MO Blog: Kuna mpasuko mkubwa baina ya watu wa visiwani kutokana na tofauti ya itikadi za kisiasa, sasa wewe unafikiri ni njia gani zinaweza kuziweka pande mbili hizo pamoja wasahau tofauti na wajenge nchi ili visiwa vya Zanzibar vifike mbali kimaendeleo?

JUSSA: Kuna mjadala mpaka leo iwapo kweli mpasuko upo au la. Wapo wanaokubali upo wengine wanaukataa, lakini mimi ningependa niweke wazi kwamba kwa mawazo yangu mgawanyiko uliokuwepo sio mgawanyiko wa visiwa na pia sio mgawanyiko wa watu bali ni mgawanyiko wa wafuasi wa vyama vikuu vya siasa.

Na nina utazama mgawanyiko huo katika sura mbili, wa kwanza ni mgawanyiko uliosababishwa na matukio ya kihistoria, na pili umesababishwa na kutokuwepo na uwiano wa kufanya shughuli za kisiasa.

Kwa upande wa historia, Zanzibar imepita kwenye vipindi vingi vya kihistoria. Ni bahati mbaya kwamba kumekuwepo na majaribio ya ama kuifuta au kuipotosha historia hiyo. Upande mmoja hasa ule unaotawala unataka kuzungumzia Zanzibar mara zote katika enzi za za utumwa, na unataka ionekane kama vile ilikuwa biashara ya Waarabu dhidi ya Waafrika na hivyo kujaribu kuuonyesha mgogoro huu kuwa ni kama vita baina ya jamii moja na jamii nyingine. Hawa tatizo lao ni kuwa wanajaribu kukataa ukweli wa historia. Hakuna mtu anayeweza kukataa kuwa Zanzibar kulikuwa na utumwa, lakini ilikuwa sio Zanzibar peke yake nyakati hizo iliyokuwa na biashara hiyo bali nchi nyingi duniani, mfumo wa wakati huo ulikuwa wa mwenye nguvu kumshinda asiye na nguvu, haikuwa jamii fulani au kabila fulani dhidi ya jamii nyingine. Mimi mara zote hujiuliza kwa nini biashara ya utumwa ya magharibi mwa Afrika inaitwa Atlantic Slave Trade lakini ya huku inageuzwa kuwa Arab Slave Trade wakati sio Waarabu pekee waliokuwa wanunuzi wa watumwa na sio pekee waliohusika kwenye biashara hiyo. Ukitizama hata huku hao watumwa wengi walikuwa wakitoka Bara, na watumwa waliouzwa ni matunda ya vita baina ya jamii za Kiafrika huku jamii iliyoshinda ikiwauza mateka wake kwenye biashara hiyo hivyo Machifu wa Waafrika na Waafrika wenyewe pia walihusika kwenye biashara hiyo.

Kwa mahojiano kamili www.mohammeddewji.com/blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Kusema kwamba utumwa ulitokana na jamii za Kiafrika kuuza wenzao ni ku simplify the issue of slavery. Waarabu waliokuwa wanawinda tembo na kuwakamata kwa nguvu Waafrika wawabebee pembe na shehena nyingine hawakusubiri vita vya makabila na kuona ni kabila gani limeshindwa ili wawakamate utumwani.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2010

    subiri komenti

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2010

    Good one

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2010

    Very interesting, Mheshimiwa anasema mpasuko haupo baina ya visiwa au watu kwa watu, lakini opening yake inajichanganya zaidi anapoendelea kusema kwa kueleza kwanini waarabu wasihusishwe na biashara haramu ya watumwa na hapo hapo anakiri kuwa ilikuwa ni enzi ya mwenye nguvu dhidi ya mnyonge, sasa atueleze waafrika walio wengi wakati huo walikuwa na nguvu za kuwazuia arabian poachers?
    Nadhani mheshimiwa yeye hasa anatumia maneno kuwa kuna watu wanataka kupotosha historia, lakini na yeye anaonekana ni mjuzi katika hili na huenda labda hiyo ndiyo vita hasa ya mpasuko, kuna wanaoilinda na wale wanaotaka kuipotosha.
    Lakini hata hivyo ningependa kuona Mh Jussa anaandika kitabu ili tuweze kusoma na kuweka kumbukumbu sawia badala ya kuongelea hili jambo katika hali ya mkanganyiko.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2010

