Mkurugenzi mwandamizi na meneja mkuu wa Philips Healthcare Africa ambaye pia ni meneja mkazi wa Philips Afrika ya Kusini JJ van Dongen akitoa mada kuhusu huduma za kampuni hiyo ya Uholanzi usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar ambako kulifanyika hafla ya 'Safari Philips ya Cairo mpaka Cape Town' yenye nia ya kuboresha upatikanaji wa umemejua na huduma bora za afya barani afrika
Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Mh. Oliver Mhaiki (wa pili shoto) akiwa na Wakala wa Philips Mohamed M. Salim (wa tatu shoto) na Khalid M. Salim (wa tatu kulia) na maofisa wengine katika hafla ya Safari ya Cairo Mpaka Cape Town usiku wa kuamkia leo hoteli ya Southern Sun jijini Dar
kifaa maalumu cha kusomea usiku kinachotumia umeme jua kilioneshwa
wanahabari wakiongea na wana Right to play kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa Mokasi Medical Systems & Electronics Services Limited Bw. Mohamed Hasham akipata maelezo katika bango la kampuni yake toka kwa Bi. Monica Mara kwenye hafla hiyo.
betri inayohifadhi nishati ya umeme jua ya Philips
ikitumika kuwashia taa za uwanja wa michezo wa muda ulioandaliwa kwenye bustani ya hoteli ya Southern Sun jijini Dar usiku wa kuamkia leo
wadau wakicheza soka katika bustani ya hoteli ya
Southern Sun uliomulikwa na taa zinazotumia umemejea za Philips

Kampuni ya Philips imeendelea na safari yake inayoitwwa Cairo mpaka Cape town jijini Dar es Salaam iliyoanza mei 12 na iantegemewa kumalizika tarehe 20 Julai mwaka huu. Katika kipindi hicho Phillips itatembelea miji mbali mbali Afrika ili kuhamasisha fursa zitanazopatikana kutokana na utumiaji wa taa mpya zinazotumia nguvu ya jua (Solar powered LED lighting) na vile vile kutoa suluhisho bora za masuala ya tiba afrika. Kadiri ya watu milioni 560 wa Afrika hawana umeme na huduma bora za afya. Phillips ikiwa kama kampuni inayoongoza katika masuala ya huduma za afya itakutana na wadau mbali mbali wa sekta hiyo katika nchi 15 ili kufanya majadiliano yatakayotoa suluhisho za matatizo hayo.

Umeme jua katika kuboresha uchumi,
elimu na afya bora
Barani Afrika kunaingia giza katika mida ya saa 12 hadi saa moja jioni na giza hili hurudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Phillips inaamini kwamba upatikanaji wa nishati ya kuaminika na endelevu ya umeme inaweza kukuza uchumi, jamii, elimu na shughuli nyingine za kiutamaduni kwa kiwango kikubwa. Taa mpya za Phillips zinajumuisha taa ndogo ya kusomea ambayo itawapa fursa wanafunzi kuweza kujisomea usiku na pia watu wazima kuweza kupata elimu masaa ya jioni. Taa hizi ni za bei nafuu na zinaweza kutoa chachu ya kuondokana na ujinga barani Afrika.

‘Ni jambo la kushangaza jinsi taa zinazotumia jua zinavyoweza kubadili maisha ya watu katika maeneo mengi. Inaweza kubadilisha Afrika katika masuala mengi,” alisema Ruud Gullit mwanasoka mashuhuri wa zamani ambaye ameungana na Phillips katika uhamasishaji wa matumizi ya taa zinazotumia nguvu ya jua ili kumulika viwanja vya soka. Uvumbuzi huu utasaidia jamii ambazo zinaishi sehemu zisizo na umeme kuweza kucheza soka usiku kwa kutumia taa hizi zenye teknolojia ya LED. Aliongeza kuwa ni muhimu kwa waafrika kuweza kupata vitu kama hivi ambavyo ni muhimu katika kujenga maisha ya baadaye.

Philips pia inashirikiana na taasisis inayoitwa “The Right to Play foundation” ambayo ina lengo la kuinua maisha ya watoto hasa wanaoishi katika mazingira magumu ulimwenguni kote. Matthijs Huizing, Mkurugenzi Mkuu wa Right To Play Netherlands amesema: ‘Tuna furaha kubwa kuungana na washirika hawa ili kuhamasisha nguvu ya michezo katika kuimarisha maendeleo, afya na amani na hii inawezekana kwa kutumia taa hizi mpya za LED.”
‘’Ikiwa kama kampuni inayoongoza katika masuala ya afya bora, Phillips ina mpango wa kuhimiza ukuaji wa Afrika katika masuala ya uvumbuzi, upatikanaji na usambazaji wa ujuzi na kuleta suluhisho za masuala ya umeme na afya,” alisema Tamer AbolgharMeneja Mkuu wa Taa za Philips katika nchi za Misri na Afrika ya Mashariki.

Uvumbuzi na Ushirikiano
katika kuboresha huduma za afya
Sub-Saharan Afrika ina zaidi ya asilimia 11 ya watu duniani lakini ina asilimia 24 ya magonjwa duniani na vile vile asilimia moja ya bajeti za afya. Maisha ya wastani kwa mtu wa kawaida katika maeneo haya ni miaka 50 toka mwaka 2002. Phillips inaona kwamba kuna dalili za ubora wa kiwango katika huduma za hospitali na watoa huduma wameongezeka katika miaka ya karibuni na miradi mingi ya afya imeweza kusaidia kubadilisha masuala ya afya.

‘Sisi Philips, tunapongeza serikali, taasisi za umma na binafsi kwa kuwa zinaongeza nguvu katika kuboresha huduma za afya kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma na kwa bei nafuu,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa Phillips katika Kitengo cha Afya.Aliongeza kwa kusema,“ watu wengi sasa wanahitaji huduma za afya bora. Nia yetu ni kuboresha kiwango cha huduma za afya Afrika kupitia elimu, ushirikiano wa ujuzi na uboreshwaji wa ushirika kati ya wadau wa umma na binafsi.”

Philips ina ushirikiano na mashirika binafsi na ya umma (Public Private Partnerships -PPP), inayosapoti miradi mikubwa inayolenga kuboresha mahospitali, kutoa mafunzo kwa watoa huduma za afya na usambazi wa vifaa vya tiba. Vile vile Phillips ina shirikiana na shirika la kimataifa la lililo chini ya Wizara ya Mambo ya nje ya Udachi (Netherlands) ili kuhamasisha ukuaji wa uchumi katika nchi zinazoendelea.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2010

    I like it whenever I see solar technology I feel good.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...