Balozi wetu Msumbiji Mh. Pastor Ngaiza pamoja na wadau wakishangilia ushindi wa chakula cha Kitanzania. Wadau, chini ya ubalozi wetu Msumbiji, walishiriki kikamilifu kuadhimisha Africa Day katika Manispaa ya Matola na Maputo. Hakika tulijitahidi sana hususan katika kuvaa nguo ambazo ni maarufu Bongo na Mapishi. Ladha ya vyakula vyetu huwavutia wengi kiasi mwaka huu mjini Maputo vyakula kama pilau, wali wa nazi, chapati za kusukuma na za maji, ndizi za kupika na nyama na maandazi vimetufanya kuibuka wa kwanza dhidi ya Afrika ya Kusini, Angola,Ghana, Kenya, Malawi ,Msumbiji,Nigeria, Swaziland na Zimbabwe.
Adam Kinguti, Ofisa Ubalozi na my wife wake Asha Kiwanga
Mdau Frank Mwega (HOC), Mshauri wa Balozi, akihakikisha mchuzi usijeongezwa maji


Wadau Aquilina Muyonga (shoto) na Asha Maulid wakiwakilisha na mavazi ya asili
Mlinda mlango wa Taifa Stars na Ferovierro ya Maputo Mohamed Mwarami shoto akiwa na wadau Ashraf Said na Salum Magimba siku hiyo ya siku





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2010

    hiyo picha ya mwisho imenichefua

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2010

    Chuki binafsi anonymous watz hatuna hizo tabia nyie wachache ndio mnazieneza,,,,hp u gt m wht do i mean.

    ReplyDelete
  3. Umaskini mbaya kweli.mkiwa nje ya bongo ndo mnajifanya wamasai.Hapa bongo mnawadharau kama sio watu vile.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 10, 2010

    We anny wa mwanzo sio picha iliyokuchefua ila ni mimba yako changa.Halafu nahisi itakuwa ya mapacha 7 wa kiume.usijali nitakusaidia kukuletea maembe mabichi,mapera,mkaa,ndimu,udongo na mbilimbi.vitakusaidia.
    Siku nyingine ukitaka kutuma maoni tumia UBONGO sio MAKAMASI.

    Mndengestan

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 10, 2010

    Vyote hivi katika ujazo wa container la mtu kula na kusaza (macontainer makubwa ya kuwekea vyakula), kupitia email au DHL:

    1. Dagaa wa kukaanga na vitunguu vingi - bila nazi (ambao walichemshwa kwanza).

    2. Njegere za nazi, tui la kwanza, mchuzi mziitoo.

    3. Vegetable rice iliyopikwa na njegere kiasi, carrots na vitunguu.

    4. Tambi za nazi na sausages (za Arusha - No Farmer's Choice).

    5. Pilipili nyiingii iliyokaangwa na vitunguu viiivngiii na vitunguu saumu viingii.

    6. Beef Burgers zenye pilipili nyingi za pale Moricco, 10.

    7. Sambusa za Shoppers' Plaza, 20 za nyama, 20 za mbogamboga.

    8. Wali mweupe wa kukaanga usio na nazi, na sukuma wiki iliyokaangwa na vitunguu na nyanya - bila nazi.

    9. Chapati za kusukuma (zenye vitunguu majani - vile virefu, na viazi ndani), visheti, vitumbua, maandazi ya nazi na Nido kubwa.

    10. Dompo carton moja, ile yenye alcohol kiasi, sio ile iliyochorwa msalaba.

    DD1, 4HY.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 10, 2010

    Nilisahau:

    11. Kababs za Tea Shop - kule Chagga Street , Mjini - 40.

    Just Joking. Kuhusiana na yote. Just Jokes. K.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 10, 2010

    Wadau naomba mnisaidie hiyo timu anachezea Mwarami sijui hiyo Firafiolo unaweza kuilinganisha na timu gani hapa kwetu kwa ubora. Ni hilo tu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 10, 2010

    Kama huyo wa kushoto Ndio tanzania teni basi anakila sababu ya kufungwa tano za kizembe maana umri umemtupa mkono

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 10, 2010

    wewe wa mwanzo hapo juu tunajuwa kilichokuchefua, na kwa ufupi you need to chill out, chuki zako za binafsi hazitokusaidia lolote maishani zaidi ya kukukondesha. Tanzania hatuhutaji watu wenye mentality kama zako.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 10, 2010

    Tumuombee Mungu huyu ndugu yetu anon wa mwanzo. Wakiwa mia tu kama hawa Taznzania basi nchi imekwisha. Ufisadi siyo wa kuiba pesa za serikali tu jamani!, chuki binafsi pia ni aina ya ufisadi..

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 10, 2010

    mdau wa mwanzo kachefuliwa na picha ya mwisho baada ya kumuona mwalami kwa msiojua mwalami ndie kipa aliyefungwa na brazil magaoli 5

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 10, 2010

    Mwarami umenichefua sana siku na brasil. Makipa wenzio wakiona siku si nzuri kwao hua wanajifanya wameumia ili kupisha wengine sasa we kilichokufanya usijiangushe kama umeshikwa na msuli ni nini? Umetutia aibu kabisa na wewe pia umejitia aibu pamoja na huyo shogako maximo nae kaonekana bonge ya kocha fala kwa kutokukutoa , goli la kwanza ,pili ,tatu,nne,tano kakung`ang`ania tu,kiufupi wewe bongo walw ukiitwa timu ya taifa kataa kwani huna kiwango kabisa usisingizie jabulani la watu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 10, 2010

    we unaesikia kichefuchefu si ukatapike.acha unafiki wako.katika wanafiki we namba moja kilichokuchefua hapo kitu gani.mimba upewe na wengine then uchefukie watu wengine fala weweeeeee!mwenye mimba kaingia mitini nini ndo sababu kila kitu kichefuchefu we mwenyewe unatia kichefuchefu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 10, 2010

    Anony wa kwanza umezoea kulala na ngombe na kuvaa ngozi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 10, 2010

    Jamani,jamani,jamani! Ni MIKATE ya maji(pancakes) na ya kusukuma(CHAPATI)..hakuna chapati za maji!Kuna aina nyingi za mikate:Mkate wa Mofa,Mkate wa(Sinia au Kumimina),Mkate wa Mayai,Mkate wa Tambi,......nk.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 10, 2010

    Mbonamnatafuna tafuna maneno? Huyo anon wa mwanzo kachukia kuona kanzu na barakashia. Usindekeze chuki ndugu yangu maana unateseka buree!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...