja wa Machava ambao unatazamana na kambi ya jeshi, eneo hili ni hatari sana usiombee kuharibikiwa na gari au kajua kakuzamie eneo hili utajuta kuzaliwa pana wezi sana na ajabu hukimbilia maeneo ya huko huko jeshini.
Eneo jingine si mbali na hapo Machava ni pale eneo la Mikadi Beach, hapa watu wanakabwa mchana kweupee, siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu ni balaa zaidi kwani jamaa wanakuwa na hasira mnoo.
Eneo jingine ni pale wanaita Makaburini, hapo hapafai hata kwa waoafanya mazoezi huponzwa na earphones zao kwani jamaa wanakaba wanavua hata viatu vya mazoezi. Pia wanawasubiri abiria wanaoshuka kwenye basi au hata kuwapora wenye pikipiki au bajaj.
Hali ni mbaya hata kwenye fukwe ambapo wezi wanakuja na magari wana park na kubomoa magari ya watu wanaiba Power Windows, Laptops, Simu au chochote cha thamani.
Taarifa zinatolewa Polisi lakini inaishia uchunguzi, uchunguzi uchunguziiii!!, Wapo waliobahatika kupata mali zao lakini wengi wetu vimekwenda na maji.
Wizi wa majumbani ndio usiseme wanaiba na wakiingia hawana haraka wanafanya kazi zao kwa utulivu kabisa.
Wizi wa majumbani ndio usiseme wanaiba na wakiingia hawana haraka wanafanya kazi zao kwa utulivu kabisa.
Kwa mujibu wa wakazi wa Kigamboni kuna kituoo kimoja ambacho hakina ukubwa wa kutosha na idadi ya askari haikidhi haja ya ongezeko la wananchi ambao wanahamia kila uchao eneo hili la Kigamboni.
Tunaomba jeshi la polisi wengi wa wezi hawa wanajulikana ni kufanya operasheni ya wiki moja tu kwani kutoka kikosi cha Polisi Central, Polisi wa Wanamaji, Jeshi wenyewe naimani wanaweza kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi kama si kulimaliza kabisa.
Raia Mwema – na Victim wa ukabwaji, Kigamboni.
Asaalaam Aleykhum.
Aisee hii ni kweli kabisa,kwenye kuiba majumbani,kuna familia moja waliingia mpaka wakapika chai wakanywa wakawaachia vikombe tu vichafu,wanaohusika tunaomba ufuatiliaji?
ReplyDeleteUCHUNGUZI GANI HUO?JAMANIIIIIIII
bila kuchukua hatua?
raia mwema naungana kuhusu pale gapco kigamboni pale ni balaa kuna siku moja saa za saa moja jioni natokea beach na waeni wangu kutoka saudi arabia mmoja wao walimpora simu ndani ya gari tukiwa kwenye foleni ya kuvuka
ReplyDeletehio ndio BONGO TAMBARARE...hayo ndio matokeo ya GAP KUBWA BTN MASIKINI NA TAJIRI...huyu mwingine ana million $$$ mwingine hata mchana hajui atakula nini...na bado MORE TO COME...NGUVU MPYA,ARI MPYA...HABARI NDIO HIO.
ReplyDeleteMdau wa Kwanza Tehtehteh teh hahahaaha
ReplyDeleteMdau wa 3 umeongea Point...
Kigamboni Kuna siku Nimepanda Bus kushuka tu Njemba mbili nazo zikashuka na Begi la laptop..
sasa kuna njia mbili ile nataka Kupita Njia ya Kichaka Njemba zilinipita Mbele hatuwa tatu siwaoni, wakati njia ndefu sana Nikajuwa zimejificha kichakani na jamaa toka Kigamboni kivuko pale, walikuwa wanazunguka zunguka kupanda Bus nikakumbuka ndio wakapanda.
Fikira za Harakaharaka nikageuza Bahati nageuza tu Kuna Mjeshi akatokea nikafatana naye kutizama vichaka Nikamuona yule Njemba Mmoja kalala chini na Vesti yake ya G-unit walibaki sababu kuona Mjeshi ila sijawachongea.... James
acheni kusingizia umasikini juu ya ukabaji. hii inatokea hata nchi zilizo endelea. toronto time after time utasikia ukabaji. the only difference between bongo and toronto ni kwamba polisi hufanya kazi yao vizuri na most of the time hao wahalifu hukamatwa.
ReplyDeleteJAMANI WATANZANIA TUMEKUWA KAMA MAJUHA HATA AKILI YA KUFIKIRIA KITU HAKUNA NTAWAPA JIBU ZURI NA RAHISI KULIFANYA. KWANZA KIGAMBONI KUNA WAKAZI WEMA WANGAPI PILI KUNA WAHALIFU WANGAPI MKISHA PATA JAWABU AMBALO NAIMANI WANANCHI AU WAKAZI WEMA NI WENGI.
ReplyDeleteMIMI MZALIWA WA SEHEMU ZA NDALA MKOA WA TABORA HAPO ILIKUWA BALAA KWA MAMBO YA KUBAKWA NA KUVUNJIWA NYUMBA TULILAMIKA POLISI HATA MAKOO YAKACHOKA. AKATOKEA MWANANCHI MMOJA AKASEMA KAZI NDOGO TUKAANZISHA JESHI LA ASILI SUNGUSUNGU NA KUWAPA NOTICE MAJAMBAZI WAKOME VINGINEVYO MAISHA YAO TUTAYAMALIZA MAANA TUNAWAJUA. BASI SASA SIYO MCHANA HATA USIKU WA MANANE TEMBEA NA PESA MKONONI HAKUNA SHIDA TULICHAFANYA KILA MKAZI WAKAJITOLEA SHS 500 KWA MWEZI KUSAIDIA KIKOSI CHA SUNGUSUNGU CHENYE IDADI KAMA VIJANA KUMI TU. NA HAPA HAKIKA USHIRIKIANO MZURI MAANA WENYE UWEZO WAMETOA HADI ELFU KUMI KWA MWEZI. HIVYO NDUGU ZANGU HAPO KIGAMBONI FANYENI HIVYO MIMI NIKO TAYARI KUJITOLEA KILA MWEZI ELFU50.
UMOJA NI NGUVU.
Mdau aliyeongelea sungusungu kaongea ukweli.
ReplyDeleteMDAU ULIYESEMA HATA TORONTO WEZI HIVYIHIVYO YA NJE YA NJE TUNAONGELEA NCHINI KWETU SIE YA HUKO NCHI ZA WATU YANATUHUSU NINI TUWEKE YETU KWANZA SAWA. KWAHIYO KAMA MAREKANI WANAWAKE WANABAKWA BASI NA HUKU WATU WAACHWE WAENDELEE KUBAKA TU?.