Ankal akiwa na Saleh Jabir huko Ukerewe

Hello kaka Michuzi,
Natumaini unaendelea vema na ujenzi wa taifa letu. Nakupa hongera sana kwa kuendeleza libeneke la jamii, kwani limekua linatusaidia sana hasa sie ambao tunazikosa habari za nyumbani.

Kuna ubishi mwingi sana unaendelea kuhusu ni nani hasa muanzilishi wa bongo flavor, mara wengine wanasema ni Mr. II na wengine wengi. Ila mie nakumbuka nikiwa kijijini kwangu niliwahi kupata Audio Cassette ya Saleh Jabir, na nakumbuka baadhi ya nyimbo zake, ingawaje yeye alichofanya ni kubadilisha nyimbo za kiingereza na kuweka maneno ya kiswahili, na pia kuna bwana mmoja alikua anaitwa Abdul yeye alikua anajiita ya kwamba ametokea Zanzibar, nae alikua amechukua nyimbo zenye maneno ya kiingereza akabadilisha. Hawa ndo watu wawili, ila pia simkumbuki ni mwana muziki gani aliimba huu wimbo wenye maneno haya "Watu wengi wanaimba kwa nyimbo zao za taifa, naimba kiswahili kuondoa hii kashfa" may be anaweza kua Saleh Jabir sikumbuki vema. Mie binafsi yangu hawa ndo vijana ambao niliona kweli walianzisha hiyo movie nzima ya bongo flavor, hao wengine naona walikuja baada ya hao.

Hebu wadau naomba mlichangie hili, kwani kuna watu wanajipa vyeo ambavyo sio vyao na wanasahau ya kwamba kujipa cheo kisicho chako ni kosa la jinai! Na kwa kujiita wewe ni muanzilishi wa kitu wakati sio wewe ni "against Intellectual Property law"

Asante kaka Michuzi nakutakia kazi njema
--
Mdau Melbourne

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 29, 2010

    Be specific, wanajipa cheo au wanapewa cheo?? maana sijasikia Sugu akisema yy ndiye??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 29, 2010

    Wewe MM ni mnafiki. Ulikuwa wapi mpaka unataka kuanzisha huu mjadala wa nani mwanzilishi wa bongo fleva wakati Mr II kakamatwa? Au nawewe ndio wale wale? Na kama huyo Saleh alikuwa akirudia nyimbo za wenzio huoni kwamba unathibitisha uasisi wa Mr II bila kujijua. Binafsi nakumbuka Saleh alirudia wimbo wa Vanilla Ice wa VAnilla Ice Baby, nyimbo ya Naughty By Nature wa Hip Hop Huree na nyimbo ya Ice Cube kama sikosei. Lakini Mr. II alikuwa wa kwanza kuimba bongo fleva yakutokopi nyimbo za kimarekani na kufuatwa na makundi kama Kwanza Unit. Kwa mantiki hiyo, kama kwasababu kukopi nyimbo sio usanii Mr. II anahaki ya kujiita muasisi.

    Halafu MM usiwatishe watu na hicho Kijichuo chako cha La Trobe. Kwa hapa Melbourne, Vyuo nguli ni Melbourne na Monash Universities tu vingine ni afadhali na kubaki Tanzania kusomea UDSM au Sokoine. Waste of time and money. Haya sasa michuzi nibanie maana unamuogopa sana Kusaga na Clouds yao ingawa mimi sitetei watyu kutukanana hadharani na kutishiana maisha kama Mr. II alivyoimba.

    ReplyDelete
  3. Msome aliekuwa mtangazaji nguli wa redio Mike Mhagama

    http://pesambili.blogspot.com/

    Anajua kila kitu kuhusu Bongo Fleva siku hizi naziita Bongo Fool Ever

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 29, 2010

    we cha muhimu ungekonsetrait na masomo hapo LA TROUBLE UNIVERSE kuliko kuuliza maswali ya kitoto sory kumbe nimekosea jina la chuo chako, haya kalale

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 29, 2010

    Kuwa mwanzilishi haina maana ya kuwa mtu mmoja tu. TANU ina waasisi wengi si Nyerere tu. ASP ina waasisi wengi pia - si Karume tu. Pioneer si lazima awe mmoja. Huu mjadala wako wala hauna maslahi kwa Watanzania zaidi ya kulisha na kutosheleza EGO yako tu.

    ReplyDelete
  6. MliakuvanaJune 29, 2010

    My point exactly, Anonymous wa Tue Jun 29, 09:30:00 AM. Post hii a little fishy but nitachangia. Sugu hajawahi kusema yeye ndie muasisi wa bongo flava, ila, ni miongoni wa bongo flava artists walioanza kuimba track zao wenyewe kwa kiswahili na sio kama hao akina Jabir waliokuwa wanabadilisha english songs into Kiswahili.

