Katika pitapita yangu kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kutizama maoni yao kuhusiana na Game la Stars Vs Brazil nimekutana na hii ya mwaka. Kama ujuavyo timu nyingi zimelalamika kuhusu huu mpira mpya uitwao JABULANI utakaotumika kwenye kombe la dunia kule bondeni ikiwemo Brazil. Na kama ujuavyo sisi wabongo hua hatukosi visingizio basi Goalkeeper wetu ameeleza vyombo vya habari vya nje kuwa alifungwa kwasababu mpira wa JABULANI hauna kiwango na sii kwamba yeye sii mzuri. Lakini jamani tukubali tu kuwa pia kiwango chetu ktk football ni kidogo ndo maana tulifungwa.
Halafu wale wachawi wa Azim Dewji waliishia wapi?
TAIFA Stars goalkeeper Muharami Mohammed has joined other shot stoppers around the world to criticise the World Cup ball 'Jabulani', saying it contributed for Stars 1-5 defeat by Brazil yesterday.Mohammed, who plies his trade with Mozambique champions Ferroviario de Maputo was between the posts and conceded all five goals as double strikes from Robinho and Ramires and one from Kaka helped Brazil easily beat their host at the half filled National Stadium.
And, Mohammed has since been the subject of criticisms as most soccer fans said he was not at his best because he conceded what they deemed to be 'easy' goals.
However, the former Simba goalie was quick to defend himself, saying he regrets to concede many goals but said 'Jabulani' was partly to blame because of what he described as the ball's unpredictable swerving motion. He also said that the ball is slippery and does not allow smooth grip.
"It will definitely be difficult for a layman to understand this, but take it from me that this kind of ball (Jabulani) will lead to new goals scoring record in the South Africa's World Cup. It will disgrace goalkeepers," he said.
Mohammed also said Stars players somewhat lost steam in the second half because they were exhausted for playing two matches in 24 hours. Stars played Rwanda away in Kigali on Sunday in the crucial African Nations Championship (CHAN) qualifier tie. They lost 1-0.
SOURCE: http://allafrica.com/stories/201006081315.html
By Mdau


uncle heshima yako nafurahi sana kulipata libeneke huku ughaibuni maoni yangu ni kuhusu MAWAZO YA GOLKEEPER wetu wa timu ya taifa kuwa chanzo cha kufungwa ni mpira wa JABULANI tukubali kuwa jamaa kiwango chake ni kidogo pia asilaumu tatizo la mpira magoli yote ni uzembe wake kauli kama hi ameitoa pia hapa kipa wa spain IKER CASILLAS ila ubora wa huu mpira uko sawa na unafaa kutumika mbona ZIMBABWE hailulalamika tunao makipa wazur please tunaomba wapewe nafasi
ReplyDeleteAkisema Carlos Kameni au David James inaonekana pointi. Akisema Mwarami Mohamed au Shabaan Kado inakuwa pumba. Wabongo bwana...
ReplyDeletegame ya kigali ilikuaje nayo mkashindwa? mpira nao ulikua wa JABULANI na mlikua mmechoka kwa mazoezi ya timu ya brazil I guess hiyo ndio itakua kitetezi chako..... si walilipwa kwani wanacheza soccer bure hao? Hiyo ni kama uwe upo kazini itokee date-sensitive project muwe mnafanya overtime halafu mfanye kwa uzembe uzembe na kulipua lipua tu ....kisingizio ni kwa vile mnafanya overtime...my man ukishakubali kufanya kitu unatakiwa unatoa 110% bila hivyo unafukuzwa kazi watapewa wengine wenye hamu ya hiyo position na hamna kutafuta sababu....kubali kushindwa kama mwanamme kweli mjifunze yaishe na kama mliona kucheza game mbili within 24 hrs ni taabu si mngesema kwa maboss wenu kuwa haiwezekani. kwanini mkakubali tu?
