Na Anna Nkinda - Nairobi.

Wakenya wametakiwa kuchangamkia mkataba wa soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki ambao utawawezesha kufanya biashara, kazi na kuishi mahali popote wapendako ndani ya nchi wanachama, kupata fursa nzuri ya kuchuma mali zaidi na hivyo kujikwamua na maisha ya umaskini.

Wito huo umetolewa jana na Rais wa Nchi hiyo Mwai Kibaki wakati akiwahutubia wananchi kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya sherehe za sikukuu ya madaraka iliyofanyika katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Kibaki alisema kuwa mkataba huo ambao utasainiwa mwezi wa saba mwaka huu utatoa fursa nzuri ya kuchuma mali zaidi kwa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki, kubuni nafasi za kazi na kuondoa umaskini.

“Katika ngazi ya kanda hii , ni fursa yangu kuona kwamba mkataba wa soko la pamoja la Jumuia ya Afrika mashariki utaanza kutekelezwa hivi karibuni hivyo basi Serikali yangu inashirikiana kikamilifu na nchi wanachama wa jumuia hii kuhakikisha kuwa utendaji kazi wa vipengele vyote vya mkataba huu unakamilika”, alisema Kibaki.

Kibaki pia alitoa rai kwa wakenya kuwakaribisha kaka na dada zao kutoka nchi za Uganda, Tanzania, Burundi na Rwanda ambao nao wataingia katika nchi hiyo kujitafutia riziki na kusema kuwa hiyo ndio njia ya kuonyesha shukrani na moyo kwa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Aliendelea kusema kuwa hivi sasa wanapenda kufungua kabisa eneo la kaskazini Kenya na kustawisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na majirani zao.

Serikali ya nchi hiyo hivi karibuni ilitoa kandarasi za kufanya uchunguzi wa ujenzi wa bandari ya Lamu, ujenzi wa reli kutoka Lamu kupitia Isiolo hadi Juba na kutoka Lamu-Isiolo hado Moyale.

Kibaki alisema “Ujenzi wa vifaa hivi vya muundombinu msingi utaanza hivi karibuni. Vilevile tumetoa zabuni ya kujenga reli ya kisasa kutoka Mombasa hadi Malaba na pia tutaimarisha zaidi huduma ya uchukuzi wa abiria kupitia magari ya moshi hapa jijini Nairobi”.

Kibaki alisema, “Matukia haya yakijumuishwa na uwekezaji tunaoufanya katika upanuzi wa barabara, utoaji wa nguvu za umeme, huduma za maji, huduma za simu na viwanja vya ndege ni ishara ya kutosha kwamba tunatayarisha nchi hii kwa hatua ya ubunifu wa nafasi za kazi na ustawi chini ya ruwaza ya maendeleo ifikapo mwaka 2030”.

Alifafanua kuwa ndiyo sababu hivi sasa wanaharakisha kazi za ujenzi wa barabara kuu ya Nauru - Eldoret hadi Malaba na kutoka Kericho hadi Kisumu na vile vile kupanua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kisumu ili kuhakikisha uchukuzi bora wa watu na ushiriki wa haraka wa masoko unafanyika.

Kuhusiana na uchumi wa nchi hiyo Mwaikibaki alisema kuwa mwaka jana uliimarika kwa asilimia 2.6 kutoka asilimia 1.6. Kwa mwaka huu unatarajiwa kukuwa zaidi kati ya asilimia 4 na 5 . Hii ni kwasababu wakenya hata wakati wa hali ngumu, wanaendelea kufanya kazi kwa bidii kuimarisha maslahi yao binafsi na ya nchi.

Naye waziri Mkuu wa Nchi hiyo Raila Odinga alisema kuwa wakenya kabla ya kupata uhuru walikuwa wananyanyaswa sana na mabepari wa kikoloni ambao walikataa kuwapa uhuru wao kwa madai kwamba hawawezi kujitawala.

“Hivi sasa tuko huru tunahitaji kuwa na katiba yetu wenyewe kwani katiba tunayoitumia sasa ilitungwa na wakoloni huko katika nyumba ya Lang’ata hakuna hata mkenya mmoja aliyeshiriki, baada ya miaka mingi tumeona ni vyema tuwe na katiba yetu wenyewe lakini bado kuna watu wanaopinga kama vile wakoloni walivyopinga kutupatia uhuru wetu”, alisema Odinga.

Aliwaomba wananchi waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya ndiyo tarehe nne Mwezi wa nane mwaka huu wakati wa kura ya maoni ili wakenya wapate katiba mpya waliyoiandaa wenyewe.

