Bi Kidude Live in Dar

Bi Kidude akila tizi na DCMA katika kujiandaa na safari ya Poland wiki ijayo
Bi Kidude na ataosafiri nao kwenda Poland wiki ijayo

Msaanii maarufu nchini, Bi Kidude binti Baraka, akiwa na kundi la Taarab la DCMA kutoka Chuo cha Muziki Zanzibar anategemewa kuwakilisha muziki wa Tanzania katika Tamasha la Muziki lijulikanalo kwa jina la Brave Festival litakalofanyika mjini Wroclaw nchini Poland kuanzia Julai 2 hadi 9, 2010.

Mweledi huyo wa Taarabu asilia pamoja na ngoma ya Unyago atasafiri Jumatano ya tarehe 30 Juni akiwa na kundi la wasanii sita wa muziki wa Taarab asilia kutoka Zanzibar wakiwemo Mahsin Basalama (Ngoma), Mohamed Othman Faki (Violin), Ismail Muhsin Ali (Oud), Ali Kassim Ali (Violin), Maulid Haji Mkadam(Qanun) and Fatma Juma Shamte (Sauti).

Akiwa nchini Poland, mkongwe huyo wa chati za muziki wa Zanzibar tangu enzi hizo na kundi lake watatumbuiza kupitia uonyesho moja siku ya Jumamosi tarehe 2 Julai 2010.
Kwa mujibu wa taarifa za waandaji wa Tamasha hilo, onyesho la Bi Kidude na kundi hilo la DCMA litakuwa ni mojawapo ya vivutio vikubwa katika Tamasha hilo ambalo pia litakuwa na wasanii na makundi mengine mashuhuri kutoka bara la Afrika.

Mbali na kufanya onyesho hilo, Bi Kidude kwa kushirikiana na msanii Mahsin Basalama wanategemewa kuwasilisha mada ya ‘Utamaduni wa Unyago’ ikiwemo na kutoa vionjo vya upigaji wa Ngoma hiyo katika mkutano na waandishi wa Habari wa nchi hiyo pamoja na wasomi wa Ethnomusicology ambao wameonyesha hamu kubwa ya kufahamu undani wa utamaduni huo.
Mahsin Basalama ni mhitimu wa Chuo cha DCMA ambaye hivi karibuni amekamilisha utafiti juu ya ‘Utamaduni wa Unyago’ kupitia mradi mafunzo ya muziki ngazi ya Diploma yaliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la Norway (NORAD) na kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ushiriki wa Bi Kidude na kundi lake katika tamasha hilo, umewezeshwa kupitia ofisi ya uwakala wa Wasanii wa Muziki nchini Dhow Countries Music Academy (DCMA). DCMA ni taasisi ya kijamii yenye kuendesha mradi mkubwa zaidi wa kusambaza elimu ya muziki nchini Tanzania kutoka makao makuu yake yalioyopo Mji Mkongwe, Zanzibar.

Kheri A. Yussuf
Development, Marketing & PR Manager
Dhow Countries Music Academy, Zanzibar
Mobile: 077.362 0202
Email: press@zanzibarmusic.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2010

    Kila la kheri Bi. Kidude!

    Kama mna muda sio vibaya mkijikumbusha..

    http://vijana.fm/2010/06/28/utashi-zanzibar/

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2010

    me iyo "mtaalam wa unyago" safi sana

    mola akutangulie nyanya

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2010

    ni watu wachache sana duniani ambao wanaweza kuishi maisha marefu kama huyu bi kidude na kuweza kuwa active especially kuburudisha watu na kusafifi mbali hivyo. LONG LIVE BI KIDUDE NA MUNGU AZIDI KUKULINDA.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2010

    Bi.Kidude
    Tunakutakia kila heri Bi.Kidude,
    wewe adhina ya taifa,na msingi wa utamaduni wa Tanzania.
    Mungu akubariki daima na uzidi upeperushe bendera kila kona duniani.
    Wasalam
    Ngoma Africa band aka FFU

    ReplyDelete
  5. US BloggerJune 28, 2010

    US Blogger)

    Nawapelekeni katika tume ya dunia ya haki za biadamu. hii ni unyanyasaji na exploitation ya hali ya juu.

    huyu mzee akifa mikononi mwenu wanafungulia mashtaka kwa hiyo muwe macho sana.

