Jaji Mkuu Mh. Augustino Ramadhani akimkabidhi hati ya uwakili Rhidhiwani Kikwete leo asubuhi Mahakama kuu jijini Dar. Jumla ya mawakili wapya 128 walipatiwa hati zao leo
Mama Salma Kikwete akiwa na Majaji pamoja na baadhi ya mawakili wa kujitegemea waliopata hati leo

Jaji Mwendwa Malecele akiwa miongoni mwa majaji waliohdhuria sherehe hizo
Mdau Lilly akielekea kupiga picha na waheshimiwa majaji
Hongera sana kijana anasema Mh. Said el Maamry kwa Ridhiwani Kikwete
Waandishi wakimpiga maswali Ridhiwani
Baadhi ya wadau waliopata hati za uwakili leo
Riwdhiwani akiwa na nduguze
Ridhiwani na wadau
Hongera mwanangu anasema Mama Salma Kikwete huku Jaji Mkuu Mh. Augustino Ramadhani akishuhudia
ankal naye alikuwepo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 55 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2010

    Vikwete Kibao kama photocopie!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2010

    Hivii,ktk hao 128wote waliomaliza ni mmoja2ndo anafahamikaa au...,ndo kusema ye kazi2ma4fotoz zats y anarushwa kiasi hicho..,au kuna uspecial flani ktk hiyo degree yake...,pengine family names nazo ni muhimu kuwa nzito ili upeperushwee,jst mtazamo2kwa jinsi suala zima la hii habari ilivyokaakaa.
    Jaribuni kuwa na usawa wa news!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2010

    hakukuwa na watu wengine? namaanishwa mawakili wengine? maana ni kikwete familiy tu lol... tayari huyo ni superstar sometimes you have to put mtu hata kama mmjui jamani acheni kupendelea

    mdau

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2010

    Jaji Malecela kavaa ndala ama?????????????

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2010

    huyo huyo anakuja huyo ohhhhh ...... kwani 2025 mbali basi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2010

    HONGERA RIZ!!

    Huu ni mfano mzuri kwa wabongo wenzengu ambao wakiona Baba/ndugu flani kapata kidogo tu (hata ujumbe wa nyumba10) wanona wamefika na kunabweteka kabisa.

    Hebu checkini mtoto wa Prezidaa,kila kitu home kipo, hata kama asingekuwa na kazi angeishi maisha mazuri sana tu,lkn kakaza buti kapata Jiwe lake lingine ziadi ya lile la UD.

    Ndo hapo sasa akipata pande la ukweli, watu wanaanza kuchonga ohoo..kapewa cheo na Babake,ohoo..karidhishwa madaraka n.k. Sasa mtu kasoma kwa bidiii sifa zote anazo mnataka nini..!!Acheni tuzidi kutawaliwa na koo flani flani tu kama watoto wetu tunawabwetesha na visent vdogo tunvyopata badala ya kuwakazania na shule.

    Hongera sana Ridhiwani, waTz tuchukulia hii ni challange na mfano wa kuigwa kwetu sote,na sio wivu na fitina.

    Mtanzania Halisi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2010

    Ah, Miraaajiiii!

    Si ndie huyo alievaa kaunda Suit ya Kijivu? Au nimemfananisha?

    Jamani huyu kaka ni handsome, yaani wee acha tu.

    Hongereni sana Mawakili.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2010

    Samahani ankal, hii sherehe ilikuwa ya kumpongeza Ridhiwani au ilikuwa ya kuwapongeza Mawakili? Liweke wazi tafadhali sijakupata vyema..maaana kichwa cha habari kilisomeka: MAWAKILI WAPYA 128 WAPAT HATI ZAO LEO. Labda uniambie Ridhiwani a.k.a yake ni MAWAKILI WAPYA 128.
    Mdau M.A

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 24, 2010

    Bwashee MIchuzi, mbona mnampa sana publicity huyu kijana, kwani ni yeye pekee amegraduate huo uwakili!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 24, 2010

