toka kushoto ni Katibu wa Tawi la CCM MOSCOW Bi Neema Charles Kengese , toka kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM-URUSI Ndg Chrispin Bakunda na kati ni Mwenyekiti wa Tawi la CCM Moscow Dr. Alfred Kamuzora. Wote kwa Pamoja wakifuatilia Taratibu za sherehe toka kwa Mwongozaji.
bwana Octavian Nyalali , katibu wa Fedha na Uchumi wa UVCCM-tawi la Moscow Urusi, akipokea Cheti cha Uwajibikaji Mzuri ndani ya tawi.
Bi Joyce Kimaro , (mhitimu) akipokea certificate yake , Katibu wa UWT tawi la Moscow
Sehemu ya vijana walioshiriki hafra hiyo fupi.


============================

Mwenyekiti wa Tawi la CCM Moscow katika shirikisho la URUSI Dr.Alfred Kamuzora, amesema kuanzishwa kwa Jumuiya ya vijana ndani ya Chama chama cha Mapinduzi ni fursa ya kihistoria ya kuleta Usawa wa kweli miongoni mwa wanachama. Aidha amesisitiza kuwa Elimu ya Vijana wa leo wakiwa makamanda wa CCM ndio siri ya kweli ya mageuzi ya Jamii ya Tanzania, na hivyo amewataka viongozi ndani Tawi , kulisimamia suala la Elimu ya sera na itikadi ya chama cha Mapinduzi kuhakikisha linafanikiwa Kimalengo na Kimkakati., kwani elimu hiyo itathibiti Mwenendo Mzima Viongozi Bora wa Chama cha Mapinduzi katika Nyakati zote zaMageuzi nchini Tanzania.

Katika Hotuba yake fupi na makini ya karibu Dakika 20, akiwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya Vijana wa Jumuiya ya Vijana wa CCM ( uvccm-urusi) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Block 6 , Mtaa wa Mikluho Maklaya , Jijini Moscow-URUSI , Mwenyekiti wa Tawi alieleza kufurahishwa kwake na Jitihada za kuliimarisha tawi zinazofanywa na Vijana wa CCM nchini Urusi chini Uongozi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM –URUSI, Ndg Chrispin D.Bakunda katika kujiletea Maendeleo yao.

Mwenyekiti alitumia Muda Mwingi kueleza Umuhimu na manufaa ya Elimu kwa Vijana wa leo ambao ndo msingi wa maendeleo ya Taifa Letu changa linalohitaji wataalamu waliobobea na makini “ Ndugu zangu , vijana wa CCM, zingatieni masomo, kwani ndo msingi wa wewe kuwepo hapa Urusi, Taifa linawategemea na linawapa thamani kubwa, Elimu yako ndo ukombozi wa Chama cha mapinduzi na Taifa kwa Ujumla”

Kwa Upande Mwingine , Mwenyekiti wa Tawi, amepongeza hatua za kuanzishwa kwa Mfuko wa kusaidia wanawake kutatua matatizo yao, Mwenyekiti alisema ,Kwa kuanzishwa kwa mfuko huu ndani jumuiya ya Wanawake wa Chama cha mapinduzi katika Tawi letu , ni hatua nzuri itakayowaunganisha wanawake wote pamoja na kusaidiana kulingana na mahitaji yao, kwani maisha ya Ugenini yana athari zake, “nawasii washika dau wote wenye mapenzi mema , tujitokeze kuwasaidia akina mama” Mfuko huo wa kusaidia wanawake uko chini ya Jumuiya ya wanawake wa CCM , hapa Urusi, ikiongozwa na mwenyekiti wake Bi Hilda D. Kifanga.

Awali , Akimkaribisha Mgeni Rasmi: Mwenyekiti wa UVCCM-URUSI , Ndg Chrispin D. Bakunda, alitoa Ufafanuzi juu ya Tafsiri sahihi ya Umoja wa Vijana , na dhima ya kuanzishwa kwake.. alisema, “ Umoja wa vijana wa CCM ni chombo kinachowaunganisha vijana wake wa Tanzania wanaounga mkono Sera, Siasa na Itikadi ya Chama cha mapinduzi.”

Akiwakumbusha lengo lake , alisema “Shabaha za Chama cha Mapinduzi za Kuunda Umoja wa Vijana wa CCM kuwa shule ya kuandaa wanachama safi na Viongozi bora wa CCM. .Umoja wa vijana wa CCM utaandaa vijana kuwa raia wema wa Taifa letu na kwamba chombo hiki ni sawa na Tanuri la Chuma la kuokea Makada wazuri wa Chama.

Kuhusu wajibu wa UVCCM, Bwana Bakunda alisema “uvccm una wajibu wa kuongoza shughuli zinazohusu maendeleo na Maslahi ya Vijana nchini Tanzania,chini ya Uongozi wa CCM na ni Jukumu letu kama vijana wa leo katika historia ya Taifa ya kuimarishaUmoja wa Kitaifa,kuendeleza Mapinduzi ya Kijamaa ya Kidemokrasia na Mapambano ya Ukombozi katika Afrika na Dunian Kote..”

