Mwl. Christopher Mwakasege

Jumuiya ya wakristo katika Uingereza na Ulaya inawakaribisha katika mkutano wa neno la Mungu utakokuwa ukiendeshwa na mtumishi wa Mungu Mwalimu Christopher Mwakasege kutoka Tanzania .

Mwl/ Mwakasege ni Mchumi na Mwalimu wa neno la Mungu ambaye mafundisho yake ni mapana na yanalenga katika maeneo yote ya maisha.

MATARAJIO
Wenye shida za kiroho, nafsi, mwili mnakaribishwa mpate majibu ya maswali yenu. Mafundisho ya namna ya kujikomboa kiuchumi kwa mujibu wa neno la Mungu yatafundishwa. Nyimbo za Injili kutoka wanamziki mbalimbali

Huu utakuwa wakati wa baraka sana jitahidi usikose nafasi hii ya pekee na Mungu atakubariki.
ANWANI YA UKUMBI
Rivermead Complex Leisure Centre,
Richfield Avenue, Reading
Berkshire, RG1 8EQ
Mikutano itakuwa inaanza
Ijumaa 30 july utaanza saa 8mchana (2pm)hadi saa 2 jioni(8pm).
Jumamosi na jumapili utaanza saa 4asubuhi (10am) mpaka saa 2 jioni(8pm).

Tafadhali tunawaomba kushiriki baraka hizi kwa kuchangia mkutano huu kwa hali na mali.
Kwa watakaoguswa kutoa,

tunaambatanisha akaunti ya bank

Account Name Association of Tanzanian Christians in Europe (ATCE)
HALIFAX BANK
ACCOUNT NO 00989146
SORT CODE 11-07-47

MAELEZO ZAIDI:
Wasiliana na mwenyekiti Reading - Peter Respigy 07888841971, Birmingham-07776358464 Jackson Kapama, London 07817479845 Elias Mwema, Milton Keynes, 07787357618, Jane maneno,-Brighton,07950324330 Joyce Jacob. Southampton 07717435287 Sekela Komba
au
07944632826./ Rev, Emmanuel Chatawe-Mwenyekiti
07776358464 Jackson Kapama /- Katibu mkuu.
KARIBUNI WOTE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2010

    Strongly Reccomended!!!!!!!!!
    Wapiga box wote was Reading na maeneo ya karibu njooni kusikiliza neno la uzima.
    Huwa namsikiliza Mch. Mwakasege katika mafundisho yake, japokuwa ni ya kidini lakini yana maana na mchango mkubwa katika maisha ya utafutaji. Simpigii kampeni, ila nasema hivyo kwa kuwa nimepata nafasi ya kumsikiliza mara nyingi.


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  2. I also do...mdau hapo juu u r very right..jamaa ana kitu cha zaidi katika mafundisho yake...very open minded na unapomsikiliza kila siku anakuwa na kitu kipya....very original kwa kweli kimaisha na kiimani mafundisho yake yanasaidia sana hasa katika ulimwengu wa sasa ambapo maisha yamejaa kukatisha na kukatishana tamaa na mambo mengi ambayo yapo so negative.so as suggested i also recommend that seminar for all those who are there to go

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...