    Hivi hawa waarabu waliotufanyisha utumwa walishawahi kutuomba radhi kwa vitendo vyao vichafu?
    Au wanadhani ilikuwa ni haki yao kufanya hivyo?
    Ni waafrika wangapi waliteseka na kufia utumwani?
    Je, ni vizazi vingi ngapi vilipotezwa?
    je, wana-compensate namna gani nguvu iliyotumiwa na watumwa katika kujitajirisha?
    Nani yuko kifua mbele kutetea madhila yaliyowapata waafrika hata kama wangelikuwa ni mateka wa vita?
    Bwana Jussa ni iliyo fahari ya waarabu katika hili?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2010

    The man is absolutely brilliant.

    Mashaka akiwa Rais, Jussa Waziri wa Sheria na Katiba, Dr. US Blogger tumuweke Fedha, Dr. Shayo Elimu, Richard Mazingira tumpe mazingira na mimi mukinipa Wizara ya Michezo, Starehe na Burudani , Peter Nalitolela apate kazi ya kupika majungu na fitna kama nafasi ya Makamba nchi hii itakaa sawa.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2010

    Hiyo hoja ya kusema kuwa siyo Wazanzibari pekee yao waliokuwa wanafanya utumwa haina msingi.
    Everybody was doing it, so that makes it okay? Kwa hiyo if everybody was jumping off a bridge, would you do it too? Jaribu hiyo defense mahakamani. "Mheshimiwa hakimu, kila mtu anaiba, kwa hiyo kwa nini na mimi nisiibe?"

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2010

    anon wa Fri Jun 04, 10:07:00 PM jee wamarekani na waingereza hao wamemuomba nani radhi? au hujui kama nao pia walishiriki katika biashara ya utumwa?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2010

    Jamani jamani punguzeni jazba! naona watu wanatuma makali yao kwa waarabu juu ya biashara ya utumwa. Je munajua historia nzima ya utumwa? jee mumesomeshwa historia ya utomwa nyie? takriba bara zima la afrika watu walikuwa wakikamatwa na kuuzwa kama watumwa, na walikuwa wakiwafanya watumwa sio waarabu peke yao, wamarekani na waingereza nao pia walikuwa mstari wa mbele kabisa, kwa hivyo mnapotaka ku-critise muwajumuishe wote na sio waarabu tu.

    Chuki mnazozionyesha hapa juu ya waarabu kushiriki katika biashara ya utumwa kwa nini hamuielekezi kwa mataifa haya mengine mawili? Jawabu mnaijuwa sawa sawa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2010

    hapa naona watu wanajifanya wajua sana wanaitaja marekani kwa sababu mwarabu katajwa jamani tupunguze jazba waingereza sawa wakati huo ndo walikuwa north america wakiwa kama wahamiaji so na wakitumikisha watumwa wao kule wengi walitoka west africa,watumwa wetu wengi walienda kwenye mashamba ya miwa huko mauritius na reeunion nawengine arabuni kuwa watumishi wa waarabu usitaje america hapa wala hizo ni chuki za arabs na SOME ARAB STATES ndo wanapenda kupoint finger in US

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2010

    Nani kakwambia wamarekani walikuwepo? hapo zamani marekani walikuwepo wahindi wekundu,watu waliowapeleka watumwa marekani walikuwa waingereza na hao wamelowea huko, MAREKANI NI YA WAHINDI WEKUNDU.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2010

    comments zote ni bulshit warabu na utumwa so what!!! tafuteni ugali na dagaa msukume siku ziende acheni kupoteza time kwa mambo ambayo yamepita na hayana faida na nyinyi mkiongea kuhusu yaliyopita itasaidia nini??????