ReplyDeleteJabulaaani! ta-ta-ta-ta-ta-ta
ReplyDeleteJabulaaani! ta-ta-ta-ta-ta-ta
Jabulaaani! ta-ta-ta-ta-ta-ta
Jabulaaani!
Jaaaabu, Jaaaabu, Jaaabulani,
Jaaaabu, Jaaaabu, Jaaabulani,
Jabulani!
Kwa hiyo ina maana huyo keeper wa Brazil yeye ndio kauzoea huo mpira wa Jabulani? Mbona yeye haku-concede magoli mengi kama huyo keeper wa Taifa Stars?
Acheni visingizio, Brazil maji ya shingo kwa Taifa Stars.
KAPATA SABABU BAADA YA KUSIKIA WENGINE WAKISEMA SIO!
ReplyDeleteHichi kweli kichekesho!!.
ReplyDeletesasa namipira ye2 ya kuzibwa pancha,viraka chungu mzima,hata uzito(volume)hauzingatiwi
Jabulani siyo tenda ya Bi Sikitu, Research imefanywa na Loughborough University,UK, walizingatia mambo mengi(Mathematocally,scientifically,equavalentlly,,thermally-bonded, three-dimensional panels,humidity ect,kwani itakua Winter SA wakati wa Tournament.
Goli zote 5 Tumeziona na zilikua za uzombe wa kipa na no 5 wake, sasa kwanini asingefungwa Gomes kama mipira mibaya??Visingizio watoe kina Buffon bwana,watu waliozoea mipira sio hawa wezangu na mie kafula nani.teh teh teh teh
mimi huyo muharami wenu sijawahi kumuona ila siku ile kwakweli yule bwana hafai hata kuchukuwa kit ya dawa ya wachezaji wa timu ya taifa kweli tumecheza na timu kubwa ila magoli tuliofungwa yeye anabeba asilimia 50 haoneshi kuwa kama anafanya hata hayo mazowezi ya kucheza nambari maoja yule hafai tena siku nikenda kuangalia timu ya taifa akiwa yeye golini naondoka kabla mpira kuanza
ReplyDeleteSamba liliwalewesha hawa jamaa.. Kikubwa tujifunze kwa makosa tuliyaona nadhani hilo ni jambo la muhimu zaidi. Makosa huwa hayakosekani katika masuala ya kiufundi.... Hapa tulizidiwa ufundi tukubali!
ReplyDeleteAnkal, Please mwambie Dewji tunazisubiri zile picha za wale wachawi baada ya uchawi wao kushindwa. Lazima tukubali: uchawi ni ujinga, ukosefu wa imani na utapeli. Haruna.
ReplyDeleteMwarami Mohamed acha visingizio goli labda la kwanza na la pili unaweza ukalaumu mabeki au hilo jabulani. Magoli yote yaliyofuta yalikuwa uzembe wako. Mwarami cha maana wewe kapige tizi ila ujua Maximo akiondoka sidhani kama utakuwa tena Tanzania one. Kuna makipa wa ukweli kama Juma Kaseja.
ReplyDeleteAma kweli kila kitu hakikosi sababu. Yaan Mwarami naye wakulaumu Jabulani?? Ama kweli ukistaajabu ya firauni utayaona ya Mussa. Kiukweli kiwango cha Mohamed Mwarami ni kidogo na hastahili kucheza National Team. Wadau msiache kupitia blogu yangu inayoitwa chikokokweli.blogspot.com
ReplyDeleteMichuzi kaka tunaomba ututafutie mtoto huyu
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=tl83QpJwZ1E&NR=1
Mwarami acha hizo wewe! We si kipa wala nini na hiyo timu unayochezea baada ya kukuona unafungwa kizembe vile lazima wakupige chini.Sasa sikiliza mziki wa kocha mpya si huyo mtalii wenu Maskio alokua anawabeba.We unaubora gani wa kumzidi Kaseja au hata Kado?
ReplyDeleteWe umefulia toka zamani sana sema ulikua unabebwa tu.