    Jaji Malecela kavaa nini miguuni jamani au ni macho yangu?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 24, 2010

    Kweli nisingependa kupata uwakili katika siku hiyo. Inaonyesha kila mtu alikuwa anampa-Mtoto wa Kikwete attention utadhani wengine wao hawakwenda shule..Including wewe Michuzi hapa kila picha inamuongelea mtoto wa Kikwete...hivi kweli huo ndo uzalendo wenu? I hope utatoa hii comment maana nawewe wakati mwingine una mambo...!! Sasa jamani hao wengine na si wamesota tu....? mbona ku-focus kila kitu kwa mtoto wa Kikwete na kuwafanya wao wasijisikie vizuri siku ya kuvalishwa kwao magwanda? Jamani na waandishi wote wamewa-ignore hao wengine..uzalendo gani huo? Au ni kujigonga? Haya mithupu usiiache hii comment.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 24, 2010

    Topito nakuona hapo mzee unang'aa...kumbe ulikuwa unawahi hilo..
    Mdau CPT

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 24, 2010

    Te he, Te he!

    Eti Vikwete!

    Wabongo!

    Mi ni hichi Kikwete Mi-nanihii tu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 24, 2010

    Bila ya shaka bw. Michuzi amekusikieni wana blog na hisia zenu. Ukisikia chombo binafsi ndio hii michuzi blog. Reginald Mengi nae alisemwa kwa kutumia TV yake ya ITV vibaya na kujipatia umaarufu. Sasa huu ndio mtaji wake Michuzi. Mimi binafsi ninauhakika vitu kama hivi havifanywi bure. Alialikwa na kulipwa fedha ili afanye coverage sasa mwisho wake ndio inakuwa karaha ukilinganisha na kwamba picha zimefocus kwa mtu mmoja. Hisia za Wazanzibari Ridhiwani asisahau kuhusu Umoja wa Vijana na Masauni. Bw. Masauni hakutaka kugombea lakini wenye CCM waliandaaa utaratibu wa kumpa uongozi na mwisho Ridhiwani kuongoza genege la kumngoa. Sasa hizi picha asione ni ni umaarufu kwamba na yeye atakuwa Rais siku moja. Tanzania inabadilika na watu wameamka. Unatoa fedha nyingi ili utokee kwa michuzi ili uwafunike wote ambao wametunikiwa vyeti. Michuzi inabidi utumie common sense ili blog yako/yetu irindime zaidi. Wewe ni mtu wa watu usiwe fanye mambo mpaka ikawa karaha .Tumia uzoefu wako vizuri kuweka mambo katika balance.Nategemea uanifahamu kwa upendo.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 24, 2010

    Jamani acheni maneno, mara ngapi misupu anaweka graduation ya chuo anataja jina la chuo lakiini picha anaweka ya mtu mmoja aliyegraduate, mmesahau kama michuzi ni mpiga picha labda kapewa tenda na ridhiwani hao wengine hawajampa tenda,

    Good job ridhiwani, keep it up ma men
    Mdau
    USA

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 24, 2010

    miraji umependezaa sasa na wewe ukaze buti kama brother ili huo u handsome wako uendane na nondoz wee ingenoga kweli

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 24, 2010

    mnalalamika nini kwani hamjui kuwa mkono mtupu haurambwi? mtajiju

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 24, 2010

    This belongs to Michuzi and he can publish what he wants.This is not a newspaper.Hongera mawakili!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 24, 2010

    mlaumu baba yako kwa nn hajawa raisi acheni wivu usiokuwa na maana..mnachoshangaa nini huyu kupigwa picha mbona tumeona michuzi kawaweka wa2 wengi sana kwenye hii blogu tena walewale akina chibiliti...mboona wengi 2 wanawekwa humu na hamlalamiki..kingine mnatakiwa muelewe huyu ni mtoto wa rais na lazima takuwa na priority hata km yeye hataki kuwekwa kwenye habari...

