Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. George Mkuchika akimkabidhi bendera ya taifa nahodha wa Taifa Stars Shadrack Nsajigwa wakati wa hafla ya kuiaga timu hiyo leo. Kesho wanakipiga na timu ya Rwanda kusaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaochezea nyumbani. Mchezo wa kwanza hapa Dar uliishia kwa droo ya 1-1. Taifa Stars watarudi Jumatatu asubuhi na jioni watakipiga na Brazil


Na Jane John
Shirika la utangazji nchini TBC leo katika uwanja wa TAIFA JIJINI DSM linazindua matangazo ya kombe la DUNIA.

Uzinduzi huo unafanyika ikiwa TBC ndiyo chombo pekee hapa nchini kupata haki ya kurusha fainali za kombe la DUNIA nchini AFRIKA KUSINI kuanzia JUNI 11 hadi JULAI 11 mwaka huu.

Katika kufanikisha yote hayo TBF imeandaa sherehe za uzinduzi huo ambapo watanzania wote watafika katika uwanja wa TAIFA bila kiingilio chochote kujionea uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2010

    Hivi hawa wanacheaza lini na Brazil. Au sio wao hilo saga la Brazili kwenda TZ nilizania ni kesho au Monday...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2010

    Mchezo si walisema, UTAKUWA TAREHE SABA - 07/06/2010 AU SI TIMU YA TAIFA HII?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2010

    Hii mechi itakuwa sawasawa na matumla kuzichapa na Mike Tyson. Yetu macho

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2010

    Hebu tewekee kikindi kitakacho cheza na Brazili kwa picha..TX in advance

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2010

    poleni Taifa stars, msipoteze matumaini mara nyingine ongezeni bidii mtafanikiwa, wanasema mliegemea sana kwenye mchezo kati yenu na Brazil sasa mimi sijui

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...