Na Woinde Shizza,Arusha
Shindano la kumsaka mrembo wa mkoa wa Arusha linatarajiwa kufanyika mapema mwezi huu katika ukumbi wa Snow Crest uliopo jijini hapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na muaandaaji wa shindano hilo Snodeo Densia Magesa ambaye ameshirikiana na wenzakea ambao wanaunda kikundi cha Malikia Promosheni wakati akizungumza na mwandishi wa Globu ya Jamii alisema kuwa "shindano hili litafanyika june 5 na litashirikisha jumla ya warembo 12 kutoka katika vitongoji vya mkoa wa Arusha".

Aliendelea kusema kuwa "hadi sasa maandalizi yanaendelea vyema na warembo wote wako kambini kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na siku ya shindano hili".

Alibainisha kuwa kwa shindano hilo warembo wamejitokeza wengi kushiriki na amefurahia kwakuwa ameona warembo wa mkoani hapa wameshajua umuhimu wa urembo wa watachuana vikali june 5 katika kinyanganyiro cha kumsaka mrembo wa Arusha.
Alisema kuwa kwa mwaka huu shindano hili litakuwa tofauti na mashindano mengine ya urembo yamekuwa yakijali zaidi sura,umbile,mavazi ya aina tofauti tofauti na muonekano wa mtu.
kwa upande wa Warembo hao walisema hawatajali hayo zaidi ya kufata vigezo vilivyo wekwa na waandaaji wa kuu wa mashindano hayo katika swala zima la kuchuana vikali june 5.

Mratibu wa shindano hilo alitoa wito kwa jamii kuyakubali na kuyapokea mashindano hayo kwani yataonesha asili ya makabila ya Tanzania,tamaduni na mavazi yao ambapo amesema kuwa mashindano hayo yatasaidia pia kuitangaza vema Tanzania nje ya nchi na washindi wa mashindano hayo licha ya kupata zawadi mbalimbali pia watasaidia kupatiwa ajira katika maeneo mbalimbali.

Kwa upande wa burudani Magesa alisema kuwa bado muda muhafaka wa kumtangaza msaanii hauja fika na pindi utakapo fika atatoa taarifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2010

    Kaka michuzi huu ni mwezi wa june iweje huyo mrembo apatikane mei 5 na wakati imeishapita? Tafadhali uwe unaangalia haya matangazo wanayokuletea kabla hujayapost.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2010

    I THINK THAT'S MAY 5 2O11!!!!!!!!!
    KAKA JITAHIDI KU EDIT HIZO COMMENT JAPO HEADING TU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...