Chuo Kikuu Huria cha Tanzania chini ya uratibu wa KITIVO CHA FANI NA SAYANSI JAMII tunapenda kuwajulisha kwamba kuanzia tarehe 28/6/2010 hadi 4/7/2010 litafanyika Tamasha kubwa lenye lengo la kueneza lugha ya Kiswahili na Utamaduni wake. Tamasha hili lenye Kauli mbiu “DHIMA NA NAFASI YA KISWAHILI KATIKA ULIMWENGU WA UTANDAWAZI” litafanyika katika Ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho Kijitonyama na Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
TASAKLI itahusisha Sanaa na fani zifuatazo:

(1) Maonesho Mavazi ya Kiswahili
(2) Vyakula vya Kiswahili kutoka katika makabila ya mbalimbali ya
Tanzania.
(3) Mashairi ya muziki wa kizazi kipya [Bongo flava]
(4) Taarab
(5) Mashindano ya Utunzi na uandishi wa kazi za kubuni kama vile Mashairi, Riwaya, Tamthiliya na Hadithi fupi.
(6) Kongamano kuhusu Lugha ya Kiswahili (Fasihi na Isimu)
(7) Ngoma za Jadi kutoka katika makabila mbalimbali ya Tanzania
(8) Maigizo (9) Mashairi (10) Maonesho (11) Maonesho ya shughuli za kitamaduni (12) Nyimbo (13) Majigambo (14) Utambaji wa hadithi (15) Maonesho ya kazi za sanaa

Madhumuni ya tangazo hili ni kuwaalika Wanafunzi na Wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania na shule za sekondari na shule za msingi na watanzania wote kwa ujumla popote walipo kushiriki kikamilifu katika Tamasha hili ili kukitangaza kukieneza kukilinda Kiswahili na utamaduni wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...