Mtumishi wa Mungu Christopher Mwakasege akiombea wa Tanzania ambao walijitokeza kwa wingi katika maombi maalum ya kuliombea Taifa letu la Tanzania na maziwa makuu,shughuli hiyo ilifanyika katika kanisa la Bethel World Outreach Church Silver Spring Md U S A
Pichani kutoaka kulia ni Mch Mwakasege,Balozi wetu wa Tanzania hapa Washington Mh Ombeni Sefue,Mr Jacob na Agustino Malinda ambao kwa hakika jitihada zao ndizo zilizoweza kufanikisha siku hii muhimu sana kwa Taifa letu.
Baadhi ya waumini waliofika katika maombezi ya Mchungaji Mwakasege.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Duh bongo zaidi ya uijuavyo wewe!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2010

    Mtumishi wa Mungu, ubarike sana na huduma yako. Mimi nipo nje ya Tz lakini kwa kupitia huduma yako ya masomo ya Mtandaoni, nimemuona Mungu kwa namna ya pekee. Ninatamani sana kuhudhuria maombezi yako physically, najua Mungu ataniwezesha tu. Bwana na azidi kukuinua katika jina lake Takatifu.Huduma yako ikafanyike kuwa baraka kwa wote waaminio.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2010

    Mimi ni mkristu na sijaelewa maelezo ya picha "siku hii muhimu kwa Taifa letu" naomba ufafanuzi
    Nielewavyo siku muhimu ya taifa letu ni kama siku ya Uhuru, Mapinduzi, Muungano, Ushindi vita vya Kagera n.k

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2010

    Jamani wenzetu wa USA mmebarikiwa kumpata mtumishi wa bwana Mwakasege. Jamani lini utakuja kwetu Canada??? Je mnafanyaje mpaka anakuja kuwalisha neno la bwana. I hope na balozi wetu siku moja ataona huo umuhimu akamwalika. Sefue mbona ukiwa hapa Canada hukufanya huo mwaliko?? watu tukapata upako.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2010

    MNA UBAGUGUZI HILO KANISA MBONA NI WAAFRIKA WATUPU HAMNA MZUNGU HATA MMOJA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2010

    Nsomba kufahamu kama Christopher Mwakasege amekuwa Mchungaji kwani ninavyofahamu mimi siku zote amekuwa ajielekeza kuwa yeye ni Mwalimu. Natumai wanaosema Mtumishi wa Mungu wako sahihi zaidi kuliko kumuita Mchungaji jambo ambalo yeye mwenyewe hajawahi kulikubali.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2010

    Anony wa Jun 03,12:22:00

    Ngoja nijaribu kukusaidia uelewe kwa nini siku ya kuombea taifa ni siku muhimu:

    Wakristo tunaamini kuna ulimwengu wa aina mbili yaani:
    1.ulimwengu wa mwili (unaoonekana kwa macho)
    2. Ulimwengu wa roho.

    Ulimwengu wa roho nao umegawanyika mara mbili yaani
    1.Ulimwengu wa roho wa nuru
    2.Ulimwengu wa roho wa giza.

    Mbambo yote yanayotokea katika ulimwengu wa mwili huwa yanaanza kutokea kwanza katika ulimwengu wa roho.

    Kwa mfano: Katika ulimwengu wa roho wa giza mtu anaweza kwenda kwa mganga kwa ajili ya kumtoa mtoto wake kafara. Kinachotokea hapa ni kafara kwanza katika ulimwengu wa roho halafu ndio kifo kinatokea katika ulimwengu wa mwili.

    Katika ulimwengu wa roho wa nuru vilevile mambo tunayomuomba Mungu leo, yanaanza kujibiwa katika ulimwengu wa roho kalafu ndio kesho tunayaona katika ulimwengu wa mwili

    Kwa hiyo tunapoombea taifa leo, sisi tunaona ni suku muhimu kwa taifa maana majibu ya maombi yetu ya leo katika ulimwengu wa roho ndiyo yanayopelekea mafanikio ya kesho ya taifa letu.

    Nadhani umeelewa kidogo. Mungu akubariki

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 03, 2010

    Mimi namkubali sana mch. Mwakasege hasa katika mahubiri yake. Kama anahubiri kwenye TV hata kama kuna mpira wa Chelsea lazima nimsikilize kwanza ndo niangalie mambo mengine, Bwana aendelee kumuinua.

    **Hivi kumbe wachungaji hawasumbuliwi kupewa VISA ya USA ubalozini Bongo eee!!

    Nkabo- Bongo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 03, 2010

    BRUNO Mazalli Mr London alikuwepo pia Luftansa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 03, 2010

    Katika maombi mchungaji naomba waombee wabongo wakumbuke kurudi makwao hasa wale waliokwenda kuuza sura na kusuka nywele.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 03, 2010

    Mtumishi natamani ungekuja huku russia nasi tupate upako.ubarikiwe sana.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 03, 2010

    Naomba kuelimishwa maziwa makuu ndio nini? siku hii ni siku gani kwa taifa hadi kusemwa ni siku umuhimu gani kwa taifa?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 03, 2010

    I wish I could be there, Mtumishi wa Mungu kupitia kwenye hii screen naamini napokea muujiza wangu ktk Jina la Yesu

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 03, 2010

    Hivi huko Washington DC hakuna wazungu? Au wao hawahitaji maombezi kama hayo?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 03, 2010

    huyu baba mchungaji hakika analisha kondoo wake malisho yaliyotukuka.mchungaji jaza upako mafisadi wana tanganyika wapate kombolewa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 03, 2010

    Badhani Lengo hasa ni kuwafikia watanzania ama wasema kiswahili ambao wako mbali na nyumbani na haya mambo yanawakosa. Ila hata wazungu huwa wanakaribishwa, mfano hata hapa UK huwa tunamualika mwalimu Mwakagege na wazungu huwa wanahudhuria tunawatafsiria.
    Nafurahi mno kuona neno la Mungu linahuiriwa na maombi ya muhimu kama hayo ya kuliombea taifa letu ili liendelee kuwa na amani yanafanyika....
    God bless u all.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 04, 2010

    barikiweni sana na mwl.mwakasege Jehova akuinue sana na akulinde dhidi ya ukengeufu na vita vya ufalme wa giza

    nawapenda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...