Mshiriki wa kwanza wa mita 100 kwa wanawake katika mashindano ya wazi ya kuogelea ya Vodacom Tanzania championi akionyesha unahiri wake wa kuogelea mashindano haya yaliwashirikisha vijana kwa nia ya kuendeleza vipaji hapa nchini leo jijini Dar
Baadhi ya waogeleaji wakichupa bwawani katika mashindano ya wazi ya kuogelea ya Vodacom Tanzania championi yaliyowashirikisha vijana kwa nia ya kuendeleza vipaji hapa nchini leo
Waogeleaji wakichupa bwawani kwa uogeleaji wa kinyumenyume katika mashindano ya wazi ya kuogelea ya Vodacom Tanzania champion
Mtoto Sonia Tumitto(katikatika)akionyesha medali zake alizojishindia baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya wazi ya kuogelea ya Vodacom Tanzania championi yaliyowashirikisha vijana kwa nia ya kuendeleza vipaji hapa nchini leo jijini Dares salaam.,wengine ni washindi wa pili Dhashrrad Magesraran(7 kushoto) na Reine Opperman
Katibu Mkuu wa Chama cha kuogelea Tanzania Noel Kiunsi akimpongeza Amal Bulengo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa mita 100 katika mashindano ya wazi ya kuogelea ya Vodacom Tanzania championi yaliyowashirikisha vijana kwa nia ya kuendeleza vipaji hapa nchini leo jijini Dares salaam. Katikati Rishi Somaiya aliyeibuka wa pili





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2010

    Tuwaone basi hawa kwenye Olimpic..Sisi wengine vipaji tunavyo lakini uwezo wa kuogelea kwenye swimming pool tulikua hatuna. Tukiwa wadogo tiliogelea na kudive kwenye mto Meru tu . Tukijaliwa kwenda kwenye pool ilikua ni New Arusha hotel kwanza kuangalia watoto wa wadosi wakiogelea tu.

    Nyie mwenye bahati ya kutumia hizi facilities pigeni buti sana mtafika...

    Wanangu hapa nilipo ninawapeleka na kuwasupport kwenye kila michezo wanayoonyesha interest. Tukiwa wadogo wazazi wetu walikua wanatwambia somaaa achana na soccer itakupeleka wapi? Lakini ulimwengu wa leo ukiwa very good in anything utafanikiwa tu...

    Hongera kwa kuanzisha hayo mashindano lakini ningewashauri wareach hata under privilege kids. Nao pia wanavipaji sana tu lakini mahali pa kishine vipaji vyao hawana...

    ReplyDelete
  2. Ka michuzi eeeee!
    nauliza wabongo wanaogopa maji?
    mbona katika hawa washindanaji asilimia 98% ni wazungu na makumbaro?

    tehetehetehete!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 06, 2010

    Wabongo hawaogopi maji ila uwezo wa kwenda kwenye hizo sehemu au kusoma kwenye shule zenye facilities kama hizo hawana. Unajua hao ndio wanaoishi bongo wengine wote wanasindikiza tu. Hapo juu kasema kweli watu wengi wanavyo vipaji ila pa kufanya hayo mashindano au mazoezi hawana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2010

    mdau wa kwanza umenikumbusha mbali acha tuu enzi hizo tuliogelea sana mto themi ulikuwa na maji mengiii kabla waosha magari na wachimba mchanga kuvamia yani ilikuwa raha kweli new arusha kweli ilikuwa ya wadosi na wanafunzi wa arusha school kiukweli watoto wengi vipaji wanavyo sema tuu umaskini huu nao ndio vinaishia gizani kina serena william wangezaliwa bongo wasingekuwa hapo walipo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2010

    Mdau wa kwanza UMENIKUNA. Umenifurahisha sana mana nimekumbuka mambo ya kuongelea kule mto Nduruma. Mwe. Haya we, unayosema ni kweli sana, yaani hata hiyo swimming pool utaionea wapi? Na waliokuwa na uwezo wa kwenda huko kweli ni watoto wa kihindi, Arusha school na St. Constantine, sie wa ENABOISHU tulibaki kuwashangaa tu. Hebu cheki hata hizo picha hapo juu, hakuna watoto wa Kayumba Primary. Ukweli vipaji vipo ila facilities hakuna. Nagira - A Tawn.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...