JK akifunua kitambaa kuashiria kufungua tawi la KCB Tanzania mjini Moshi. Kuume ni Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo nchini, Dk. Edmund Mndolwa
JK akitata utepe kufungua milango kwa benki hiyo
JK na viongozi wakuu wa KCB Tanzania wakitembelea ofisi za benki hiyo

JK akihutubia baada ya uzinduzi huo
JK akiwa na viongozi na wafanyakazi wa tawi hilo la KCB Moshi

Kenya Commercial Bank (KCB) Tanzania na wateja wake na wananchi wa Moshi mkoani Kilimanjaro wiki hii walishuhudia kuzinduliwa kwa tawi lao la mjini Moshi na mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Uzinduzi huo ambao ulikua ni wakipekee kwa Benki hiyo na wateja wake ulifanyika katika ofisi za Benki hiyo iliyopo Baranara ya Boma, Moshi mjini na kushuhudiwa pia na mamia ya wananchi waliokuwa wamesimama kando kando ya barabara.

Tawi hili la Moshi ni miongoni mwa matawi kumi na moja ya Benki hii ambayo ilianzishwa rasmi hapa Tanzania mwanka 1997.

Katika uzinduzi huo Mheshimiwa Rais aliuagiza uongozi wa juu wa Benki hiyo kupunguza riba za mikopo ili watu wengi waweze kufaidika na mikopo inayotolewa na asasi hiyo na nyingine za kifedha.

Mbali na hayo, Mheshimiwa Rais pia alisema kuwa serikari katika bajeti ya mwaka huu itatoa zaidi ya shilingi bilioni mia moja kwa ajili ya Benki ya uwekezaji ili kuwawezesha watanzania wakope na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande mwengine, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya KCB Tanzania Dk. Edmund Mndolwa alisema kwa upande wake Benki imejidhatiti kutoa huduma bora kwa wateja wake na kugusia uanzishwaji wa huduma ya kitechnolojia ya kiBenki ya T24 ambayo itawawezesha wateja wa Benki ya KCB popote katika ukanda wa Afrika mashariki kupata huduma za kiBenki popote ilipo Benki hiyo ya KCB.

Naye mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo nchini Nd. Joram Kiarie mbali na kuwashukuru wateja wa Benki hiyo kwa kufanya biashara nao, pia aliwasihi wale wote ambao bado hawajapata fursa ya kuhudumiwa na Benki hii, wafanye hivyo ili waweze kufaidi na kufurahia huduma bora zinazotolewa na Benki hiyo.

Benki ya KCB ndio Benki kubwa kwa rasilimali katika ukanda wa Afrika Mashariki na ni Benki kubwa ikiwa na matawi zaidi ya mia mbili (200) na mashine za kutolea pesa yaani ATM zaidi ya mia nne (400).




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2010

    Jamani Waziri wa fedha yuko wapi?kwani mpaka aende JK.kaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2010

    Halafu wa Kenya wakisema kwamba watanzania hatujitumi tunalalamika. ona benki yao Kenya commercial bank inafungua matawi hadi moshi wakati sisi hatuna hata benki moja nje ya Tanzania.
    sob sob.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2010

    TFF NA HASARA YA MABILIONI
    BRAZIL VS TANZANIA: Kwanza sijui namna gani watarudisha hilo deni na kama walikopa benki maana yake jumlisha na riba aidha shortrun au longrun term.Kama TFF ingekuwa ni benki basi ingefirisika na hivyo crisis!.Mimi sipingi kufanyika kwa mechi,ila je walijiandaa vipi kukusanya hizo bilioni 4(nne) ambapo wenyewe wameambulia kukusanya bilioni 1.6 TU!.Sasa wanajipanga namna ya kuzirudisha je shughuli za TFF zitaendeshwaje?(yaleyale...!!!) . USHAURI:
    Mfano TFF ilitakiwa ishirikiane na vyombo kama hazina(ofisi za posta) katika kuuza ticket hadi mikoani sio DAR tu!ili kuepusha usumbufu kwa wateja hasa wa mikoani. pia kwa vile ticket ilikuwa ni ghali ,walitakiwa kuuza ticket hata kwa mkopo kwa maajenti wa uhakika kama vile watumishi selikalini,wafanyabiashara nk. Mwisho TFF ni mpira lakini pia ndani yake ni uchumi pia!.Hivyo basi tusiajiri tu wanaojua kukimbia au kudaka bali pia wanaowezesha kukimbia au kudaka nikimaanisha wataalamu ndani ya TFF .NI MIMI MDAU MTANZANIA a.k.a (TATU-TATU) ALGERIA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2010

    Na bado, wakenya wataendelea kutesa Bongo wanavyotaka, kwa raha zao. Wabongo endeleeni na usingizi wenu mnono!

    ReplyDelete
  5. Bongo Live!
    Now you can receive SMS ads of your interest on your mobile. Sign up
    now at www.bongo-live.com
    Bongo Live!
    www.bongo-live.com
    Bongo Live! is a mobile services company based in Dar Es Salaam, Tanzania. We’re a team of individuals committed to bringing the next level of mobile and SMS based services to Tanzania. We believe that ...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...