basi dogo aina ya Toyota Hiace lenye nambari za usajili T 185 AFD likiwa limezunguwa na wanachi mara baada ya kupinduka mchana huu.basi hilo lifanyalo safari zake kati ya Mbagara rangi tatu - Mbande lilipata ajali hiyo mara baada ya dereva wa gari hilo kushindwa kulikontroo katika kona kali sana iliyopo katika eneo ya Mwembe Bamia,Mbagala Mbande.
mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo akielekea katika gari nyingine ili aweze kuwahishwa hospital kwa matibabu.
wakazi wa maeneo ya jirani na ilipotokea ajali hiyo wakisoge jirani na gari hilo ili kuweza kutoa msaada.
wakilinyanyua gari hilo ili kuona kama kunaweza kuwepo na mtu alielaliwa na gari hilo,lakini hakukuwa hivyo na ni abiria wachache tu ambao walijeruhiwa.
gari ishanyanyuliwa na dereva na konda wake walishaingia mitini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2010

    Mwembe Bamia? Toba!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2010

    kwanza nawapa pole wote waloguswa na hii ajali, pili tuzingatie sherea za usalama barabarani jamani chonde chonde!

    alfu ankali tuweke ishu za brazil na stars basi! au ndo mambo ya exclusivity!!!??

    ReplyDelete
  3. MAWAZO YANGU.....IN ADITIONAL TO KUWACHOMA MOTO VIBAKA, MADEREVA WAZEMBE PIA INGEBIDI WAKIKAMATWA WACHOMWE MOTO VILEVILE. HII INGESAIDIA MADEREVA KUWA MAKINI ZAIDI...HAYA NI MAONI YANGU TU.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2010

    samahani nipo nje ya mada, anayetaka kuangalia mechi ya tanzania na brazil aende www.tanzaniaireland.blogspot.com

    ReplyDelete
  5. Madereva wengi wa bongo hawana akili au hawazitumii walizo nazo.Utaendeshaje kwa kasi sehemu yenye mkunjo(curves) au utakataje kona kwa kasi? Ajali nyingi zinazotokea bongo sio kama haziwezi dhuirika bali ni upumbavu na ujinga wa hawa madereva mbuzi wasiozingatia sheria za barabarani au kujua kuwa huwezi kupush vehicle beyond its capability. Habari ndiyo hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...