Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Bw. Phillip Marmo akitembelea mabanda ya taasisi mbalimbali wakati wa kuadhimisha siku ya kupiga vita madawa ya kulevya dunini bustani ya mnazi mmoja garden jijini dar wikiendi hii. mbele ni Kamishna wa Tume ya kudhibiti madawa ya kulevya nchini Mh. Christopher Shelukindo na mwenye kapelo ni mkuu wa mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Bw. Phillip Marmo akioneshwa pipi za 'unga' walizokamatwa nazo wasafirishaji wa cocaine ambao huzimeza na kuzibeba zikiwa tumboni kwenye banda la Tume ya Kupambana na madawa ya kulevya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Bw. Phillip Marmo
akiangalia cocaine kwenye banda la Tume ya kupambana na madawa ya kulevya
madawa ya kulevya
wadau wakitembelea banda la chama cha skauti na girl guide
banda mojawapo lilotia fora kuonesha njia
mbadala za kuwafanya vijana waachane na madawa ya kulevya
wadau wakitembelea mabanda mbalimbali
mojawapo ya mabanda ya wanaharakati
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge) Mh. Phillip Marmo
akiangalia mkono wa 'teja' uliosinyaa kwa alama za sindano alizojidunga wakati wa kubwia unga
Mh. Marmo akisikiliza maelezo katika banda la TRA
Mwenyekiti wa Tume ya Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini, Mh. Christopher Joseph Shekiondo, akiwa na kikosi kazi cha makao makuu ya Tume kwenye banda lao wakitabasamu baada ya kufanikisha maonesho ya siku mbili pamoja na siku ya kuadhimisha siku hiyo











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2010

    YAANI MWAKA MZIMA WAMEKAMATA PIPI TATU TU HUO NI UONGO MKUBWA HEBU SOMENI HABARI HII MKENYA AKITOKEA TANZANIA TENA JANA TU SIKU YA KUADHIMISHA HAYO MADAWA YAO AMEBAMBWA UGIRIKI -YAANI SASA WANATUPAKAZIA ZAIDI WATANZANIA SIO MAULAYA FUATA HABARI HII http://www.newsit.gr/default.php?pname=Article&art_id=32346&catid=4&la=1

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2010

    Naomba kuwauliza hao waheshimiwa hatua gani imechukuliwa kwa wale watu vigogo waliotajwa katika listi ya waliotajwa kushughulika na biashara ya unga?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2010

    Kama hayo madawa yaliyokuwa displayed hapo ni ya ukweli, forensic stock taking inatakiwa ifanyike maonyesho yakiisha, au tusije skia ooh vipipi viliibiwa na wanachi waliokuja maonyeshoni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...