Ankal nanihii salaamzzz...
Napenda ku-share na wadau hii kitu wakati Tanzania ikiadhimisha siku kupinga vita madawa ya kulevya duniani. Yaani wapo watu kama hawa ambao muda wao wa kutafuta fedha ulishapita.Swali ni je, anatumiwa kwa ajili ya manufaa ya kwake au ya watu wengine?
Mdau wa Globu ya Jamii,
J.J. Lyimo
Bi Kizee mwenye umri wa miaka 94 akiwa kabambwa na kago la bangi lenye uzito wa kilo zaidi ya 10 akiwa kajifunga mwilini huko Nogales, Arizona, Marekani. Hii inadhihirisha kwamba sio tu kazi ya kubaini wanaosafirisha madawa ya kulevya si ndogo bali pia wanaofanya kazi hiyo si lazima wawe vijana
Ukaguzi ukianza
kago alilokutwa nalo bibi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2010

    Hilo ni kweli lakini pia kama wasemavyo "THIS IS AN ISOLATED CASE"

    Pia ni kweli kwamba tatizo hili sana sana lipo kwa vijana zaidi kuliko wazee. Ila swala ni kwamba bali na usawishi pia umaskini unachangia kwa kiasi kikubwa tatizo la madawa na usafirishaji wake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2010

    Haya Matatizo wengine wengi wanafanya kwa ziki ya pesa Ukiwacha wale kwa ziki Ya Njaa wengine wanatoka familia tajiri na hili wanafanya... Ila wengine hasa vijana wa kike wanadanganywa.

    VIJANA WENGINE NIMEONA WANALAZIMISHIWA MZIGO THEN WANAWATUPA TU AIRPORT WAO WANAKIMBIA WAHUSIKA..

    HUYU BIBI MZIGO WAMEMUWEKEA KWA LAZIMA NA KUMSHUSHA AIRPORT WAHUSIKA KUKIMBIA SIZANI KAMA HUYU BIBI KATAKA KUFANYA HIVYO.

    MZ.

    ReplyDelete
  3. Bradha mbona naona hao wanaompekua kama ni wanaume vile!?!

    Kwani hata kama ni mhalifu hana haki zake za kimsingi za kibiinadamu jamani!?!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2010

    Pure mjasiriamali....

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 28, 2010

    Awekewe kwa ulazima si angejipeleka mwenyewe kwa officers usalama wa airport? Au utatuambia kuwa kajukuu kake kameshikiliwa mateka? Kwa taarifa yako wazungu wazee kibao wanabeba unga tena ktk masanduku, namshangaa huyu kajivika, ndo maana kashtukiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...