Naibu Meya wa Ilala Mstahiki Jerry Silaa katika mahojiano maalum kwa watoa mada yaliyofanyika makao makuu ya Benki ya dunia mjini Washington DC usiku wa kuamkia leo katika siku ya pili ya mkutano.
Naibu Meya huyu alielezea mikakati mbalimbali ya manispaa ya ilala na jiji la Dar es salaam kwa ujumla inayolenga kumpunguzia makali ya maisha mwananchi wa hali ya chini. Mahojiano hayo yatatumika na vyombo mbalimbali vya habari nchini marekani na kwenye tovuti ya benki ya dunia.
Haya Michuzi...tumesikia. Anaenda kugombea Ubunge jimbo gani..Ukonga, Kinyerezi au Kawe?
ReplyDeleteDogo anataka kuja kugombea Ubunge nini? Maana hiyo promo?
ReplyDeleteHivi huko pia wanaongea Kiswahili au?
kaka MICHUZI habari ya asubuhi,pole na kazi.tafazari kaka naomba tuwekee hiyo link ya maojiano ili na sisi tupate kuiona vizuri,asante.LIBENEKE OYEEEEEEEEE.
ReplyDeleteMdau-Ukerewe!!!
We appreciate your representation of our district to the world bank conference,hoping laters' development plan regarding the 3rd world countries' cities will be thoroughly executed by you leaders upon your arrival at home so that one day, our Dar es salaam-Ilala can be similarly to Pennsylvania avenue.Congrats bro
ReplyDeleteMatunda ya Ukonga primary school - 1995...Ulianza vizuri tokea Mwanzo, hongera kijana,ila ukiwa kama kijana, uwe chachu kwa wazee, uwaonyeshe kwamba vijana pia wanaweza kuleta maendeleo,
ReplyDeleteCHANGE, is all we want...tunahitaji speed & accuracy kwenye kuleta maendeleo, na siyo SIASA.
NI MATUMAINI YANGU KUWA UMEWAPALEKEA PICHA ZA ILALA ILI WAONE UCHAFU UNAOZAGAA MITAANI NA HASA SOKO LA BUGURUNI NA FERRY. TAFADHALI USIJARIBU KUWAONESHA KUWA ILALA NAYO NI SAFI KAMA HUKO KWANI UTAKOSA MISAADA NA ITASABABISHA WATOTO KULALA NJAA.
ReplyDeleteAhaa jamani hamuoni alivyojitahid e.g Kujenga dalaja lilokuwa kilio cha mda mrefu,hamuoni barabara za Gmboto ndani ndani nying zimebadilika sasa,angalini barabara ya Banana-kivule,hiyo ni mifano tu. Generaly amejitahidi sana.
ReplyDeleteMambo mengine ni sababu ya mmbunge "BOMU" tuliyenae, kakalia mamboyake tu na ufisadi na kusahau wananchi wake.
BIG UP JERRY !!
Mdau-mwisho wa lami
Mdau hapo juu unayeomba Mungu kuwa awe amepeleka picha zinzoonesha uchafu ili apate misaada HAUNA AKILI KABISA! Kinyan'ganyiro wahed mkubwa we
ReplyDeleteNi lini jamani mtaondokana na hii laana ya kutegemea kila kitu upewe misaada?
Hata kufagia uchafu jamani? Sasa hapo si nchi pia tuwape moja kwa moja.
Kuna mwenye CV ya huyo naibu meya? Vijana tunahitaji inspiration..
ReplyDeleteMtunza kumbukumbu
kaka MICHUZI namjibu mdau wa 03:12 anayetaka kujua CV ya Jelly Silaa ni kama ifuatavyo.
ReplyDeleteDarasa la kwanza mpaka la saba.Ukonga Shule ya msingi.
Kidato cha kwanza mpaka cha Nne.Pubu Boys secondary school.
Kidato cha tano na cha sita Jitegemee secondary school.
Degree ya kwanza aliipatia Chuo kikuu cha Mlimani samahani kama nimesahau chochote kile tafazarini wadau nisameheni na vilevile pia mtaniwia radhi sijaweza weka miaka.naomba kuwakilisha.Asaante sana kaka MICHUZI.Mungu akubariki unapoendelea kutupatia habari motomoto ya blogu yetu ya Ukweli.
Mdau-Ukerewe!!!
Mdau wa Thu.Jun 24.02:19:00 PM Umekurupuka mbayaaa! Dude, U got to learn to read between the lines.Kwa mbumbumbu kama wewe huwezi kutambua ujumbe unaotolewa na huyo mdau lakini wajanja wanatambua.Kwa kukusaidia ni kwamba jamaa analenga kuonesha ilala bado kuna tatizo hasa la uchafu maeneo aliyoyataja na pia anagusia suala la matumizi mabaya ya misaada kwa kuchomekea "watoto kulala njaa" ni ujumbe ulio katikati ya mistari so next time be careful unapotoka kwenye kindi na kuingia humu kijijini.
ReplyDeletewatu humu ndani wamepinda balaa! kinyang'anyiro wahed we! mbavu sina!
ReplyDeleteWewe anon wa Ukerewe, huna upeo wowote..hakuna chuo kikuu cha Mlimani.
ReplyDeleteMdau Mbije,A
we Mdau unayejiita MBINJE A,we ndo bwege na sakara kabisa.na wewe ndo huna upeo wowote kwa sababu unakurupuka tuuu unachoongea hukijui.naomba kuwakilisha...
ReplyDeleteMdau-Ukerewe!!!
Mbije A, na Mdau wa Ukerewe matusi ya nini????? Mdau wa Ukerewe naomba uelewe yafuatayo: (1) Hakuna Chuo Kikuu cha Mlimani kama ulivyotoa maelezo yako. Ukweli ni kuwa Jerry Slaa alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani Campus) labda utuambie hicho chuo kiko wapi? Hutakiwi kutoa maneno machafu wakati umekosea. (2) Pili Jerry Slaa hakusoma Pubu Boys Secondary School kama ulivyoandika bali alisoma Pugu Secondary School iliyoko maeneo ya Pugu. Sasa sijui hiyo Pubu Boys Secondary School iko wapi ndugu yangu!!!!! Kutokana na lugha uliyotumia kuwakilisha CV ya Mheshimiwa Jerry Slaa sikutegemea ungetumia maneno kama "Bwege" kwa mchangiaji mwenzio.
ReplyDeletewe annoy wa 11:59...we ndo unajifanya mtu wa kurekebisha watu sio,hujatulia wewe kaazi kweli kweli,huna jipya kaa kimya tu alahaaa.
ReplyDeleteMdau-Ukerewe!!!