Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema (pichani) akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo kwenye makao makuu ya jeshi hilo wakati alipozungumzia uvamizi wa kituo cha polisi cha Hedaru uliofanywa na wananchi 300 baada ya kuvamia kituo cha polisi na kuchoma moto pamoja na magari matatu na nyaraka mbalimbali kituoni hapo.

Akifafanua zaidi IGP Said Mwema amesema mnamo tarehe 28-5-2010 mtoto mdogo aitwaye Garce Kelvin mwenye umri wa miaka 5 alitoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha akiwa anatokea shule ya chekechea katika mji mdogo wa Hedaru, baadae katika hatua za ufuatiliaji zilipokelewa taarifa kuwa mtoto huyo amepelekwa katika kijiji cha Chome Mlimani katika msitu wa Shengena ambako pia kuna machimbo ya Dhahabu kwa imani za kwamba huenda ameenda kutolewa kafara huko kwa imani za kishirikina.

Tarehe 30-5-2010 mkuu wa kituo akiongozana na wapelelezi walifuatilia taarifa hizo zilizopokelewa kutoka kwa wananchi ambapo katika oparesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wapatao sita na waliendelea kuhojiwa katika kituo cha polisi Same.

Mnamo tarehe 31-5-2010 kulitokea kundi lingine la vijana waliokwenda katika msitu wa Shengena kijiji cha Chome ikidaiwa walipata taarifa kwamba mtoto huyo amepelekwa kutolewa kafara kwenye machimbo ya dhahabu kwa imani za kishirikina, hata hivyo vijana hawa hawakufanikiwa kumpata mtoto badala yake waliwakamata watu nane wanaume saba na mwanamke mmoja waliowakuta na vifaa vya uchimbaji wa madiniya dhahabu na kuwapeleka kituo cha polisi Hedaru.

Majira ya saa mbili usiku tarehe hiyohiyo watuhumiwa wakiw akituoni Hedaru uvumi ulizagaa kwamba watu waliokamatwa na kundi la vijana ndiyo waliohusika na kutoweka kwa Grace Kaelvin hivyo kundi la wananchi 300 walivamia ktuo cha polisi na kuchoma moto kwa nia ya kutaka kuwauwa watuhumiwa hao, hata hivyo hakuna vifo vilivyotokea baada ya polisi kufanikisha kuwatorosha watu hao , leo tarehe 162010 mtoto Grace aliyetoweka aliokotwa sokoni eneo la Pasua na kwasasa anapelekwa kuungana na familia yake zaidi yahapo watuhumiwa watano wamekamatwa kwa kuchoma kituo.

Mwema amesema tabia ya kushambulia vituo vya polisi kwa hisia au kuchukua sheria mkononi kunavuruga amani na utulivu nchini, lakini pia ni uvunjaji wa sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 01, 2010

    That what happens when police do not do their job properly. Wananchi wangelegeza uzi tu mtoto asingerudi huyo. Tuko pamoja wanafamilia wa mtoto Grace.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 01, 2010

    Sijaona nchi yenye ushirikina wa kupindukia, mara mtoto kafara ya machimbo ya madini, mara ndugu zetu albino watawezesha watu kupata utajiri, mara mtu kaanguka toka ktk ungo akielekea Seycheles n.k

    Hivi watu wamekosa kabisa fikira mbadala ya kupata maendeleo Tanzania?

    Mdau
    Shimoni Kariakoo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2010

    Angalau mtoto amepatikana.

    Polisi anatakiwa awe rafiki wa raia; polisi jamii.

    Kuhusu hao waliochoma hicho kituo cha polisi moto, nadhani ni hasira tu, provocation; wame-react kutokana na kitendo cha hao waliotaka kwenda kumtoa kafara huyo mtoto. Sio kwamba nawatetea.

    Ni ule uchungu wa kufikiria mbali kwamba, ingekuwa vipi kama watu wasingeenda huko kwenye huo msitu wa hayo machimbo ya dhahabu na kumuokoa huyo mtoto? Si ingekuwa ni murder case - kifo cha huyo mtoto? Japo reaction yao imepitiliza kiasi, kufikia kuchoma moto kituo cha polisi. Polisi katika kuwashughulikia hao waliokamatwa kwa tuhuma za kuchoma moto kituo cha polisi, wajaribu kutilia maanani hisia walizokuwa nazo hao wananchi.