Golikipa Mwarami lofa, tena mwongo sana Asianze kujitetea. Tulikuwa tunaona wote pale ulofa wake. Hebu niambieni, kuna goli gani pale lilitokana na yeye kuponyokwa na mpira hata aseme Jabulani unateleza???
ReplyDeleteYoyote mwenye picha inayoonyesha kuwa kuna goli lilifungwa kwa mpira kuponyoka tafadhali atuwekee kwenye hii blog ya jamii.
Mwarami uwongo. Si ukiri tu kuwa ulikuwa unawatetema kina Kaka, Robinho nk!!
Mpeni ushaidi nyie mliopiga picha, picha zote za magoli yaliyofungwa siku ile. Kaa kimya, usituudhi watanzania.
Watu tukishakutetea kuwa wale ni mabingwa mara tano wa dunia, leo unaanza sababu za kitoto. Acha utoto, kamdanganye kocha wako Maximo labda atakusikiliza.
WATANZANIA TUSIACHE UZALENDO WETU TUMSAIDIE MWENZETU KULALAMIKA NA KUTOA SABABU ZISIZO ZA MSINGI KWANI HIYO NI JADI YETU. STARS WALICHOKA KUTOKANA NA KUCHEZA MECHI MBILI NDANI YA SAA ISHIRINI NA NNE LICHA YA KUWA HATA MECHI YA KWANZA WALIFUNGWA HII INATOKANA NA HALI YA HEWA NA KUCHEZA UGENINI AMBAKO WALIKOSA WASHANGILIAJI. PIA KIPA WETU NI MTAALAMU SANA KWANI YEYE ANAJUA VIWANGO NA UBORA WA MIPIRA KWANI AMEBOBEA KWENYE FANI HIYO.
ReplyDeleteHuyu Mwarami si kipa, nashangaa huko Msumbiji anafanya nini. Siamini kama ni kipa wa kwanza wa timu yoyote, sembuse Ferraviarro ambao ni mabingwa. Huyu ni kipa wa Maximo tu. Ila tukubali ukweli mwingine, hata Kaseja si kipa kama tunavyodhani. Nilishuhudia mechi zake, jamaa haokoi hatari kali hata moja. Niliona mechi yake na Yanga. Tanzania hatuna kipa hivi sasa.
ReplyDeleteMwarami anakaa Msumbiji hivyo alikuwa translator(mkalimani) wa Maximo, kwa vile Mozambique wanaongea ki-Portuguese kama wa Brazil, hivyo hapo National siku hiyo alifanya kazi zaidi ya ukalimani kuliko ukipa.
ReplyDeleteMdau
Wa-Pemba
Nchumbiji
Kwa hili Mwarami umesema! Maoni yangu mimi inawezekana umesema ukweli, ukweli ambao ulishasemwa na wale wenye ubora wa kimataifa. La ubovu wa mpira hilo ni la kweli lakini halina uhusiano na magoli uliyofungwa! Mchezaji aliyecheza ovyo zaidi ni huyu namba 5 akifuatiwa na Mwarami. Goli la kwanza beki huyo alitaka kulazimisha mpira uende mbele wakati kuna mwenzake alikuwa na nafasi kushoto kwake. Mimi binafsi namshukuru sana Maximo kwa kutufikisha hapo ni kocha mzuri sana. Ushelisheli walikuwa wanatufunga hapa hapa kabla ya Maximo. Tatizo usimba na uyanga walio nao watanzania ndiyo umemshusha hadha. Kaseja alikuwa kipa muda mwingi kabla Maximo hajaja hapa lakini taifa stars kushinda ilikuwa ndoto wala msisema Kaseja ni bora, watu muache ushamba katika football. Kocha mpya anakuja msipoangalia mtamuona hafai muda si mrefu mkiendelea na ushabiki wa kizamani wa kulazimisha kocha lazima amuite mtu mnayemtaka nyinyi.
ReplyDelete