    ReplyDelete
  20. MICHUZI NI MBABAIKAJI SIKU ZOTE, KWA WASIOMJUA MICHUZI. MICHUZI ALIKUWA MPIGA PICHA WA GAZETI LA SERIKALI HAKUWAHI KUSOGELEANA NA WAKUBWA WAKUBWA. ALIPOKUJA KUWAJUA IKAWA MATAKO KULIA MBWATA. WATU 128 WAMEPATA VYETI UNAENDA KU KISS BUTT YA MTOTO WA KIKWETE NA WADOGO ZAKE. MAONI YA WATANZANIA HAPO JUU IKUONYESHE KWAMBA WABONGO SIO WABABAIKAJI SIKU HIZI. MKUBWA OVYOOO..

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 24, 2010

    Hii ni mbaya sana kwa umoja na mshikamano wa nchi yetu yaani watu 128 woote si kitu ila familia ya JK. Mbona wakati wa Mkapa, Mwinyi, Nyerere familia zao zilikuwa off public view?. Au ndiyo mashikolo mageni kama wengine wanavyosemaga, yaani ukoo watumia mgongo wa "The President of URT" hicho ni cheo ambayo ni dhamana, Nilitarajia kuwa watu 128 wote ni sawa bila kujali ni watoto wa nani.

    Yaani mpaka Jaji mkuu ana-feel responsible kwa uwepo wa familia ya bosi wake.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 24, 2010

    wadau hapo juu sikilizeni bwana sio mnakurupuka tu na kusema yasio na maana siku zote watu maarufu ndio wanapendezesha habari au picha au matukio,hapo ridhwani kikwete ndio selebrity nani zaidi,mdau makambako.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 24, 2010

    Hongera sana wote,Namsifu Ridhiwani kwani ni mtu wa kukaza buti shule tangu looooong time, sio jana wala leo.hongera sana.pia wabongo acheni kuchonga kwakuwa katolewa sana kwa michuzi,mbona kuna wengine pia huwa wanawekwa kwa michuzi wakimaliza nondoz zao,na pia huwezi kujua labda wengine hawakupenda watolewe kwa michuzi.pia ana jina kubwa thats why, hata wewe ungekua mtoto wa prezidaa ingekuawa hivyo,yani unapata attention everywhere in everything you do.nnachosikitika ni kwamba bongo tuna wanasheria kibao lakini hakuna haki hata kidogo.wanyonge wanaonewa zaidi when it comes to sheria.inasikitisha sana.
    mdau washington

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 24, 2010

    RIDHIWANI YUPI WA IKULU AU MPIGANAJI? MAANA WAKO WAWILI HAPO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 24, 2010

    Ridhiwani....Malecela...so what! kwani ndio peke yao!

    Hata huyo Salma kaa yake hapo pichani ni kama mmojawapo ya mawakili!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 24, 2010

    Mwambie dada mwendwa,tunampenda sana.. lakini siku nyingine, asivae viatu hivyo.. anaweza kanyagwa bure..afla kama hiyo inawatu wengi

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 24, 2010

    Wadau kwani hamjui kuwa Michuzi ndio zake kujipendekeza kwa kina somebody fulani. mara utasikia dada Mwamvita Makamba, mara kaka January mara kaka Mafuru mara dada Shyrose ilihali hao wote ni wadogo kwake sababu kubwa wana majina fulani au wapo sehemu fulani nyeti. inawezekana hapo alimuamkia huyo dogo Ridhwani. Michuzi kumbuka utu wa mtu unashuka pale anapojidhalilisha yeye mwenyewe. ni ushauri tu bure sababu Michu mimi ni ndugu yako tumekuwa wote Aggrey ukibania comment hii sawa tu lakini ujumbe utakuwa umeshafika .
    mdau Pakacha UK.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 24, 2010

    Sio ndala, ndala ni za kuogea bafuni bali hizo ni 'sendoz' aka sandals. Hakutakiwa kuvaa sendoz na gwanda anyway, lol

