Na John Bukuku
Mchezaji Patrick Ochang akikabidhiwa jezi yake yenye namba 10 mara baada ya kusaini mkataba wake na Timu ya Simba ya jijini Dar es salaam akitokea timu ya Saint George ya Ethiopia ambako alikuwa akicheza mpira wa kulipwa kabla ya kuja katika timu ya Simba.
Patrick Ochang mwenye miaka 24 na raia wa Uganda anacheza nafasi ya ushabuliaji na kiungo na viongozi wa simba walifanikiwa kumnasa baada ya kufuatilia uchezaji wake na kuridhika na kiwango cha mchezaji huyo na kwamba ni dhahiri kwamba ataisaidia sana timu hiyo katika mashindano ya kimataifa mwakani na ligi kuu ya Vodacom pia.
Wengene wanaoonekana katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu maarufu kama (Perez) aliyeko kushoto na kulia ni mmoja wa wanachama wa Simba kutoka Kundi la Friends of Simba Bw. Musleh mjumbe wa kamati ya usajili wakimkabidhi jezi mchezaji huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HUU MKATABA UMESAINIWA OFISI ZA SIMBA AU FRIEND OF SIMBA MAANA HII TABIA YA TIMU ZETU KUSINIA MIKATABA MAOFISINI KWA WATU NI YA AJABU NA KUTIA AIBU, TIMU KAMA ZA SIMBA AU YANGA KUENDELEA KUWA TEGEMEZI HADI KWENYE ISSUE NDOGO TU ZA OFISI NI AIBU NA INAONYESHA NI JINSI GANI MPIRA WETU USIVYOWEZA KUENDELEA KAMWE KAMA TUTAENDELEA KUWA NA VIONGOZI WENYE MAWAZO MGANDO, INACHOSHANGAZA TIMU INAENDA MASHINDANONI NA MARA MOJA WANAMWONA MCHEZAJI NA KURIDHISHWA NA KIWANGO CHAKE NA KUMSAJILI, JIPANGENI JAMANI MAANDALIZI YAFANYIKE KWA KUANGALIA MAHITAJI YA MUDA WA KATI NA MUDA MREFU HAPO KIWANGO CHETU CHA SOKA KITAINUKA NA TUTAANZA KUONA MABADILIKO KINYUME CHA HAPO TUTAENDELEA KUSAGA MENO KWENYE SOKA KA KITAIFA.

    MDAU
    MTANI WA WEKUNDU WA MSIMBAZI

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2010

    Kaburu, vipi? Utanilipa lini?

    Kosovo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...