Mama wa Waziri mkuu Alberina Kasanga akimzawadia kuku JK alipowatemebelea nyumbani kwao eneo la Kibaoni,wilayani Mpanda,mkoa wa rukwa jana mchana. Kulia ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda,Baba ya Waziri mkuu mizengo Pinda
akiwa pamoja na wazazi wa Waziri Mkuu mhehimiwa mizengo Pinda huko nyumabni kwao Kibaoni, wilayani Mpanda,mkoa wa Rukwa jana mchana.Kushoto ni Mzee Xaveri Kayanza Pinda(80) Baba wa Waziri Mkuu na kulia ni Mama Albertina Kasanga(70) Mama wa Waziri Mkuu
Mtaalamu wa Maabara katika hospitali ya mkoa wa Rukwa bwana Dodea Mlenda akimpa maelezo Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi mashine mpya za kisasa za uchunguzi wa maradhi zinavyofanya kazi muda mfupi baada ya Rais Kuzindua maabara ya kisasa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa jana asubuhi.Maabara hiyo ya hospitali ya mkoa wa Rukwa ni kati ya maabara 23 zinazojengwa katika mikoa mbalimbali nchini kwa msaada wa shirika la Abbott Fund lenye makao yake nchini Marekani.Kushoto ni Mbunge wa Kwela Chrisant Mzindakaya na watatu kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Waziri wa Afya Dr.Pamela Sawa.
JK akikata utepe kuzindua ujenzi wa mitambo mipya ya kuzalisha umeme mjini Sumbawanga jana asubuhi.Mitambo hiyo itauwezesha mji wa Sumbawanga na wilaya za jirani kupata umeme wa uhakika.Watatu kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja,wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO mhandisi Willoima Mhando na wane kushoto ni meneja mahusiano wa TANESCO Badra Masoud. 

huyu waziri mkuu sio mwizi kabisa si unaona kwa wazazi wake kulivyo hongera pinda
ReplyDeleteMtoto wa mkulima kweli ana makuu...ingekuwa ni fisadi ungekuta wazazi wake wanaishi kwenye nyumba ya gorofa.Huyu na Sokoine tu ndiyo walikuwa wameka utaifa mbele.
ReplyDeleteJe Je Je hawa ni wazazi wa Pinda kwa maana ya Kumzaa? Maana Pinda mwenyewe alizaliwa Mizengo Kayanza Peter Pinda (born August 12, 1948) hivyo kwa sasa ana miaka 62. Je kama mama yake ana miaka 70 basi alizaa akiwa na miaka 8? n baba yake ana miaka 80 je alizaa akiwa na miaka 18? Naomba majibu ili nijue hawa ni wazazi wa kumzaa waziri mkuu wetu au wazazi wadogo? Naomba ufahamu.
ReplyDeleteWala usipate tabu ndugu yangu hapo juu hawa ni wazazi wake kabisa wa kumzaa nawajua tulikuwa majirani henzi hizo hapohapo Kibaoni Mpanda bigup wazee kwa kumlea kamanda Mizengo Peter Pinda kweli alitakiwa kuingia madarakani tangu zamani
ReplyDeletegood question??? wadu tunaomba jibu ili tuendelee kuosha kinywaaaaaa??!!1
ReplyDeletecha ajabu kipi kama ni baba yake wanaume wazaa hata wakiwa na umri mdogo labda huyo ni mama yake mdogo yaani baba yake alioa mke mwingine
ReplyDeleteJamani Waziri Mkuu amefanana na mama yake. Hongera wazazi.
ReplyDeleteMimi Baba yangu ana miaka 58 mama yangu ana miaka 56 Mimi nina miaka 43 naomba mnijadili mimi na wazazi wangu...nakaa manzese kwa tumbo sina wadhifa wowote serikalini wala kwenye mashirika yenu ya umma, ninauza karanga mtaani!!!!
ReplyDeleteHii imenifurahisha sanaaaa. Si muda mrefu uliopita nilimuona Mheshimiwa Pinda akimjulia hali Mzee Edward Nsalamba, aliye kuwa mbunge wakati huo halafu tena namuona HE JK anawajulia hali wazazi wa Pinda. Hii inaonyesha wazi watu hawa walivyolelewa katika maadili mema ya upenda.Mi nilisoma na Vijana wa Mzee Nsalamba anayeitwa Christopher E. Nsalamba, na tuliishi majirani sana Mpanda kama ni mpenzi wa blog ya jamii basi anipe email tuwasiliane.
ReplyDeleteMimi nadhani umri wa wazee wetu hawa umekosewa.Tujaalie mtu kuzaa akiwa na miaka 14 basi mama yetu huyo anatakiwa awe na miaka 76 na siyo 70 na baba awe kazaa akiwa na miaka 18 hapo kitaeleweka. vinginevyo mtuambie hawa ni awlezi wa Mizengo Kayanza na sio wazazi wa Mtoto wa mkulima mwenye umri wa miaka 62
ReplyDeleteWewe Mon Jun 21, 12:30:00 PM ujaweka email yako halafu unasema nikupe email tuwasiliane. Wewe vipi?
ReplyDeletehaya je na haya majina ni ya kikwetu kwetu au ya kisumbiji sumbiji na portugal jamamani naona kuna XAVI NDANI HUMO?
ReplyDelete