Mkurugenzi wa Mahusuanio ya Jamii wa Vodacom Tanzania
Bi. Mwamvita Makamba
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imeanzish
a huduma ya kutuma ujumbe mfupi bure kupitia Cheka SMS.

Ikiwa na wateja zaidi ya milioni nane, huduma hii mpya itawawezesha wateja wa Vodacom kuwasiliana zaidi kwa gharama nafuu na kuwafikia watu wengi.

Huduma hii mpya pia inamruhusu mteja kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda mtandao wowote hapa nchini na sio Vodacom peke yake.

Mkurugenzi wa Mahusuanio ya Jamii, Bi Mwamvita Makamba amesema kuwa kupitia huduma hii mteja anaweza kupata kwa wakati mmoja fursa ya kutuma ujumbe ufupi 25 bure na dakika 25 za bure za muda wa maongeze kwa shilingi 1000.

Ameongeza kuwa mteja pia anaweza kupata fursa ya kutuma ujumbe mfupi 15 bure na dakika kupata dakika 10 za bure za maongezi kwa shilingi 400 tu.

Huduma hii mpya pia inatoa fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno mara tano kwa kujisajili kwa shilingi mia moja. Amesema kuwa huduma zote zinapatikana kwa masaa 24 baada ya mteja kujisajili.

Ili kujisajili alisema kwa mteja wa shilingi 1000 anapaswa kupiga *147*1000#, wa shilingi 400 napaswa kupiga *147*400# na wa shilingi mia 100 anapaswa kupiga *147*100# wa siku nzima.

Pamoja na uzinduzi wa huduma hii mpya huduma ya Cheka Time ya muda wa maongeze bure bado inaendelea ambapo mteja anapata dakika 15 za bure kwa kujisajili kwa shilingi 200 na dakika 60 bure kwa kujisajili kwa shilingi 500.

Mteja ambaye anajisajili kwa shilingi 2000 anazawadiwa dakika 100 za maongeze bure na ambaye atajisajili kwa shilingi 5000 atazawadiwa dakika 300 za bure.

Bi Makamba amesema kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2010

    WHICH IS WHICH?

    . You can't SEE without your glasses?

    OR

    .You can't BE SEEN without your glasses?

    Nevertheless,

    I must say we really enjoy seeing your face in this blog nearly every other day.

    You are looking very beautiful.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2010

    Wow, I like this ready, too smart, too talented, too respective even herself,hope well educated. Is she married already?.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2010

    I hope so,with those double rings aside man.

    Stakeholder Mbije,A

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2010

    Mdau wa pili uliyetoa maoni, mimi naona bora ungetumia kiswahili maana sisi waswaz ndio tungekuelewa na ungeeleweka vizuri, kwa jinsi ulivyomuita huyu mama eti "ready", sijui ulikuwa unamaanisha "lady" au ndio kujifanya kiinglishi kimejaa mpaka kinamwagika? Ovyoooooooooo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2010

    Sasa ndio nini kuamka asubuhi na kukuta picha ya wife kwenye blog yako?

    Hivi imeshindikana kabisa kuiweka jioni au mchana?

    ushantibua akili yangu tayari

    ahhhhhhh

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 23, 2010

    yap ameolewa tena na mzungu,na ana mtoto mmoja .

    ReplyDelete
  7. "fursa ya kutuma ujumbe ufupi 25 bure na dakika 25 za bure za muda wa maongeze kwa shilingi 1000."

    au

    "fursa ya kutuma ujumbe mfupi 15 bure na dakika kupata dakika 10 za bure za maongezi kwa shilingi 400 tu."

    SWALI: HIYO BURE IKO WAPI?????

    si tunalipia 1000 au 400 kwa ajili ya huduma hii. Badala ya BURE ingetumika neno kama, NAFUU...

    ReplyDelete
  8. KALEGABAHOJune 23, 2010

    Michelle Obama lookalike! She’s trying really hard to look like her, what a show of insecurity and confidence!
    It’s almost a nightmare now seeing her pictures on the blogs, is she after any government posts?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2010

    I think she is either trying to look like Michelle or she admire Michelle dressing style soo much which is not bad at all. The worst thing is not to have identity/brain of your own. I think she is a nice lady but I often question her judgement on things especially when she hang around women who are "no brainers". Sorry I think if you have a smart brain you should know where to spend your energy. Like the say " Tell me who you hang around with, and I will tell you what kind of a person you are". So watch out lady, this is just a personal advice.I hope Michuzi you will publish this it is just a wake up call for this lady.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 23, 2010

    mdau wa mwisho unalako jambo eti Michele Obama look-like....hivi kweli hao watu wawili wanafanana....acha wivu...kizuri acha watu wakisifie

    na wewe unayedai kaolewa kwani ilikua lazima useme tena na mzungu
    unataka kumaanisha nn...kweli watanzania we have a long way to go

    mtoa maoni wa kwanza amenifurahisha sana

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 23, 2010

    Hayo ya Mrs. Obama look-alike mnayasema nyie. She looks good that's all I can say. go gal!
    Your admirer.
    dadako,
    Sweden

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 23, 2010

    pyeeeeeeeeeeee FAULO!!! Ankal anacheza faulo pale!!!! teh teh teh Ankal nahisi harufu ya unfair play hapa!! mbona pajazzzzz umeikata kimtindo??? au ni kwa ombi maalumu?? teh teh teh teh. weka picha nzimanzima bwana ankal stock imeniishia!!! hivyo vya miss redds hapo juu vyote havina mvuto vyembambaaaaaa!! teh teh teh
    Mdau wa pajazzzz+titizzzzzz

    ReplyDelete
  13. KALEGABAHOJune 24, 2010

    ITOE HII MICHUZI!

    The lookalike issue has been going on for quite some time now, we know she does this to boost her ego, but people don't copy almost everything from a person and not to expect a backlash! We expect her to model herself with Mrs Obama development issues and not clothes, hairstyle and such, and eve going further and believe that she might be the President one day (God forbid!) or even a first lady (as if!).
    Mwamvita be yourself, loose the copycat otherwise you might even one day forget that Mzee Makamba was actually born in Tanga and not USA!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 24, 2010

    HUYU NI BINTI WA MHESHIMIWA MAKAMBA HAKUNA HAJA YA "..DNA .."

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 24, 2010

    mweee!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 24, 2010

    .......rangi tuuu! anafanana na babake badala ya mamake! au makamba hakuchagua kitu ndio maana watoto wame opt kwake? ila watu watanga wazuri, wanaume ma Handsome ...wanawake we acha tuu, ukizaa nao watu wanafika bei mapemaaa!punguza uzungu hiyo minywele ya bandia na usambaa wapi na wapi!

    ReplyDelete
  17. Nitajua vipi salio la message zangu za bure (nafuu) na huu muda wangu wa bure (nafuu) wa maongezi??? nimetwanga *147# hakuna jibu linalo husiana na message za nafuu (bure)...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...