Huku akiongea kwa Kujiamini , bila kutetereka, na kushangiliwa kwa makofi na Vijana ndani ya Ukumbi, Bwana Bakunda aliwahakikishia vijana wa Urusi kuwa Umoja wa Vijana wa CCM unaongeza harakati za kutetea maslahi ya Vijana na kuwa kiungo kati ya Vijana wanamapiduzi wa Tanzania na kuwaasa vijana Kurejea Nyumbani Pindi wamalizapo Masomo, kwani Chama Cha Mapinduzi Kina Mategemeo makubwa na Vijana katika Muundo wake wa Uongozi ili kuendelea kutekeleza azma tuliojiwekea ya Ujamaa na Kujitegemea. “Tusibweteke kubaki Ughaibuni,Twendeni Tukajenge Taifa letu”

Akitoa Majumuisho ya Dhima ya Sherehe ya Vijana, Bwana Bakunda, alisema kuwa Kupokea kadi ya CCM ukiwa kijana ni ishara tosha ya kuingia katika safari ndefu ya mabadiliko ndani ya chama na serikali.

Mheshimiwa Bakunda Aliongeza na kusema kuwa Uongozi wa Vijana-tawi Una imani kuwa :- wanachama wote wa CCM tawi la Urusi watakua na staha, Uadilifu,busara na Nidhamu kwa viongozi wa Chama na watendaji wa serikali katika eneo lao la Uwakilishi, ili kufikia malengo ya kila mmoja katika kutatua matatizo ya kijamiii hapa Urusi ,bila kusahau dhima ya kupata viongozi bora na si bora viongozi, pindi Vijana wanapohitimu Masomo na Kurejea Nyumbani.

Bwana Bakunda aliwataka vijana wote katika tawi letu, kushirikiana na kuhakikisha kuwa tawi letu hapa Urusi linakuwa imara na Endelevu kimshikamano na kushinda katika kila sekta kuanzia michezo, Elimu na utamduni hasa katika kuitangaza Tanzania hususani katika Vivutio vya Utalii na Ukuzaji wa Lugha ya Kiswahili hapa Urusi

Katika sherehe hiyo ,ilipambwa kwa shamra shamra ya Aina yake kwa Chakula na Muziki wa Kitanzania,, Jumla ya Vijana 53 toka katika Vyuo vikuu tofauti mjini Moscow walijiunga na Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) na wengine 12 walijiunga Rasmi na Chama Cha Mapinduzi.

Pia, Wanafunzi wanne kati ya 18 wanaomaliza Masomo yao,Walitunikiwa vyeti vya Uwajibikaji , toka Uongozi wa Tawi la CCM Ikiwa ni ishara ya kushiriki vema katika shughuli za Tawi na kuliwekea Mwongozo Imara kwa kipindi cha mwaka 2007-2010. Walionufaika na Vyeti hivyo ni Joyce B. Kimaro ( katibu wa UWT), Zawadi Kapungu Katyoki ( Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Tawi ). Monica F. Makupa ( Katibu wa Uchumi na Fedha UVCCM) na Victor Joseph ( Mjumbe wa Baraza la Vijana wa Tawi).

Sherehe hiyo, ilihudhuliwa na wageni mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa Uongozi wa Jumuiya za Wanafunzi wa kitanzania toka katika vyuo Tofauti nchini Urusi..

Wasiliana nasi: ccmmoscow.blogspot.com
ccmmoscow@gmail.com or uvccmmoscow@gmail.com
Picha na Matukio: http://www.facebook.com/group.php?gid=115655648470594

Imeandaliwa na Kuthibitishwa :-
Idara ya Habari na Maelezo.
2nd June 2010
Jumuiya ya Vijana wa CCM-URUSI.
Moscow.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2010

    CCM oyeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2010

    Hongereni CCM Moscow. Wenzenu wa tawi la Marekani(Houston) issue imeshaingia mdudu. Waanza kufukuzana hata kbla tawi halijakomaa. Kazi kwelikweli.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2010

    Njaa hizi zitatuua...wenzetu wakienda nchi za nje ni kuelimika na kujifunza mapya. Leo CCM huku CCm kule..Mimi naseme siku vije kuanzishwa vyama vingine vya kisiasa vinavyoipinga CCM nje ya nchi sijui mtamlaumu nani hapa....Kutakua na vingine vinasupportiwa na watu wasiopenda amani ndio mtakaposema hakuna kufanya vyama vya kisiansa nje ya nchi....At that time itakua too late...Nyerere nakumiss sana tu...hawa wote wanaokubali kuanzishwa vyama vya ksisa nje ya nchi ni kwa ajili ya matumbo yao..lakini hawajali the consequences za kuwa na vyama hivyo nje ya nchi...

    Hivi hamjiulizi hivi kuna nchi yeyote hapo Tanzania inayooendeleza chama chao cha siasa hapo nchini kwetu? Magaidi wako kila mahali wanasubiri nani wakumsupport ili waone wanapigana.....

    hawa wote wanajua kuna ulaji kwenye CCM ndio maana wanakusanya CCM warudi bongo nazo ...

    Lord have mercy on us

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 06, 2010

    Mdau mtoa maoni wa jun 05, 06:41:00 PM nakuunga mkono kwa asimila zote... Hawa watu watafuta ulaji hakuna lolote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...