wasamaria wema wakijaribu kufungua boneti la gari lililoshika moto maeneo ya sinza vatican jijini dar usiku wa kuamkia leo wakati likiwa limepaki karibu na kiota kimoja cha maraha katika barabara ipitayo tandale kutokea kijiweni. mwenyewe hakuonekana mara moja ikabdi wasamaria hao watumia mabavu kufungua boneti na kujaribu kuzima moto kwa maji ya bomba
haikuwa kazi ndogo, ila moyo uliooneshwa na wasamaria hawa kwa kushughulikia gari ambalo si lao namwenyewe hawamjui ni kielelezo tosha la jinsi mioyo ya watanzania ilivyo penye shida


Jamani Watanzania sisi! Mungu na azidi kutubariki! Yaani tupo tofauti sana yaani! Yaani tuna umoja na mshikamano na upendo! Sijawahi gota hapo tena! Nadhani legacy ujima na ujamaa inachangia, kwa hiyo tusimlaumu sana Baba wa Taifa kwa siasa zake hizo! Kwani matunda yake ndio kama hayo!
ReplyDeleteIngekuwa nchi nyingine hapo, yaani ndio basi tena, kitu kingeteketea hicho, kwani hamna mtu wa kujali lisilo lake!
Kweli Mungu na azidi kutubariki. I wish kama mipasuko ya kisiasa nayo isingekuwepo! Yaani ingekuwa Burudani kwa kwenda mbele.
Hapo yawezekana kabisa kuwa wasamaria wema ni 15% na wengine hapo hawatabanduka mpaka kieleweke atakapotokea mwenye gari na wengine watajibambika kuwa walisaidia na kudai posho. Mwenye gari akigoma au akisema hana fedha za kuwalipa basi litaweza kuwashawa moto hilo au hata kuwekewa misumari kwenye magurudumu. Hivyo wasamaria wapo ila wengi wao ni wahuni tu wanataka kuingiza siku yao hapo.
ReplyDelete