Mzee Misupu,
Pole kwa kazi ngumu ya kujenga taifa. Sijui kama mwaka huu utagombea ubunge kwenye lile jimbo letu la nanihii.
Kaka Michuzi kero yangu ni moja tu. Toka asubuhi ya leo hadi mda huu wa usiku mitaa ya kigamboni kumekuwa hamna umeme. Huu umekuwa ni mchezo wa karibu mara 2 ama 3 kwa wiki sasa.
Sijui watu wa huku hatuna haki ya kuupata kila siku ama vipi. Umeme umekuwa kero kubwa sana na unatulazimisha hata kutupa vyakula kwenye majokofu yetu.
Kaka naomba utusaidie.

Mdau Omar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2010

    Mdau Omar, umesahau kuwa katiba ya nchi ilifanyiwa marekebisho kuwa kila mtanzania antakiwa alale giza angalau masaa matano kwa siku?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2010

    HAYO NDO MATUNDA YA MIAKA 40 YA UHURU MJOMBA,HADI TODATE TANZANIA BADO HAKUNA UMEME WA UHAKIKA,THIS IS SHAME.LAKINI MDAU BADO TU UTAPIGIA CCM KURA THIS ELECTION YEAR,KWELI NI RAHISI KUWATAWALA WADANGANYIKA.

    MDAU-CALIFORNIA,USA.....................BY THE WAY NIMEISHI HAPA FOR 5 YRS NA THERE HAS NEVER BEEN A POWER BLACKOUT NEVER!
    POLENI SANA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2010

    Kwani Aboud Jumbe hakai tena huko Hahaaha. Subirini kiongozi au watoto wa vigogo wahamie mitaa yenu. MZ.

    ReplyDelete
  4. KalegabahoJune 25, 2010

    Wewe unalalamika umeme unakatika mara kwa mara, sie wenyeji wa bunju b hatuna umeme kabisa!
    Sa ingine ni haki kulalamika ila tujaribu kujiuliza pia, je wale ambao hawana umeme kabisa na wako dar es salaam wanaishije ishije!?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 25, 2010

    wenyewe tunaishi masaki na mikocheni, tunaofisi zetu maeneo ya posta huko tunakuja jioni kubarizi tu, umeme wa nini huko.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 25, 2010

    Uamuzi unao Oktoba hii 2010.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 26, 2010

    Viongozi wanaohusika wezi tu.Wao makwao umeme haukatiki hata siku moja.Mdau ni haki kulalamika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...