Home
Unlabelled
baraza la mawaziri leo dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
JK Unampya? ama ndio maelezo mtelezo ya kumalizia ngwe?
ReplyDeleteNatumaini wana discuss matatizo yetu, kuuzwa kwa open spaces, matatizo ya umeme, maji, afya, elimu, barabara, rushwa, huduma kwa jamii, usafiri, foleni, kukata matumizi ya serikali kwa kuondoa na kuyauza mashangingi yote, kukata posho za mikutano (maana wanalipwa mishahara!).
ReplyDeleteNatumaini JK anawapiga mikwara kuwa walalahoi wamecharuka, wanataka haki zao, na kiongozi asiefanya kazi yake lazima ale vumbi!
Natumaini JK analalamika wamemwangusha, akisafiri na kuwaachia nchi wao wanajirusha na kuwa lege lege!
Naapia ni lazima haya yameongelewa, AU?
mwana hapo kinachojadiliwa ni jinsi gani wataendelea kuwepo kwenye bunge lijalo... yaani kweli wamechosha sana hawa jamaa.... kweli kama utapata kuyajua wanayozungumza unaweza kutapika ama ukashikwa na kizunguzungu...
ReplyDeleteMmmmmh sijui kama wanaongelea hayo! Kwa vile ninavyowajua. Wengine ni mawaziri lakini hata majina hatuwajui, ujue hawafanyi kazi.
ReplyDeleteThe late President Kennedy once said: " Ask not what your country can do for you - ask what you can do for your country". Tuache kufikiri tu eti serikali ndio itaweza kututafutia chakula cha asubuhi na mchana, kututafutia kitanda, chandarua, sigara(?). yes, they do have responsibilities, but at the end it's each for him/herself. that's the reality of life. take it or leave it. Even in the USA no government has been baby sitting it's citizens. Watanzania tumezidi utegemezi. Tuondoe uvivu na maisha yatapabazuka. Angalia wenzetu waChina walio Dar. Mtu anakuja masikini toka kwao China, anaanza-kumachinga barabarani for a few months, and then huyo keshafungua duka na maisha yananyooka tambarare. Akina sisi tunabaki tunamachinga pale pale kona ya trafiki laiti miaka nenda miaka rudi. Don't blame JK or the ministers, look in the mirror!
ReplyDeleteAnanymous 09:50 am
ReplyDeleteWananchi wanaweza kuisaidia nchi kama viongozi wa nchi wanafanya kazi yao, kama viongozi wameendekeza rushwa, kununua magari ya kifahari, kuwa na mijengo kadhaa, kusomesha watoto wao nje huku wakijua elimu ya apa haina kitu na hawafanyi lolote, kutibiwa wanaenda nchi za nje wakijua ni swala la kurekebisha elimu ya nchi yao na kujiangalia wao tu na familia zao katika kupambana na matatizo ya nchi huku wakiwaacha wananchi bila huduma muhimu na za lazima.
Huyi uliomnukuu ni hayati President Kennedy wa Marekani, lakini tujiulize, je wakati anasema ivyo Marekani ilikua kama sisi? Kwamba umeme, maji, afya, barabara na huduma za jamii ni kama hakuna?
Sio kwamba hela za kufanya haya mambo hakuna, la, zipo, ila zinaliwa, sasa wewe unataka mwananchi wa kawaida afanye nini? Maana kazi yake ni kutoa kodi kwa kufanya kazi, kununua bidhaa na kulima, serikali inapata malipo yake hapo na inatakiwa kuwajibika kwa kutumia hayo malipo vizuri.
Wale wanaokaa vijiweni na kuangalia magari na kusogoa maneno siku nzima nakubali ni wavivu na dawa ya kuwasaida hawa ni ujarisirimala mdogo mdogo ambao nawe natumaini umesoma ripoti jinsi mabilioni ya JK yalivyotumika, AU?
Sidhani hata ulaya wanaweza kutushinda kwa ujasirimala mdogo mdogo, walalahoi wanahangaika sana na kutafuta maisha bila kuwa na msaada wa maana kutoka serikalini, lakini wewe uliowanukuu hebu jiulize kama viongozi wa nchi zao wako kama wetu? Na wanawasaidiaje walalahoi wa nchi zao.
Usije na manukuu ya kutoka nchi za watu bila ya kuwa na data na kuanza ku comment bila kutumia akili!