    Watu, acheni imani za kishirikina. Kama ipo, ipo tu. Hamna uhusiano wowote kati ya ushirikina na mafanikio. Ni imani potofu tu. Hivi mtu unalalaje usiku huku ukijua kuwa mali ulizonazo zinatokana na makafara? Unaua viumbe vya watu ili upate pesa? Siku ya mwisho sijui mtaficha wapi sura zenu.

    Huyo mtoto ajaribu kuhojiwa taratibu, pengine anaweza elezea alikuwa wapi, na kama alifanyiwa nini. Huyo aliyeanzisha huo uvumi kuwa mtoto anataka kutolewa makafara, pia ahojiwe taratibu tu, alijuwaje? Inaweza kuwa chanzo kizuri cha kumalizana na huo mzozo.

    Jinsi ambavyo polisi wamelichukulia suala hili la kuchomewa moto kituo chao cha polisi na pengine kunusurika hata na wao na 'watuhumiwa' kuchomwa moto, ndivyo vivyo hivyo inabidi walichukulie suala la uchomaji moto wa vibaka, kwani wanahukumiwa kabla ya kusikilizwa, na ni kinyume cha sheria pia.

    Maelezo na Mhariri wa 'Gazeti'.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2010

    Kitu kikiongelewa na radio mbao mara nyingi kinakuwa na ukweli ndani yake, jamaa baada ya kuona moto unawaka ikabidi wamwachie mtoto la sivyo ndio alikuwa amekwenda huyo kama watu wangetulia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 01, 2010

    Siungi mkono watu kujichukulia sheria mikononi, lakini panapofuka moshi ujue kuna moto. Polisi wafanye kazi invyotakiwa la sivyo wananchi wataendelea kupoteza imani nao na matokeo yake ni hayo. Hakuna mwenye uwezo wa kuzuia nguvu yya umma mifano iko mingi duniani. Hata uwe mabomu ya nuklia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 01, 2010

    Proof kuwa tanzania ukifata sheria za nchi hufanikiwi, wananchi wamechukuwa hatuwa mikononi mwao na kutaka kuwaua watuhumiwa siku ya pili tu mtoto kapatikana, polisi imewachukuwa muda gani?

    huko nyuma kuna watu walipendekeza jeshi lote la polisi livunjwe na kuundwa upya toka chini hadi juu naungana nao mia fill mia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 02, 2010

    Si support hii kitu lakini hiyo itawafanya Police wawe wanafanya lkazi zao kwa haraka haraka na kuwajibika zaidi.

    hata kama hakupelekwa huko kwenye misitu lakini ukweli upo pale pale mtoto wa miaka mitano ataondokaje Hedaru afike pasua mwenyewe?

    Mpaka apatikane aliyempeleka huyo mtoto huko na hao wachawi wanastahili kuchomwa moto kabisa.

    Ila na wazazi wakumbuke kuwa ulimwengu wa siku hizi si wakumwacha mtoto wa miaka mitano atembee peke yake

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 02, 2010

    Asante Yesu kwa mtoto kupatikana akiwa salama..

    ReplyDelete
  9. Mplang'ombeJune 02, 2010

    Jeshi la polisi linatakiwa kujiangalia lenyewe kuwa ni kwa nini hasa matendo kama haya yanatokea?. Adui mkuu wa Amani ni kutotenda haki, kama wananchi wanaona kuwa jeshi hilo halitendi haki ama kwa kupokea rushwa au kwa kuzembea majukumu yao ya kulinda mali na usalama wa raia, basi ni wazi kuwa wananchi watakosa imani na jeshi hilo. Huu ni mwanzo tu kwani tunapoelekea si pazuri hasa pale serikali kupitia vyombo vyake inapoonekana haiwajibiki ipasavyo. Nyerere aliishasema kuwa kitu kibaya zaidi kwa amani ya nchi yetu ni pale wananchi wanapokata tamaa na serikali yao.

    IGP na polisi kwa ujumla wanatakiwa kubadilika na kuwa na mtazamo waurafiki zaidi na raia wema kuliko uadui. Ni kweli kuwa wananchi hawa wamevunja sheria ya nchi kwa kuvamia kituo na kujichukulia sheria mkononi, lakini hili lingeweza kuepukika kama tu Jeshi la polisi lingeoneka na wananchi linachukulia matukio kama haya ya kupotelewa na mtoto kwa uzito wa pekee. Hiatoshi kutuma askari kanzu pekee, bali Polisi walitakiwa si tu kuonekana bali kufanya kazi yao ipasavyo.

