wadau wakiwa wamepiga foleni kujinunulia ving'amuzi (decoder) za StarTimes katika jengo lake lililo ndani ya makao makuu ya TBC maeneo ya Kijitonyama jijini Dar leo. Kwa mtaji wa kiasi kama 80,000 na ada ya shilingi 9,000 kwa mwezi wengi wameonesha kumudu na kujichukulia wakajifaidie kombe la dunia.
Mtaalamu wa StarTimes akiwasomesha wadau namna ya kutumia king'amuzi

Mtaalamu akieleza faida za king'amuzi cha StarTimes, mojawapo ikiwa ni uwezo wa kunasa stesheni za TV zote za bongo bila chenga na pia kupata chaneli zingine za nje kama 40 hivi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2010

    Mambo matamu ndo umuhimu wa kuwarudisha nyumbani watz waliopiga hatua nje ya nchi na kuwapa nafasi kama mzee Tido Mhando. Safi sana!Ila tbc kuna dogo mmoja anatangaza mara mojamoja kwanini mnamficha? Huyo dogo anaitwa Noeli mwakarindire sijui kitu kama hicho yaani anatisha why?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2010

    Inatumiwaje? Wanatoa antenna au inatumika kwa msaada wa dish?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2010

    Tafadhali, haishiki stesheni zote za bongo. Inanasa TCC1&2 na chennel 10. Kama mimi sielewi tueleze zinashikaje hizo channel nyingine. Toa msaada tafadhali

    ReplyDelete
  4. Hicho king'smuzi hakishiki stesheni zote za bongo, kinashika TBC1 na TBC2, channel ten kinashika picha lakini sauti ni ya magic fm... kenge kweli yaaanni.. halafu matangazo ya mpira kenge, picha na sauti zinapishana, utasikia mtangazaji anasema gooo, wakati mfungaji hata hajaupita mpira...

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2010

    channel ten ina tatizo hilo ila cha msingi bonyeza kwenye rimoti yak sehemu iliyoandikwa TRACK hiyo sauti ya redio itatoka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...