    Kwa ujumla wao wote ni waasisi wa genre hii ya muziki, na Sugu (tena wakati ule alijulikana kama II Proud na Mr. II) hajawahi kusema ni yeye ndio muasisi, ila alishasema yeye ni miongoni mwa artist wa mwanzo sana katika fani hii.Na bado yupo katika game!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 29, 2010

    Lbda mtenganishe mawili hapa, kutumia kiswahili na artist kuimba mashairi yake mwenyewe. Maana hapa kila mtu atakuwa ana uanzilishi wake ukizingatia haya mawili lasivyo mjadala hautafikia muafaka, kwa mtazamo wangu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 29, 2010

    Nasema OPP...!!! x2 Ice ice baby ooh oooh x2. Kina Jabir walikuwa wanachukua nyimbo za kiingereza wanarudia kwa kiswahili na kisanii uwezi kumuita mtu kama huyo muasisi wa kitu chochote mana ame-copy. Pia baada ya kurudia hizo nyimbo ulipita muda mrefu sana mpaka kina mr. II kuja kuingia na bongo fleva zao na kina Dola soul,pia na Balozi ndio wakajaga wakaangukiwa na Jukwaa kwenye Fiesta flani ivi iliyoandaliwaga na kampuni ya Sigara.

    Waulizeni wale waliodondokewa na JUKWAA wana machungu ya majeraha watawaelezea vzr tu habari ya Bongo fleva. Watu wana machungu ya kudondokewa na Jukwaa wewe unaleta habari zako za nani MWANZILISHI? Haya we...! @ dayworker.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2010

    Hakuna cha salehe Jabir wala nani kwenye hii mada. Huyo naye ni mchangiaji wa juzi tu.

    watu tulianza kuflow na mistari ya kichwa katikati ya nyimbo toka Mennonite sunday schools siku nyingi sana (70's) makanisani na wakati wa makambi.

    Unafikiri hiyo ilikuwa nini kama si Bongo Flava with a Christian touch!

    ReplyDelete
  10. yaliyomo yamoJune 29, 2010

    wewe mm huko unawaza bongo fleva au masomo?
    anyways, unachotakiwa kujua ni kwamba kuna kudesa na kufanya kazi. alichokuwa anakifanya sele jabri ni kudesa, Sugu alifanya kazi yake mwenyewe.

    kitu cha pili unatakiwa uweze kutofautisha bingo fleva na hip-hop. maana watu wengi mnashindwa kutofautisha.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 29, 2010

    Unapozungumzia muasisi sio mpaka iwe wimbo wazushi nyie acheni hizo. Saleh Jabir ndio muasisi. Unapozungumzia uasisi (Genesis) hata dhana au wazo pia ni uasisi. Aliyefungua pazia la mawazo ya kuwa na aina tofauti ya muziki ni yeye Saleh Jabir. Kabla yake ilikuwa ni dansi tu na taarabu za kina Shakilla. Halafu hivyo vyuo vyenu bomu vile vile, vyuo viko huku maandishi matatu (USA).

    Mdau

    University of Illinois

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 29, 2010

    wana diplomats wa tambaza je? mmewasahau wao pia ni miongoni mwa waanzilishi wa hii fani mwawakumbuka.
    haya azania rusheni mawe ya chuki.
    ha ha ha napasua roho za watu hapa.

    tazama
    mbele
    zaidi

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 29, 2010

    Wakati Saleh Jabir anaimba hizo mnazodai "copy", Sugu alikua Kigogo anasoma Nursery School. Nakumbuka vijana wengi walikuwa wakiiga hata syle yake ya kuvaa

    ReplyDelete
  14. MASUMBUKOJune 29, 2010

    Hapa unachokitafuta ni kuhusu kukamatwa KWA MR.II.HUYO JAMAA HAPO JUU HAKUWAHI KUWA NA BITI YAKE HATA SIKU MOJA.NI SAWA NAWASUKUMA KWENYE HARUSI KUTUMIA BITI ZA CHAKACHAKA KUIMBA KISUMKUMA.
    ISSUE -Hapa ni VITA DHIDI YA WATU WANAOISHI KWA KUJIPENDEKEZA??? SIJUI MICHUZI HILI WEWE UNALIONAJE HASA KWA UPANDE WAKO???