    Dr. US Blogger
    Alumni Oxford University
    Economics Department

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 28, 2010

    Mitaa ya Mwanza ama Shinyanga hakatizi huyu bibi. Mikoa mibaya sana hiyo kwa vikongwe. Kama mnabisha mpelekeni Mwanza muone.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2010

    @ US Blogger) Hebu tuondolee la wewe kero zako hapa...sijui you have nothing to do today? kila post umo tu na comment zingine hata hazina kichwa wala miguu...Huyu mzee unajua umri wake na afya yake...Betty White anavyochangamka na majukumu yake mbona hupanui mdomo and she will soon be 90...

    WE need more people like her...so many Tanzanians turn off their careers just when they turn 65 yrs old...It is the good example and let people see this...They need to know if you take care of yourself you can do what you want at any age....

    I hate kila siku nikiona watu wame graduate au wanaolewa hapa kwenye Michuzi blog na wengine wanatilia ohhh mzeee, ohhh ulikua wapi....age ain't nothing but number.... if she can handle it let her do what she does best.....

    All the best Bi Kidude and make us proud

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2010

    hivi huyo hapo juu mwenye kusema bi kidude hawezi kwenda mwanza au shinyanga akili yake ni nzuri kweli au amechoka na maisha. why would someone say something like that unless amelewa tena vibaya sana. kama unatoka hizo sehemu mimi ninaona unawaibisha wenzio. kama huna la kusema ni afadhali unyamaze.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2010

    we anony unayemsema us blogger kwa kutoa maoni yake unakosea au niseme hukuilewa comment yake.

    kwanza kabisa huwezi kumfananisha berry white na bi kidude kwa vile tu wote ni wazee. berry white ana access ya health services 24/7,je bi kidude anayo? na kama anayo, hiyo service ni ya quality gani? na je bi kidude ameshasafiri masafa marefu hivi karibuni au ndo watu wanatest zali??

    hatuombei mtu yeyote mabaya lakini wazee wako more vulnerable kwa magonjwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwahiyo safari kama hizo za masafa marefu inabidi kuwa makini nazo.

    ila tunamtakia kila la heri katika safari yake.
    Kama ni for her own accord, fine. ila kama imeandaliwa ili kum-exploit bibi wa watu,,,shame on them.!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 29, 2010

    sorry wadau!! sema kweli mimi sijawahi msikiliza bi kidude wala kumuona zaidi ya kwenye picha !! sasa nimeamua kuangalia hii clibe kuthibitisha kama ni kweli anaimba!! na jibu langu mi naona anapiga kelele kama kuimba maybe uko zamani!! angalia msije ukawaliza watoto wa watu uko ugaibuni !! NA HILO BASKET PEMBENI MWAKE NI LA KUTEMEA MATE AMA??

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 29, 2010

    Kwa kweli tufike mahali tukubali huyu bibi alifanya kazi nzuri zamani sasa aachwe apumzike. Tatizo hakuna bima wala nini kwa ajili ya watu kama hawa hivyo serikali ifanye juu chini kumsaidia ili asiendelee kuhangaika kupata pesa ya kula

    Observer

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 29, 2010

    kwa kweli kwa umri wake kusafiri masafa marefu sidhani kama nivyema saana, hope mtamweka business class ajilalieee wee walau asichoke sana manake economy na umri huo mmh hainogi kabisa!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 29, 2010

    ni kweli bi kidude ne mzee lakini kama anaweza kuimba it does not matter how watu ni lazima kumsifu kwa kuweza kufanya hivyo akiwa na umri huo. hata kama ata shindwa leo kuimba at least atakuwa ameishi maisha yake to the fullest. huyo betty white kwanza hajafikia umri wa bi kidude. it does not matter hata kama anapata health servises za namna gani sijui kama atafikia umri wa bi kidude. kwani kwenye golden girls si yeye amebaki. some of you peole japokua mmeenda shule lakini minds zenu ni very shallow and i find this problem more with tanzanians than kenyans. i wish huyu bi kidude alikuwa kenyan angefika mbali na tunge mpa heshima sana.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 30, 2010

    wewe unaye-wish bi kidude kuwa mkenya kwanini usienda kutafuta vizee vya kikenya vyenye talent uvisafirishe au uvifikishe mbali..kila kitu tanzanians have problems than kenyans..who told you so?? as if we havent lived or worked with kenyans who are worse than anybody in east africa..grow up mate or else get a life!! and stay away from a tanzanian blog..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...