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 24, 2010

    Tusidanganyane bwana, kubebana bado kupo kwa sana tuu, huoni hata picha ni zake nyingi (Ridhiwani Kikwete) kwani yeye tu ndio yuko kwenye kikundi? Ningemshauri Ridhiwani atafute Identity yake, baba yake anapendeza akicheka lakini ni natural, yeye anakuwa anai-force tabasamu, wakati mwingine mtu kuwa hajacheka sana inaonyesha ujarisi fulani na sio kila picha wenzake wanaonyesha kicheko anachoangua. Unaweza uka-stand-out kwa wewe kuwa na tabia na mguso fulani sio kama wa fulani tuu vile umeambiwa mnafanana na nibaba yako, mimi sioni kama mnafanana hiiivyo, sijui wengine wanaangalia wapi, au ukipenda chongo unaita kengeza ahhh

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 24, 2010

    yes kavaa ndala kwani?:)kwi kwi kwi

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 24, 2010

    Michuzi acha kujipendekeza.Hii ni globu ya jamii, sasa mbona umempendelea Ridhiwani.kwa kuwa mtoto wa mkubwa au?

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 25, 2010

    Huyu si ndio mjumbe wa halmashauri kuu au wanafanana tu nakumbuka yule wa halamashauri kuu alikua anasoma sijui UK aualisoma UK...Hebu tuelezee vizuri sio kuweka picha tu kama vile tunawajua kama sala kwa vile ni watoto wa KIkwete...

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 25, 2010

    Ok, kwa hiyo ile harusi ya Chelsea Clinton inavyotangazwatangazwa mpaka hata CNN ina maana Marekani hakuna harusi zingine????????

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 25, 2010

    Michuzi mbona hujaweka picha za mtoto wa jaji mkuu Augustine Ramadhan na yeye amepata uwakili siku hiyo ???????

    ReplyDelete
  35. We Michuzi acha UFALA wewe!

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 25, 2010

    WEWE MICHUZI ACHA HIZO.....MAMBO YA UKOO KURITHI HII NCHI YAMEPITWA NA WAKATI NDIO MANA ZANZIBAR TUNAMPA SHAIN NA COME 2015 TUTAMPA SHIBUDA. HIYO VCCM NA UWT HAZITUHUMIZI KICHWA.HALAFU HUYU SI ANA MKE MBONA HAONEKANI AU YUKO MARTENITY????MANA KWENYE PICHA NI MAMA NA DADA AU BADO NI WA MAMA.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 25, 2010

    Heri mimi sijasema.

    Lakini mbona hata waandishi wa habari wooote wanamhoji RK ina maana na wengine waliojiwa hivyo?. Msimwonee Michuzi kama angeweka PICHA ya Kayumba nafikiri comment hizi zinazoanzisha siku yangu vizuri leo zisingekuwa nyingi hivi. Nimecheka saaana na Michuzi kakua maana hata comment zinazomkandia kaziweka. HONGERA MICHUZI na MAWAKILI.

    Observer

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 25, 2010

    Mmesahau kuwa:
    i. Aidha Michuzi kalipwa na Ridhiwani, au
    ii. Hata kama hajalipwa, taaluma yake ya uandishi wa habari inamlazimisha kutoa 'attention' kwa Ridhiwani maana kwenye taaluma hii inajulikana kuwa 'BIG NAMES MAKE BIG NEWS'.
    Halafu huyu dogo ni fighter wa ukweli, ana network zake za ukweli hata kabla dingi hajawa prezidaa. Waulize wa Faculty of Law-UDSM

    ReplyDelete
  39. Sitaki Kura za wafanyakazi - JKJune 25, 2010

    Mishupu kichwa cha habari nahisi kimekosewa kutokana na coverage ya picha.. badala ya kuwa """"mawakili wapya 128 wapata hati zao leo"""" kilitakiwa kuwa "" Ridhiwani Kikwete apata hata ya uwakili leo""" au wadau munasemaje?

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 25, 2010

    Ankal nakusifu kwa kuziachia comments ....maana jamaa wamekunanga kweli! ukweli hata mimi nilipoona hizo picha, nikasema ....khaaa hii ni zaidi ya mnoo! kumbuka ku balance kaka!