Kenya ilipata uhuru wake mwaka 1963 baada va mapigano yaliyosababisha watu wengi kupoteza maisha yao kutoka kwa wakoloni wa kiingereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2010

    wakati wenzetu wana mikakati kamambe kama hiyo sie bado tumelala. viwanja vya ndege bomu na vina landing fees kubwa zinazosababisha nauli kuwa kubwa sana kiasi cha kukwamisha utalii.(hapa nina ushahidi wa kutosha). isitoshe wanaiba sana mizigo yetu.

    pili bandari shida tupu. wizi wa kutisha. wanaiba hadi viatu achilia mbali vifaa vya kwenye gari kama radio hata fire extinguisher n.k

    tatu bara bara mbovu kupita kiasi na barabara za sehemu zenye mazao ndo kabisa simesahaulika.

    nne treni kwishneni kabisa. mwekezaji bomu. sijui alipatikana vipi.

    mwisho kabisa rushwa iliyokithiri. hatuwezi kupata maendeleo.

    mdau wa Arusha

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2010

    Msiokuwa na viwanja Dar changamkeni.Msiokuwa na mashamba kimbieni haraka Kibaha mkanunue.Wenzetu hata kama wanapesa hawana jeuri ya kununua ardhi maana walishauziwa walowezi tangu kabla ya huru,kama ilivyokuwa Zimbabwe.Sisi kuishi Kenya hatuwezi maana kila uchaguzi unaambatana na vita.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2010

    mdau wa Arusha umenena. wakati sisi bado tunasubiri misaada ambayo ni asilimia 10 tu ndo inamfikia mlengwa, wenzetu wanawekeza kiakili. kweli bongo ni bongo tu. tumeshindwa hata kudhibiti wizi kwenye bandari na viwanja vya ndege. kwanini mtu asipitie sehemu salama. tutashangaa tutakavyoachwa tumesimama

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2010

    Anoy hapo juu kula tano mwanangu umemwaga kila kitu. Hii serikali ya kifisadi haina program zozote zile inazozijua.

    ReplyDelete
  5. wenzetu ajira kwao ni issue. tuwe makini

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2010

    WE ANON WA KWANZA VIPI MI NILIFIKIRIA UTALIONA HILI LA KUUNGANA NA KENYA KUMBE WENZETU BADO WANAENDESHA NCHI KWA KATIBA YA WAKOLONI WALIOTUNGIWA BILA KUSHIRIKISHWA,NA BADO WAKO WANAO ISHABIKIA ISIGUSWE,TUTAWAMINI VIPI KAMA AWAJATUMWA NA WAKOLONI KWA MASLAHI YAO.UHURU WA KENYA NI UHURU WA BENDERA JELA ZA KENYA AFUNGWI MZUGU ATA AKIUWA.

    ReplyDelete
  7. Mama HellenasraJune 03, 2010

    mmh hapa sasa kazi ipo! watz tulivyo wavivuu!!!!!!! nahisi tutaishia kwenda nairobi kuwa mahousekeeper!
    Mtu ana kadiploma fulani tu basi anaridhika kabisa wkt wenzetu wapo juu kielimu lzm waje kutufunika.
    Tunajionea wnyewe kwnye mashindano ya vyuo kupitia zain,Wakenya ndo wanaonekana na upeo zaidi hvyo vyuo vyao kuingia fainali na hata kuwa washindi.
    Sie mmh wasomi wa vyeti tuuu.
    nahic tutaanza kuwa wanyonge kwenye nchi yetu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 03, 2010

    ok mdau wa kwanza hayo uliyoyasema tuseme ni kweli, jee wewe binafsi kama mtanzania mwenye uchungu na nchi yako umefanya jitihada gani kwa upande wako kukomesha tabia hizo? Au nawe ni kama walio wengi kukaa pembeni na kulalamika tu?

    Watanzania muda umefika wa kuacha kulalamika na badala yake kufanya ukweli kwa vitendo.

    Muda wa kusema enough is enough umefika, wanaoiba wanajulikana, wanaodai hongo wanajulikana kwani ni sisi sisi tunaowapa hizo hongo, wabadhirifu wa mali ya umma wanajulikana, wanaotumia madaraka kwa manufaa yao wanajulikana, wanaotumia vyeo na madaraka ya waume zao kwa manufaa yao binafsi wanajulikana. Kinachotakikana ni wananchi kuungana pamoja, kutokuwa na woga na kuwasimamia kidete wapewe adhabu kali na mali zao zote kutaifishwa! Hangon a minute! i must be dreaming hii ni tanzania,
    hakuna umoja, kila mtu anajali maslahi yake tu!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 03, 2010

    Hawa wakenya waamke mara ngapi jamani? mbona wameshakamata sana hilo soko, hebu watuache na sie tule kidogo sio hivi ka mchwa! wanaamshana tu!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 03, 2010

    Wakenya wenzi wangu jotokezeeni kugombea na kuchuma mali huku TZ. Nchi haina wenyewe kila mtu kivyake vyake. Tutapata ajira arizi tele.Hawa jamaa wanawanyenyekea wageni sana .Tutakuwa maarufu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 03, 2010

    haya shughuli imeanza wenzetu wanajipanga sie ndio kwanza tunatumia mabilioni kuiangalia brazil, walimu hawajalipwa pesa zao mshahara wa kima cha chini bado ni mdogo subirini wa kina kamau waje wachukue ajira zetu ardhi yetu ndio tutatia akili kichwani.baada ya hapo ndio tutasimama kwa miguu yetu wenyewe.
    kwa kweli nasikitika sana as naona hali itakavyokuwa mbeleni.degree owner atakavyokuwa shoeshine

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 03, 2010

    Haya mambo ya jumuiya ya Afrika Mashariki yananichosha sana.Ya kazi gani kujiwa na waKenya kufanya kile watakacho Tanzania wakati sisi wenyewe bado tunajitafuta..Wabaki huko huko kwao na mambo yao ya ukabila.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...