Na Ripota wetu Mwanza
Imethibitishwa kuwa Sheria iliyoiunda Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora ya Tanzania, ina mapungufu makubwa ya msingi, likiwemo suala zima za Tume hiyo kutokuwa na meno yoyote kisheria, hivyo haina uwezo wa kutoa maamuzi yoyote ya kisheria, hivyo kubakia kushauri tuu na kutoa mapendekezo, wakati tume wa Kenya na Uganda, zina nguvu kisheria.
Uthibitisho wa udhaifu huo, umeelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bibi Mahfudha Alley Himid, wakati akielezea changamoto mbali mbali zinazoikabili Tume hiyo, kwenye Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, inayoendelea mjini Mwanza.
Bibi Mahfudha, amesema, kukosekana kwa meno ya kisheria, kunaifanya tume hiyo kupata kigugumizi katika kuyapatia ufumbuzi matatizo ya ukwiukwaji wa haki za msingi za binaadamu, kama matatizo ya Loliondo, mauaji ya Albino n.k.
Bibi Mahafudha amesisitiza kuwa suala la haki za binaadamu ni suala nyeti na la msingi sana katika ustawi wa taifa lolote, ndio maana Tume za Haki za Binaadamu za mataifa mengi, wakiwemo majirani zetu, zina mamlaka ya kisheria, hivyo maamuzi ya tume hizo ni lazima yatekelezwe kama uamuzi wa mahakama.
Makamu Mwenyekiti huyo, ametolea mfano maamuzi ya mabaraza ya Ardhi ya Vijiji na Mikoa,Baraza la Ushindani na Tume mbalimbali kama za Ushindani, yana uwezo wa kimahakama kusikiliza shauri na maamuzi yake yana nguvu kisheria na yanaweza kuhojiwa mahakamani kama kuna upande haujaridhika, hivyo akashangaa, iweje Tume muhimu kama ya Haki za Binaadamu na Utawala bora, yenyewe haina nguvu za kisheria (meno)?.
Pia alieleza changamoto nyingine mbalimbali zinazoikabili Tume hiyo, ikiwemo ufinyu wa bajeti, hali inayopelekea Tume hiyo kufungua Ofisi zake kwenye kanda 4 tuu wakati mahitaji halisi ya haki za binaadamu ni masuala ya kitaifa, ofisi zake zinahitajika Tanzania Mzima. Mwisho.
fungulia mbwa yetu imerudi tena..
ReplyDeleteBig up sana kwa hayo matengenezo makubwa natumaini tutapata vitu vya ukweli...
Dada Ummie katoka TAMWA. Bado ana ng'umruma! YOU GO GIRL!
ReplyDeleteKweli ni tume muhimu sana, nami nashangaa kuwa haina nguvu za kisheria. Je, serikaliw atafanya nini kuhusiana na tume hiyo?