Mratibu wa Kitaifa wa Shirika la Kazi Duniani(ILO) Bi. Rhoda Mwamunyange (katikati) akitangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Kyela kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Jimbo hilo hivi sasa liko chini ya mheshimiwa Dkt Harrison Mwakyembe. Wengine kushoto ni Mpambe wa Rhoda na kulia ni Ofisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Mwirabi Sise.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2010

    heeeh jamani
    na mimi kesho lazima nitie timu HABARI MAELEZO kutangaza nia yangu ya kuutaka ubunge wa PERAMIHO
    mama JENISTA kaa chonjo,naweka nia na mimi sasa,heeehhh maana hii ngojeangojea mwana atakuwa si wangu!!!!
    kesho wadau tukutane HABARI MAELEZO
    MDAU WA LIPINJAPINJA
    THE GREAT

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2010

    WANAWAKE MNAWEZA, JITOKEZENI!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2010

    Hongera mama, Wanawake juuu, kwani hivi mwakyembe hagombei tena?? itanidi amawage sera zake sasa, hongera sana mwaya kaza buti mama sisi tunajua unaweza

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2010

    Mimi sikatai swala la kuwa na demokrasia ya kweli nchini kwetu. Ila tatizo langu ni hili:
    1. Ninaona swala la kugombea ubunge limekuwa kama mchezo wa kitoto tu. Sasa wewe mama unataka kugombea ili ufanye lipi zaidi ya Dr Mwakyembe kama sio huo uroho na tamaa tu.
    2. Dr Mwakyambe hatakiwi kupingwa na inabidi aendelee kuwa mbunge wa Kyela kwa sababu kuu za msingi ambazo wewe unazifahamu na wala hamna haja ya kuzitaja!
    3. Kugombea ubunge ni kujituma na wala si kutafuta hizo hela za ubunge kama wengi wanavyofikiria.

    Mimi kwa maoni yangu naona anayempinga bwana Mwakyembe ana matatizo yake ya binafsi na hii haitasaidia jamii ya Kyela ila ni kutaka kuharibu kitu ambacho kimejengwa, Haya wanieni ubunge tuone mtakachofanya kwa taifa. Cha muhimu ni kuhakikisha taifa letu linabakia na usalaama wa kweli ambao baba yetu Kambarage alituachia.

    Mdau kutoka Kagera

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2010

    SWALI LANGU MJA NAULIZA..HAWA WOTE WANAOTAKA KUGOMBEA UBUNGE WANA UWEZO WAKITAALUMA WAKUONGOZA???SASA NAONA SIASA IMEKUWA NI NJIA YA MIGAHAWA...!!!!KIASI BAADA YA KUPIGA HATUA MBELE TUNARUDI NYUMAA....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2010

    jamani watanzania Mwenyezi Mungu akitupa nabii tunadharau! hivi kweli unataka kumpinga Mwakyembe amekosea wapi kwa mtazamo wako kwa Tanzania nzima achilia mbali jimbo lake, yeye amekuwa mpigania haki ya wantanzania kwa ujumla na si kwenye jimbo lake tu! Tuelewe UONGOZI NI WITO lipi la zaidi unalotegemea kulifanya zaidi ya aliyoyafanya Mwakyembe! acha kuaribiana mpe muda tena afanya kazi za kuokoa wananchi wa Tanzania

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2010

    Mimi niko neutral; lakini najua kuwa wote Harrison na Rhoda ni wazalendo na wachapakazi. Ninachoweza kusema ni May the best candidate win.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2010

    NDUGU WANA BLOGU KUTOKANA NA UKWELI WA HALI YANGU KIFEDHA NA MATATIZO YA MAISHA LEO NAOMBA NIWAJULISHE RASMI NIA YANGU YA KUREJEA NYUMBANI TANZANIA ILI NIWAHI KUCHUKUA FOMU NA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LOLOTE NITAKALO SHAURIWA NA MPIGA RAMLI{SA NGOMA} HUKO KWANI HAPA UGHAIBUNI MAMBO YANGU SIO MSWANO KWA MUDA SASA,PIA UPANDE WA MAKARATASI NAYO YANAGOMBA KIASI CHA KUKATISHA TAMAA BORA NIKUBALI KUSHINDWA TAFADHALINI MUNIOMBEE.
    AHSANTENI.
    MTANZANIA
    INDIA.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 24, 2010

    ......VUVUZELA !!!!, fujo uwanja mzima, mwisho wa siku.....!!"tatu bila"

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 24, 2010

    nimependa afro

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 24, 2010

    Mimi ninam-support Mdau kutoka Kagera. Kama Mwakyembe amekuwa akifanya kazi yake vizuri, kwa nini kumharibia? Tukumbuke sio kila mtu atakuwa mbunge kwa wakati mmoja kwenye jimbo moja. Mpeni nafasi Mwakyembe aendelee kwa term nyingine.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 24, 2010

    Haya Mama Rhoda... Kama ameshika Jeshi na wewe wataka shika jimbo na "wizara ya wanawake na watoto" au "Wizara ya Kazi". Mimi sijui kama wewe au Mwakyembe yupi ni bora na clean... lakini nafikiri wote mna haki ya msingi kugombea hata u-president.... Go for it mom.
    Goodluck to you maana wewe hujawa na msukumano na CCM huko nyuma unaweza kupitishwa hata ukikosa unaweza kupewa Ubinge wa kuteuliwa maana Brother CDF anaweza kukuombea kwa Jamaa...

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 24, 2010

    AFRO... shirazParty bomba kishenzi

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 26, 2010

    Ushauri wa bure kwako rhoda, ni vyema ungeanzia na udiwani wa mburahati. Na nilisikia kwamba unagombea udiwani now from no where unagombea ubunge ..tena jimbo la mwakyembe...si bure...umetumwa wewe!

    Mwana mburahati mwenzio

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...