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 29, 2010

    Nyinyi watu mnavutana masikia bure,je mimi ninaekuna kichwa hapa Cambridge University na yenyewe sio shule?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 29, 2010

    WW YANI BONGO FLAVA INAANZISHWA WE UKO KWENU KIJIJINI,LEO UKO AUSTRALIA UMESHA VUA MAWANI YA MBAO FUTA TONGOTONGO KAMA KWELI UNASOMA SOMA ULICHOFUATA,MJADALA WAKO UNATUKUMBUSHA VICHWA MWENYEZI MUNGU ALIVYO VICHUKUA,DANDU NA WATOTO WA OSTERBAY MOROGORO STORE,YES MR 11 RESPECT.NA MUNGU AKUJALIE USIPELEKWE KIJIJINI KUWA MENEJA WA MRADI WA NJIMBO,

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 29, 2010

    Hivi nyinyi mnajadili muziki gani huo. Bongo Fleva ni muziki gani hasa? Ule ulio na midundo na melody za Kimarekani, lakini maneno ya Kiswahili au ule ulio na midundo na melody za Kitanzania pamoja na maneno ya Kiswahili kama vile Msondo Ngoma au Sikinde? Kabla hamjaanza kujadili Bongo Fleva hamna budi kuu-define kwanza ili muwe na working definition ya kufanyia mjadala. Navyojua mnachojadili ni rap music au Hip Hop kwa ujumla, yaani kurhyme kwenye beats kwa maana ya rap au kuryme pamoja na singing, kwa maana ya Hip Hop, lakini kwa kutumia Kiswahili. Lugha pekee haiwezi kufanya muziki uwe na fleva ya Bongo. Fleva inatengenezwa na melody na beats. Kalagabaho

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 29, 2010

    Nadhani mnakosa kumbukumbu muhimu kuhusu bongo fleva jinsi ilivyoanza kwanza kabisa kulikuwa na muziki wa kukopi, na miongoni mwa walionzisha koping kwa maana ya bongo fleva walikuwa ni Raiders Posse kundi la wakina Adil Kumbuka aka Nigga One, Kibacha aka KBC, D-Robbie, pamoja na makundi mengine ya VG gang star wakina Chief Ramson walikuwa watoto wa Temeke, wengine walijiita West Coast Rappers, hao ni watoto wa Ilala Flats kama Erick B pamoja na Balbo B, pamoja na kundi la 2bad Mothers wakiwamo Eazy B na Fresh G. hao ni miongoni mwa waanzilisha wa bongo fleva ya kukopi. Baadae kidogo aliibuka Salehe Jabir na kuzibadilisha nyimbo na kutia maneno ya kiswahili. Mr. II alikuwa wa kwanza kutunga nyimbo zake mwenyewe. Kwa hiyo hao wote tunaweza kusema ni waasisi. Wapo wengi wakina Cone Fransis, Fresh XE.

    ReplyDelete
  19. Mwanzilishi wa Bongo Fleva ambayo ilianza kwa jina la "Swahili Rap" Ni Salehe Jabir.


    End of story.

    Acha niwakumbushe basi mistari yake enzi hizo:

    -----

    Ice Ice Baby ... ndindindindindindindiiii

    Ice Ice Baby ...ndindindindindindindiiii

    Kitu kimenikaa moyoni sasa naamua kukitoa mdomoni
    You know what I'm saying?
    No I don't know
    Kusema mengine, naona choo
    Kama hunipendi go kacheze
    Sitopenda wengi kama Maumba

    Ice Ice Baby ... ndindindindindindindiiii

    Ice Ice Baby ...ndindindindindindindiiii

    ---
    Hiyo kitu aliishusha mwaka 1992

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 29, 2010

    Naona wengi wenu mmeshindwa kumsaidia! Huyu jamaa ili aweze kuelewa inabidi aende chuo cha sanaa Bagamoyo ndo atapata kila kitu na mengine asiyoyajua hata mwanzilishi wa dansi, taarabu atawajua thats ol.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 29, 2010

    June 19, 12:51
    Not sure abt huyu Saleh, bur You are almost right, Kwanza Unit kina D-Rob, Adil, may THE LORD rest them in eternal peace, na wenzao KBC and Ramson, na kina Eazy B ie Bernard Luanda.
    Then ndo wakaja kina Balozi na Sygon Treach...Mr II alikuja baada ya hawa niliowataja juu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 29, 2010

    SOMENI KWANZA KABLA HAMJA HUKUMU HUYO JAMAA KAPIGA TU PICHA NA MICHUZI NDIO MICHUZI KAWEKA, ILA MADA INAONEKANA KAWEKA MTU MWENGINE SIO SALEH JABIR.

