Ankal,
Jumamosi Jumuiya ya Watanzania michigan TAMI iliandaa siku ya kujumuika pamoja katika kutemebelea viwanja vya maonesho ya bembea za aina mbalimbali na burudani huko Cedar Point kwenye Jimbo la Ohio.
Jumamosi Jumuiya ya Watanzania michigan TAMI iliandaa siku ya kujumuika pamoja katika kutemebelea viwanja vya maonesho ya bembea za aina mbalimbali na burudani huko Cedar Point kwenye Jimbo la Ohio.
Wanachama na familia zao pamoja na Watanzania wengine ambao walipenda kushirikiana nasi tukiwa na marafiki zetu wengine kutoka England, na Congo tuliweza kujumuika katika kufurahia majira haya ya joto kwenye viwanja hivi maarufu ambapo wenye kuthubutu waliweza kupanda bembea ziendazo kasi na kushuhudia burudani nyingine mbalimbali. Mjumuiko huu ni wa kwanza kwa mwaka ambapo TAMI imelipa gharama nusu ya tiketi na kukodisha usafiri wa kwenda huko.
TAMI imeandaa shughuli nyingine za kutuunganisha Watanzania pamoja katika furaha, umoja, upendano na udugu ambao msingi wake ni kuheshimiana, kushirikiana na kuwa pamoja katika shida na raha. Wiki ijayo TAMI inashirikiana na jumuiya za Wana Afrika Mashariki wenzetu katika kuandaa sherehe ya Siku Kuu ya Uhuru wa Marekani, Julai 4. Mwishoni mwa mwezi wa saba TAMI imeandaa vile vile burudani ya muziki wa "kukata na shoka" katika tarehe, muda na mahali ambapo tutathibitisha baadaye.
Zifuatazo ni baadhi tu ya picha za baadhi ya wanachama wakiburudika Cedar Point. Unaweza kuona picha zaidi kwenye tovuti yetu ya:
http://www.tamiusa.org
Asante
Wadau Michigan!!
Ebwana I didnt know kuna chama cha wabongo hapa michigan. Nipo Northville, MI off of Livonia, Novi na Plymouth n I didnt know kama wakurugenzi mna chama chenu hapa. What's up kuna agenda gani mpya za maendeleo? So mlienda cedar point, ba kubwa, but nilidhani Avalanche bay iko karibu zaidi I might be wrong. But anyways update website yenu na contacts ili tujue kitu gani kinaendelea. And Poleni kwa tornado warnings zinazoendelea!!Mdau Wayne County
ReplyDeleteAsante sana mdau toka Northville, tunacho chama hapa kwa muda mrefu, unaweza kujaza fomu iliyopo kwenye tovuti au kutupigia simu na unakaribishwa kwenye siku kuu ya Fourth of July at the end of the week!
ReplyDeleteKATIBU TAMI
Mdau hapo juu kaa mbali na hicho chama utachangishwa pesa za wafu kila kukicha kila anayekufa bongo wanataka mchango.Hiyo apparment yako ya Wayne county itakushinda.
ReplyDeletewe anon wa 9:39 acha kutisha watu nyau! We umesikia chama gani cha wabongo ambacho kimegharimia shughuli yake bila kuchangisha watu? As a matter of fact hata hii July 4th tunakutana kwa BBQ gharama yote inaingiwa na TAMI. Kila chama kina michango yake ya kawaida ya uanachama n.k ambayo ndio sababu kinaitwa "chama". Kama unapenda mambo ya dezo ambapo hauingii gharama yoyote ni bora ubakie huko huko uliko. TAMI ni chama cha umoja, upendo na ushirikiano kwa kila ambaye anafuata masharti yake, ambaye hataki halazimishwi.
ReplyDeleteNashukuru kwa TAMI kunikaribisha na nimewaalika wabongo wengine ambao walikuwa hawajui uwepo wake.