    mchukie mwarabu kesho wewe au ndugu yako yupo chini ya mlango wa mwarabu anaomba shida zake

    mchukie mzungu kesho wewe au ndugu yako yupo kwa huyo mzungu anaomba kazi ya kubeba maboks

    better life jitafutie kula yako wachana na siasa unajiingiza kwenye siasa wakati hakuna hata mwana siasa anaekujuwa hupati hata ruzuku shwain.

    ankal mgeni wangu wa ughaibuni wawekee watanzania ujumbe huo wajitafutie ugali sio kujiingiza kwenye mambo hayana faida na maisha yao.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2010

    Wewe jamaa wa Sat Jun 05, 04:29:00 PM,wewe ndiyo comment yako ni bull*. Angalia topic ilipoanza, watu walikuwa wana respond to hoja ya huyo Dewji. Yaani wewe ndiyo unajua kitu gani watu wajadili na kipi wasijadili? Kusema kuwa Waarabu au Wazungu walikuwa wanafanya biashara ya utumwa siyo chuki, ni historia. Marekani kwenye ukienda shule unasoma historia ya utumwa; sasa na wao wana chuki? Kama huna la kusema kaa kimya, siyo kuwakataza watu wazima wasiongelee kitu fulani. Wewe umekua nani?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2010

    Nafikiri unaweza kuona mgawanyiko wa kidini katika komenti.

    Dini nzuri: waarabu walifanya utumwa.

    dini fulani: wazungu ndo walifanya na kununua watumwa toka kwa waarabu.

    TUWE WAKWELI: woote walaumiwe sawa kwani walifanya dhambi

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 05, 2010

    katafute kibarua ufanye hujui chochote ungekuwa unajuwa usingesema kuwa watu wanajadili hapo hamna kujadili kuna kushutumu watu fulani nani asiejuwa historia ? nani asiesoma history? kama umepita shule lazima itakuwa umesoma history ch#$^*)(* pamb*%$f

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 06, 2010

    ANON WA HUU MUDA Sat Jun 05, 07:03:00 PM WEWE HUNA KICHWA KIZURI KABISAAAA

    MWENZAKO KATOA USHAURI WAKE KUWA WATU WAACHANE NA KUANGALIA YALIYOPITA KWA KUMAANISHA KUWA WATU WALIOTANGULIA HAWAJADILI KAMA UNAVYOFIKIRIA ISIPOKUWA WANASHUTUMU WATU WARABU NA UKIANGALIA JAMBO LA WATUMWA HALIKUWA KWA WARABU PEKEYAO LILIKUWA KWA WAZUNGU NA WARABU SASA MKISHIKILIA KWA WARABU PEKEYAO INAMAANISHA WAZI KUWA MNA UPENDELEO FULANI WAKULAUMIWA NI WOTE NA ANAEULIZA KAMA WARABU WALIWAHI KUOMBA MSAMAHA JUU YA HILO JE AJIULIZE WAZUNGU WALIMUOMBA NANI MSAMAHA? NI NANI ALIEFANYA MATESO MAKUBWA KWA WAAFRIKA DUNIANI KATI YA MWARABU NA MZUNGU?

    MPAKA LEO WAZUNGU WANAENDELEA KUWATESA WAAFRIKA KWENYE NCHI ZAO NA MPAKA NDANI YA NCHI ZA WAAFRIKA MZUNGU ANAENDELEZA UBABE ANGALIA ZIMBABWE ANGALIA AFRIKA YA KUSINI
    AU WALE NI WARABU?

    CHUKI ZA KUMUONGELEA MWARABU ITAKUWA NI CHUKI BINAFSI NA SIO KWA MATENDO YAO

    KAMA KWELI MJANIFANYA MNAFATA HISTORY ZA MAISHA YA WATUMWA KAANGALIENI SINEMA YA.....

    KUNTA KINTE JE KWENYE SINEMA YA KUNTA KINTE KUNA MWARABU PALE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...