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 25, 2010

    michuzii kama kuna picha nyingine zaidi letaaa, hata mwewe akiwa angani vipi huona kuku mweupe tu ingawa kuna makuku weeengi lakini mwewe anafata ile kuku nyeupe tuu, shee!!

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 25, 2010

    Hongera sana Ridhwani...wewe ni mfano kwa watoto wote wa kishua tulioshindwa enda shule tukitazamia mali za wazee. Natamani ningekuwa na busara na werevu kama wako, pongezi kwa mh. kikwete pia kwa malezi bora.

    Kaka mithupu ahsante kwa post iyo, labda ungewabidilishia tu wadau iyo heading (Title), imhusu ridheani pekee. Tatizo watu hupendelea watu maarufu waandikwe ktk media for wrong reasons only..hii sio sawa.

    Shukrani!

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 25, 2010

    acheni kuficha moto kwenye makaratasi km uspecial ndo umefanya arushwe hv zaid ya wengine na ankal obvious utakuwa ndo umerahisisha apate uwakili kwa wepesi mbona watu kibao wanafel iweje yeye

    ReplyDelete
  44. Hongera Uncle Mh.Anthony Malisa!!!

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 25, 2010

    Sasa mnataka Ankal akale Polisi?

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 25, 2010

    Miraj shavu shavu..u look great mwana!

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 25, 2010

    Kinaumaa! kinaumaa! kiroho kinatuumaa! Na bado kiroho kitatuuma!

    Watu wengi tumezoea kukandya watoto wa wakubwa kuwa hawataki kusoma, wakisoma ooh wamepelekwa nje kusoma bongo wangeshindwa. Sasa huyo Ridhwani wakati baba yake akiwa waziri wa mambo ya nje na waziri muda mrefu tu serikalini yeye na dada yake Salama wamesoma UDSM na Muhimbili.

    Na huyo anayeuliza kuwa wengine wanafeli basi na Ridhwani afeli, kwa taarifa tu Ridhwani LLM (Masters of Law) yake kaipatia UK ambako hakuna kupewa maksi kwa kuwa baba yako ni Rais!

    Kinaumaa kiroho kinatuuma, kinaumaa kiroho kinatuuma! Hongera Bwana Ridhwani kwa kuwa wakili, sasa mpe nafasi na mkeo nao apate Master yake na yeye ya Law ili tuongeze wanawake wa wakiswahili wenye elimu ya maana!

    Mswahili!!

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 25, 2010

    Sasa jamani kelele zote za nini, post ndo hiyo imeshatoka, sioni tatizo kuweka attention kwa Ridhwani maana pengine ndiye aliyemjua na akaamua kuanza naye, Niwaulize nyie walalamikaji, Michuzi amewaambia amemaliza coverage ya tukio hilo? Akileta nyingine za msiowafahamu mtacomment kitu gani, acheni wivu wa ajabu nyie, Michuzi kazi yako tunaifahamu kwanza umetujulisha na sisi tuliokuwa hatufahamu habari za RK we chapa kazi kama kawaida wachongaji endeleeni kama kawaida yenu, mmeumbwa mchonge msipofanya hivo mtaugua.
    Big up michuzi
    Mdau
    Uholanzi

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 25, 2010

    Njaa mbaya..............

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 25, 2010

    Labda huyu ndo mtoto pekee wa JK kumaliza chuo,sabu kama sio hivyo zen waaat,waTz wangapi ni mawakili orede na washafanya mambo mengi2makubwa ila hawapewi publicity like zaat!!!???
    Halafu zile sura na kamera zao zilizomzunguka huyu dogo na kuwapa kisogo wale127waliobaki hazijish2kii kuwa zinajichoresha na kushobokea li-surname la huyo mtoto au....?????

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 25, 2010

    Hello Ankal.