    Ushauri kwa IGP ni kwamba, mpaka pale watakapoona kuwa jeshi la polisi linatakiwa kufanya kazi kisasa zaidi kuliko wakati wa zamani wa kuonekana kuwa jeshi la polisi ni adui wa raia kwa manufaa ya watawala pekee, basi wafanye yafuatayo:-

    1. Kurecruit watu wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kabla ya kuchukua hatua kama za kupiga watu n.k

    2. Mbinu za kipelelezi za mateso na unyanyasaji katika kutafuta ushahidi ziharamishwe, ziwe illegal

    3. Jeshi litumie mbinu za kisaikolojia zaidi katika kutafuta ukweli kuliko mbinu za kutisha wananchi kwa kuwapiga risasi ama kuwatesa kwa kuwakalisha kwenye ncha za chupa wakiwa uchi au kuwapiga short ya umeme au kuwachoma na kiberiti cha gesi sehemu za siri.

    4. Polisi kuacha kuomba na kuchukua rushwa toka kwa raia ambao wanaona kuwa hawana mtetezi kwani kama huna pesa ujue wewe ni wa kuonewa katika nchi yako.

    5. Jeshi liache kubambikia raia wema kesi zisizo na kichwa wala miguu ili kutengeneza mazingira ya rushwa.

    6. Sijui kama Mwema anafahamu kuwa vituo vya polisi vimegeuzwa kuwa sehemu za biashara, yaani unapoenda toa taarifa ya uhalifu unatakiwa kulipia kiasi fulani ili kuweza kufanikisha muhalifu kukamatwa na akiisha kamatwa pia hata kama akionekana hana kosa basi haachiwi hivihivi tu lazima pia pesa itoke(wakati mwingine wanaita KUINGIA BURE KUTOKA PESA)

    Ni dhahiri wananchi wamechoshwa na hali hii, hata kama jeshi litaamua kuwafunga wananchi wote hao 300 bado haitasaidia kitu. walichukulie tatizo hili kwa mtazamo chanya kuwa ni changamoto ya wao kujiangalia wakoje na kubadilika. Kama kuna hawawezi ni bora wale askari wote wenye mtazamo wa kimakamenguvu wakastaafishwa kwani tunakoelekea ni dhahiri kuwa bunduki na mabomu pekee havitoshi kuwazuia wananchi kufanya watakayo huko mbeleni, kwani kwa baadhi yao kuishi na kutoishi kunaonekana hakuna tofauti. You can't be unfair to good citizens and expect them to behave fairly to you.

    Katika mambo ya anger management kuna vitu vikuu viwili:-

    (a)"TRIGGERS" - hivi husababisha vurugu na ghasia miongoni mwa raia pindi vinapofanyika na kwa bahati mbaya zaidi ni kuwa Jeshi la polisi Tanzania linafanya kazi zake zote kwa kutumia vitu hivi.

    (b)"INHIBITORS" - Hivi ni vitu ambavyo vinatakiwa kufanyika ili kuweka hali ya amani na masikilizano, kama kuacha kutukana watuhumiwa, kuacha kuwapiga virungu, kutowatesa, kutowaomba rushwa n.k. Bahati mbaya ni kwamba jeshi letu limejitenga hivi vitu. Ndiyo maana wananchi wanakuwa na hasira kuanzia na polisi wenyewe mpaka na watuhumiwa.

    Jeshi la polisi livunjwe na kusukwa upya, hili linawezekana, tangaza tu nchi inapeleka ulinzi wa raia kwa jeshi la wananchi kwa miezi sita na polisi inavunjwa na watu wanapelekwa mafunzo watakaofaulu watarudhishwa wakiwa na mtazamo mpya wa kufanya kazi.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 02, 2010

    kutoka Hedaru hadi mtoto kupatikana pasua sokoni mbona ni mbali sana! Hii inasikitisha sana! Jitihada za wananchi zimesaidia sana kupatikana kwa huyo mtoto, kwa story hii bila hizo jitihada za wananchi mtoto asingepatikana! ila wamechemsha sana kuchoma moto kituo cha polisi! watu tunalia kila siku vituo vya polisi viongezwe wao wanachoma!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 02, 2010

    Nimeipenda hii..Wananchi wanainuka na wanachukua hatua..kama serikali imejaa ifisadi na haiwasilizi..tufanyaje...this is the only means kurudisha redemption tuliyoipoteza toka Nyerere atoke madarakani...Wamejaaa matapaeli na mafisadi du serikali ya sasa..Na bado..wait uchaguzi..mtaona mengi