    JAMAA NAKUMBUKA NYIMBO YAKE IMETOKA MIE NIPO BUNGE PRIMARY DARASA LA PILI 1992 SASA KUHUSU SUGU NIMEANZA KUMSIKIA 1994 au 1995 LABDA TUSEME MR II NDIO KAWEKA SAWA MISTARI YA KISWAHILI NYIMBO ZA KUFOKA.

    KUHUSU NENO BONGO FLAVA MIE NIMEANZA KULISIKIA 2000 au 2001 KWAHIYO HAPO SASA ALIYEANZISHA BONGO FLAVA NDIO MADA SIJUI NANI.

    MZ.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 29, 2010

    MIE NAIKUMBUKA 1992 kama mtu anaweza kutuwekea Youtube aweke ila kama wengine MR II ndio kaweka sawa kipaji cha kuimba Nyimbo za kiswahili za Rap. Jamani Bongo Flava ndio nini Haswa hata Bolingo si Flava ya Bongo? WATU HAPA WANAANZA KUCHUKULIA KAMA NANI NI MKALI HAWAELEWI MADA VIZURI. JAMES.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 29, 2010

    1.DICCA SHARP
    2.COOL JAMES
    3.MOROGORO STORE BOYZ
    SEMENI SASA ....

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 29, 2010

    wakuu nadhani hapa tunabishana bila sababu...kwa sisi vijana wa makamu tunakumbukumbu...na sidhani kama sugu anaweza kusema alianzisha hii rap bongo...

    miaka ya mwanzo ya 1988 hadi 1990 kwenda mbele watu walianza kurap...lakini wengi walikuwa wana rap ili wapate fame tu..kwenye neighbohood..kuna mtu ametaja kina adili,eazy e,fresh xe..etc....,na zaidi walikuwa wakicopy rap za mtono...baada ya hapo wakaja kina Kwanza unit,Ibony Moalim...,etc...wote hawa walikuwa wanaimba ..but hawauzi..
    miaaka ya 1992 watu walianza kufanya concert za kulipa ...pale ukumbi wa korea...etc..kabla walikuwa watu wanaimba bure coco beach..na kwenye ma graduation....

    wakati watu walipoanza kuimba kwa kiingilio...walikuwapo kwanza foundation,GWM[Gangstza with matatizo],LWP[live with purpose]....diplomatz,N2P[niggers to public]etc.....na pamoja na kuwa walikuwa wanaimba kwa kiingilio walikuwa hawalipwi zaidi ya kupattikana pesa kidogo za kugharamia maandalizi...enzi hizo watu wenye pesa walikuwa hawaiingii concerts zaidi ya vijana wasio na kazi au wanafunzi..rap ilionekana ya kihuni...

    mwaaka 1992 too proud ...ndio aliingia kwenye game ...akitokea mbeya alipokuwa anasoma...TUKUBALIANE MAPINDUZI ALIYOLETA ...yeye ndie wa mwanzo kufanya rap ni biashara....kwa mara ya kwanza alianza kukataa kuimba bure..jeuri ya kukataa kuonewa hakuanza leo.....wakati huo alikuwa na Albamu..[ NI MIMI!!!]..nipo kwenye microphoone ..hata unipe nini sitamani ..sioni!!..

    SUGU ndio wa mwanzo kabisa kuanza kufanya biashara ya kugonga copy kwa wahindi...yaani kuuza kazi zake...albamu ya pili alimuuzia mzee FM .....bahati mbaya akazulumiwa..ALbamu ya tatu aliiuza mwenyewe....na alimchana vibaya sana mzee FM ...kwa kula jasho lake.....nadhani baada ya hapo ndio aakaenda kiwanja...
    Baada ya TWO kuna makundi kama diplomatz nao waliuza kazi zao ...lakini hawakufanikiwa sana...kina saigon..[are you down with the diplomatz]...baada ya hapo kuna kundi la kina nigger j ,ambaye alikaribishwa na wenzake ...

    so kimsingi SUGU sio mwanzilishi ...ila heshima pekee anayo ya kuasisi mapinduzi ya kweli kwenye bongo flava...,kutetea maslahi zaidi na kuufanya bongo flava iwe ni biashara.......sidhani kama kuna atakayemnyima hiyo heshima..siku zote tukubali kuwa amekuwa mtu wa harakati .....na akipigwa vita vile vile ....tangu kuanzia kwa wahindi ,na waswahili wenzake kama mzee FM.....

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 29, 2010

    hehe haya maswala ya nani mwanzilishi nimeshawahi yazungumzia, hapa inaonyesha kuna mapungufu ya upatikanaji wa habari,ukusanyaji na utunzaji, hivyo historia ya kweli ni ngumu kupatikana.

