Bro Mithupu,
"ndege" nyingine "ilianguka" sehemu hizo hizo za Manga Mkoani Tanga siku kadhaa zilizopita.Mwendo kasi sana wa shangingi-ndege ulisababisha gari kupaa na kugonga nguzo ya TANESCO iliyopo mlimani , na baadaye shangingi hilo kutua mtaroni.Abiria wote walipona.
Mshuhudiaji
Mdau Lawrence

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. mhandisi msanifuJune 30, 2010

    Watanzania tunafurahia mkeka (rami barabarani) ukweli ni kwamba hio barabara haijasanifiwa vizuri. Inabidi tujieleweshe kuwa barabara nzuri sio lami bali muundo wake.
    Pia hio mistari ya kutenganisha barabara mbona kama ni ikiinimacho. Kwa stahili hio, magari mengi yanakuwa yanaacha njia, tunabakia kujiuliza......hakuna mchawi hapo ni uzembe wetu wenyewe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    no tatizo siyo kasi haya mashangingi ya siku hizi bure kabisa hayana balance barabarani spidi kidogo tu linahama njia

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    Hiyo Shangingi ni ya Wizara tu (SIRIKALI) tu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2010

    magari mendgi yanarudishwa viwandani kutokana na kukosewa kwa mahesabu flani katika balance na miundo ya breki kwenye kompyuta za viwandani. sasa hapa bongo sijui kama hilo linaangaliwa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    Duu poleni sana. Natumai wote walitoka salama. Kwani walikuwa wanaenda kutangaza nia nini??? Maana ukiwa na nia tu watu wanaanza kukutumia MASCUD.....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    Naona kauli mbiu ya mwendo kasi unaua inasahaulika haraka sana. Nahisi ni gari ya serikali manake hata plate namba zake zimechomoka wakati wa ajali hiyo....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2010

    Michuzi si vema kutumia lugha za utani kwenye habari za majanga, grow up...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2010

    Gari hilo TOYOTA Landcruiser LC200 ilikuwa jipya kabisa na ni mali ya Jamhuri.Namba zimehifadhiwa.
    Abiria na dereva waliokolewa na Air Bags zilizo fumuka humo ndani la sivyo wote wangekuwa vibogoyo!
    Kwa wasioyaelewa haya magari wajue kuwa yanaenda kwa kasi ya zaidi ya 200km/hr , na udadisi tuliofanya ni kuwa gari hili lilikuwa likielekea Mwanza kupitia Arusha.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 01, 2010

    Na kesho dereva huyu dereva atapewa electronic license mpya bila hata wasiwasi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 26, 2010

    Tatizo ya mashangingi haya mapya ni mabua jamani,yanapea kabisa barabarani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...