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 02, 2010

    mi nadhani itafikia wakati sasa hata mafisadi inabidi wafatwe makwao maana sheria imeshindwa fanya kazi,watu hawana imani tena na dola kwa kifupi.Ni kweli ni uvunjaji wa sheria lakini kama ham-amiki unafikiri jamii itafanyaje?Kuna haja ya mambadiliko makubwa sana katika uongozi mzima wa nchi yetu la sivyo tutafikia mambo ya kuuwana hadi mitaani kwa kuona kwanini huyu anatumia gari ya kifahari mi sina hata baiskeli.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 02, 2010

    Kuchukua sheria mkononi ni ishara ya wananchi kutokuwa na imani na vyombo vya sheria. Bw Mwema unatakiwa kushirikiana na wananchi na kuchunguza kwa nini wanafanya hivyo na kurekebisha jeshi lako, huo ndio ufumbuzi wa kudumu!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 02, 2010

    Ikiwa mtoto huyo kapatikana basi ni kweli kabisa walitaka kumfanyizia, ila watu wameungana... binafsi wala sikasiriki walivyounguza kituo manake labda hata polisi walikaa tu kimya hawafanyi kitu kama kawaida wanasubiria hongo tu. Nikiwa kama mzazi kwa kweli nitaua eti umwibe mwanangu?
    Pesa hii itatuua.... kwani sie tunaofanya kazi za kawaida tu mbona tunaishi japo kwa shida? wenzetu ndio watake kumtoa mtoto kafara?
    Mwisho kabisa uchungu wa mwana aujuae mzazi... wengine wote ni hawataona kitu ila hii ni fundisho kwa wote watakaotaka kuiba watoto wengine kwa manufaa ya "TAMAA"

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 02, 2010

    Mniibie mwanangu ndio mtanijua mi nani, babangu mchawi kijiji kizima wanamwogopa, mi binafsi nishaanza kukabidhiwa kwahiyo jaribuni mtanijua

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 02, 2010

    SI WATU WALISHASEMA SERIKALI IMELALA HIVYO WANANCHI WANACHUKUA SHERIA MKONONI NA KUFANYA WANALOONA LINAFAA. NA BADO.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 02, 2010

    Ndugu IGP Mwema, sidhani kama wananchi kuchukua sheria mkononi kama ni jambo geni miongoni mwa waTanzania. Unaonaje kama kungetafutwa sabb ya kwa nini wananchi wafanye hivyo! kuendelea kukamata wanaojichukulia sheria si suluhisho. Wananch hawa wamekosa imani kwa polisi. Jenga maadili miongoni mwa polisi. Polisi akikosea analindwa kama nini! lakini raia akikosea kwa kutomwamini polisi mvujna maadili anaadhibiwa vibaya.Washauri polisi wamrudie Mungu wetu,kama imeshindikana kuwadhibiti,
    wawatendee haki wananchi, na kujichukulia sheria kutaisha.

    Hebu Mr IGP fikiria kama angekuwa ni mwanao aliyekuwa amepotea na ukaamini kweli kachukuliwa kutolewa kafara, ungefanyaje?

    Mie naomba , jinsi wanavyoachiwa mapolisi wakikosa, na hawa jamaa waachiwe.

    mzalendo

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 02, 2010

    Eneo la Hedaru ni kichaka cha majambazi na wavunja sheria. Juzi tu tukisafirisha msiba tulipewa taarifa kuhusu mabedui walojificha vichakani. Hedaru iku mbali kiasi toka Same na Mombo hivyo mavunjifu wa amani hujificha hapo. Hedaru is too remote from regional HQs in Tanga and Kilimajaro making the few policemen do whatever they wish/lax.
    Matokeo ya wananchi kujichukulia sheria mikononi huko Musoma. Shinyanga, visiwani na Hedaru husbabishwa na wasimamizi wa haki kutowatendea haki wananchi, has wanapopokea rushwa toka kwa wahalifu. Matokeo ni kughafilika au frustration na matokeo ndo hayo. IGP afanye utafiti ndani ya jeshi na kufanya marekebisho. Mimi mwenyewe nilipigwa risasi na majambazi kwenye awamu ya pili na ikaonekana walofaywa hivyo ni walinda amani. We call for total overhaul of the police force followed by improved welfare/motivation.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 02, 2010

    Mkome kabisa na watoto wa Kipare...!! No more comments,
    Mdau-NYC, USA

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 02, 2010

    Amani na utulivu vimeanza kuyeyuka...

