JUMUIA YA WATANZANIA UK
-TANZ UK-

Tawi La Leicester

Kwa heshima unaalikwa kuhudhuria Mkutano wa Kwanza Rasmi wa Jumuia ya Watanzania UK tawi la mji wa Leicester,
Mkutano huo Utalitambulisha tawi kwa Wakazi wa jiji hili
Na Kufuatiwa na zoezi la Kuandikisha Wanachama,
na baadaye kufuatiwa na
Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa tawi

SHIME TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA WANACHAMA
NA KUGOMBEA UONGOZI

TANZ UK NI JUMUIA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA.

MLEZI WAKE NI BALOZI WA TANZANIA UINGEREZA,
MAKAO YAKE MAKUU YAKO LONDON. WANACHAMA WAKE, KWA MUJIBU WA KANUNI, NI RAIA WA TANZANIA
AU WALE WOTE WENYE UHUSIANO NA TANZANIA JAPO SI RAIA

Sifa za Mwanachama:
-Awe Mtanzania kwa Uraia
-Asiwe Raia wa Tanzania, bali awe na
Uhusiano wa karibu na Tanzania
-Awe mkazi wa Leicester
-Awe tayari kulipa ada ya Uanachama
Itakayopitishwa na Uongozi wa Tawi

Sifa za Kiongozi:
-Awe na sifa za Mwanachama
-Awe tayari kulitumikia Tawi na Jumuia Kwa
Mujibu wa Katiba ya Jumuia

MKUTANO UTAFANYIKA:
SIKU: JUMAPILI 04-07-2010
MUDA: SAA TISA KAMILI MPAKA
SAA KUMI NA MOJA KAMILI MCHANA
(3.00-5.00PM)
PAHALI: HASHI COMMUNITY CENTRE, NEDHAM STREET LEICESTER (MKABALA NA CHARNWOOD PRIMARY SCHOOL)
TAFADHALI TUJUMUIKE KWA WINGI NA TUWAARIFU WENZETU
Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na:
Abdul Dau- dau33@hotmail.com- Simu 07404563772
Frida Kusamba- johnfrida@yahoo.com- Simu 07969968623

AHSANTE SANA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2010

    pesa hizooooo?? maalim khamis a.k.a khamis biriani vp atakuwepo maana hatuji bila biriani!!!. na maalim khamis sahal mumempa taarifa za uongozi huo???!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2010

    hahahahah sifa ya pili ya uanachama huu imenifurahisha shana...Mmeshajilipua wote huko UK lakini hamu ya bongo mnayo....Mweeee bongo hii na ugumu wa maisha inafanya mengi....

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2010

    Jamani waswahili mna mambo kwani mna lazima kusema maneno mengi kama hutaki kuhudhuria usiende tu hujalazimishwa kama watu wamejilipua au vipi hiyo haikuhusu labda na wewe pia ndio katika hao waliojilipua sasa maneno ya nini hajakatazwa mtu kwenda wewe mdau wa anonymous lazima tujitahidi tuache uswahili jamani wenzetu wanaendelea wewe sisi tunalumbana sio vizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...