    Muhimu kutochangia maoni kwenye jambo usilolijua.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 30, 2010

    Oyaaa mazee hakuna cha sugu wala saleh el nani sijui nakupa wasanii ninaowakumbuka mpaka 1999 waanzilishi walikuwa wakina Fresh X aka edo king au fresh xe huyu jamaa alikuwa akivaa hadi saa ya ukutani shingoni kama public enemy na Conway Francis na young millionaire mnamo mwaka 1984 crew yao iliitwa bad boys ,kuna Dika shap aliwashinda wakongwe hapo juu kwenye yo rap bonanza then kina samia x , Cool moc c ,master t , Dj ice-q , nigga one akiwa na kwanza unit Easy B, D-Robb, KBC ,Y thang , Killa b , nakumbuka enzi za utoto tulikuwa tukisikiliza mistari yao kila weekend coco beach na bado nakumbuka alipopata ajali pale mawenzi hotel lilikuwa ni pigo kubwa kwa sanaa pia kuna mawingu waliimba oyya msela oyaa , Hard blasters Terry (fanani) na wenzake Crazy One, KC 1, Trigger F, Tuff Jam proffesa jay hakuwepo hapo mtoto mdogo kwa fanani nakumbuka kim na yo rap bonanza hard blasters ndio walikwa wanafunika dah fanani sijui yuko wapi ila 1991 saleh jabir akaibuka alafu akapotea alishinda yo rap bonanza hali iliyowaudhi wakongwe wngine hapo ,baadae ndio wakaja kina P funk , Niggaz II public kina Mr 2, WWA aka Weusi wagumu asilia ,Gwm , Mac Muga aka Mugamugawao not sure kama ndio yule anayeimbwa na alikiba , soggy , Bob lessa , Lutengano , Rough nigazz hawa ni , kina eddy T na steve 2k aka easy E, sosi b , Deplowmatz , gwm , Da young mob alikuwemo sugu pia , Bantu pound kina soggy ,LWP,NWP,Jontwa,Ugly Face, xPlastez underground souls , Afro rains ,kina Lady jaydee steve B na Sebastian Maganga aka nature p Dray ,Juma Nature , Gangwe mob ,Buggsy malone , Ebony Moalim,Cool james, Gs mob ,4 Crewz Flavour, Dream team Witness na dataz , undergroung kindom kina jaymoe,jafarhai,Solothang ,crazzy gk ,Mr ebbo , mwana fa . mack T Ml Chriss , jimmy kabweRay c ,Fina mango ,Stara thomas emmanuel nkulila dully sykes na wengineo

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 30, 2010

    Cambrige ilikuwa enzi zetu bwana,kwa sasa ni sawa na Kampal International University mwananngu.

    Mdau Mbije,A(0718563311)

    ReplyDelete
  29. Binadamu hawana shukurani na wivu unawaua. Brother Saleh big up kwa mchango wako wa kuibua hisia za muziki mpya wa kizazi cha vijana. Kama inadaiwa Saleh aliingiza maneno tu je na Sugu nyimbo zake zote zimepigwa ala kwenye kompyuta utaita huo ni muziki? Mdau mmoja ametoa verse za Salej je huo haukua ubunifu? Sugu alitoka shamba tunamuaona wakati huo vijana saloon wanapiga nyimbo za Saleh. Vivaa Saleh Jabir

    Bana

    McGee Link,
    Los Angeles

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 30, 2010

    Mwanzilishi wa bongo flavour ni saleh Jabir; karibu miaka 20 iliyopita. Mnaobisha nadhani wakati huo mlikuwa wadogo.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 30, 2010

    BONGO FLAVA ILIANZA DAR ES SALAAM WAKATI ILIPOANZA TV MIAKA YA 93 KAMA SIKOSEI WAKATI HUO KINA SALEH JABIR WASHAREKODI NYIMBO ZA NAUGHTY BY NATURE NA SI KUTAFSIRI ILA WALIIBA MZIKI SIO,SI DHANI KAMA WALIKUA NA UWEZO WA KUFAHAMU MANENO YALIYOTUMIWA NA NAUGHTY BY NATURE BADALA YA HIYO ICE ICY BABY TU,KULIKUWEPO NA BONGO FLAVA KABLA YA SUGU KWA MFANO ITV ILIKU IKITUMIA MATANGAZO MFANO SALAMA CONDOM WATU WALIANZA KUIMBA NA USWAHILINI MATOLA NI WATU WA MWANZO MWANZO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...