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 02, 2010

    Hivi watanzania walio wengi ni kwa sababu ya ukosefu wa elimu!? Huwa tunaamini uvumi na kuchukua hatua kali bila hata kuuliza! Leo mtaani mtu akiitiwa mwizii..watu wanaanza kushambulia bila hata kujua kaiba nini na wapi. Watu wengi wasio na hatia wameadhibiwa kwa hukumu hizi za kuvumisha na kusingiziana. Halafu hii sheria ya kuuwa watuhumiwa mbona inashika kasi sana, eti wananchi wenye hasira. Ni kweli vyombo vya dola kuna rushwa na uzembe hivyo wakati mwingine haki haitendeki au inachelewa, lakini solution ni wananchi kujichukulia hatua mikononi? Tuna uhakika gani kwamba huyo aliyeitiwa mwizi au muuaji ni kweli kafanya hilo kosa? Nchi yoyote duniani haiwezi kutawaliwa bila sheria. Lazima tujifunze kufuata na kutii sheria bila kujali kama imekuathiri kiasi gani. Vibaka wanaolalamikiwa kwamba wakipelekwa polisi huwa wanaachiwa, ni kwa sababu walioibiwa huwa hawaendi kutoa ushahidi. IGP Mwema amelibadilisha sana jeshi baya la polisi alilorithi toka kwa dikteta Mahita na angalau siku hizi polisi wanafundishwa customer service..polisi jamii n.k, kwanini raia badala ya kuwapa ushirikiano tunawashambulia? Tuwaache wafanye kazi yao kwa amani.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 02, 2010

    Naomba kumuelewesha mkuu wa polisi kuwa wananchi hawashambulii vituo vya polisi bila sababu.Polisi wamekuwa chukizo mbele ya wananchi..polisi wanakula rushwa, wanaachia wafungwa mpaka wale wanaohusika na mauaji, wezi wa kutumia silaha n.k. na pia polisi wanaazima/wanakodisha silaha kwa majambazi. Wananchi wa Tanzania tumechoka na hivyo vitendo vya polisi ambavyo wakubwa wake kama Mwema wanajifanya hawaoni.POLISI TENDENI HAKI SIKU ZOTE hakuna mtu atakayegusa vituo vyenu au vitendea kazi vyenu. Msiseme hizo ni hisia bali ni ukweli usiopingika tuna jeshi la polisi ambalo ni dhaifu na corrupt kuliko pengine nchi yeyote duniani, hatuoni kazi wanayofanya zaidi kujihusisha na rushwa na unyang'anyi.Itafika siku hasira za wananchi hazitaishia kwenye vituo na vitendea kazi vya polisi bali zitakuwa kwa kila polisi anayeonekana...tunaomba tusifikie hapo.fanyeni kazi

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 03, 2010

    mafisadi kuwafata makwao ndio linalo fuata maana selikali iko likizo na jeshi la polisi liko hanimuni itabidi wananchi waingie kazini kutetea nchi yao kuwaburuza mafisadi na kuwachapa viboko mmoja baada ya mwingine na kuwasurubisha msalabani.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 03, 2010

    TWENDE MBELE TURUDI NYUMA HIVI VITUO VYA POLICE VINAVYOFANYA KAZI HUKU MIJINI SI SAWA NA VIJIJINI, huu ni mtazamo wangu kiasi kwamba hadi raia wachukue hatua kama hizi ina maana wamechoshwa na tabia ambazo zinazembewa na hawa mapolice. mfano kimara majambazi kila kukicha si kama kwamba police hawaelewi ama hawajui nini kinawasibu wananchi ila wao wanaona kama sehemu haina maslahi na wao ya nini wahangaike? JAMANI SISI TUNAYAONA HAPA KIMARA.

    Inachosha hii jamani wananchi si wajinga.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 03, 2010

    Mhe IGP hii ni mwanzo tuu,muda si mrefu hawa trafiki wako wataanza kula kichapo hapa jijini manake wamezidi kuvuta gari za barabara moja wengne mnakaa zaidi ya dk 50 kny foleni,sasa subiri raia washaanza kuwatolea maneno machafu hao wazee wa feva mf ni yule aliyekuwa pale magomeni usalama jana jioni,siku abiriA wakishindwa kuvumilia utasikia mengne. msije mkawatafuta raia ubaya. HIZI NI SALAMU KWAKO MJOMBA!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...