    Napenda kuchukua fursa hii kama mtanzania nilyesoma, si shule za kubahatisha bali ni shule za Kweli, nikisema shule za kweli si maananishi kuwa zile za kupia kwa dola au FM academia, la hasha ila ni shule zetu hizi hizi, nimefanikiwa kusoma shule na hawa watoto wa wezetu wakubwa, akiwepo Ridhiwani na kuwa naye katika uongozi wa Daruso yeye akiwa mweyekiti wa Faculty of Law.

    Huyu kija amekuwa akipewa promo tangu akiwa secondary kwa kofia ya baba yake na wal si kingine, pale chuo alipata uenyekiti wa sheria kwa ajili ya kumsaidia baba yake kwenye kampeni za uraisi kwa kilikuwa ni kipindi karibia na uchanguzi, sijawahi kuona kipya kwa huyu kijana pamoja na baba yake zaidi ya maneno na porojo.

    Hakika mpaka sasa kijana amekuwa ni zungumzo kwenye vyombo vya habari kasi kwamba inatia aibu kwa vyombo vya habari kuconcentrate na habari za Rhidhiwa wakati kuna watanzania wengi ambao wanashinda na taarifa zao haziandiki magazetini wala kwenye blog kama yako ili wapate kusaidia shida za mablimbali zinazo ikabili jamii yao.

    Mwaka 2005 to 2008 nimetembela maeneo mengi sana Tanzania, ambay hata waheshimiwa wetu wengi hawajayafikia iwe kwa magari ya ya gharama ama kwa helicopter, hakika watu wanashinda sana, hakuna barabara, MAJI, kila kitu ni hakuna,, wananchi wanachojua ni kula na kuzaa tuu, hakuna cha NGO yeyote ambayo ishawafikia jamaa hawa.

    Watu kama hawa ndiyo tunahitaji habari zao na wala si siasa za kufagiliana kwa sababu baba yako ni rais au waziri.

    Kuna mambo mengi ya kijamii ambayo tunahitaji habari zake, kuna matatizo ya ujambazi kwenye border na nchi za jirani kama Rwanda na Burudi, maeneo kama Muhange, Nyauronga etc watu wanaimba gunia la Mahindi kwa bomu la kurusha kwa mkono, tunahitaji habari kama hizi.

    Hakika Ankal ulijitegenezea jina sana pale mwanzoni, mimi binafsi nilikuwa lazima nifungue blog yako hata kama nipo nje ya nchi, kuna kipindi nilikuwa nchina na wameblock google service ilibidi niwaambia jamaa zangu wa bongo waniletee kwa kama pdf web yako, hii yote ni kwa sababu nilikuwa napenda habari zako kwani zilikuwa zimejaa jamii ila kwa saasa sioni umuhiwa wa kuwa ndani ya blog yako mara kwa mara kwa sababu imejaa kuwafagilia waliyoko madalakani.

    Sijui tatizo lipo wapi, ila nahisi kama wanakulipa kufanya hivyo kwani umekaa kibiashara zaidi.

    Hakika mtawafagilia sana ila siku yaja amabapo hata wao watajua kuwa hawana nafasi tena katika nchi hii, nani ajuaye ya kesho.

    Wako,
    Mtanzania halisi

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 25, 2010

    WENYE MAONI HASI WIVU UMEWAJAA, NYO! NYIE MMEKATAZWA KUGOMBEA?

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 25, 2010

    Tarehe Fri Jun 25, 06:11:00 AM, Acha umbeya na udaku na hujui unalosema..shut up...Nani kaonyesha harusi ya mtoto wa Clinton..Hajaolewa bado get the facts right.

    Watu wakisema ukweli wengine ni kutetea kwa umbeaya ndio maana hatuendelei watu wakisema ukweli mnaona wivu.....

    Kamau where are you?

    ReplyDelete
  54. AnonymousJune 25, 2010

    Hongereni wasomi mbarikiwe mmje kufanya haki si tena marushwa rushwa.daah huyi kaka aliebeba ua haandiiisam

    ReplyDelete
  55. AnonymousJune 26, 2010

    Pongezi nyinyi wote na Mwenyezi Mungu awabariki. Amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...