Kikosi cha Wazee Ugiriki
Kikosi cha vijana Ugiriki

Timu ya wazee Ugiriki iliweza kusawazisha katika dakika za majeruhi na kutoka droo ya 2-2 na vijana wa jiji hilo kwenye uwanja wa Faliron Piraeus wikiendi ilopita.
Vijana ndio walianza kufunga dakika ya 30 kwa bao la KASSIM LIGOPORA kabla HOZZA hajaongeza la pili.. Wazee nao walipapatua kwa goli la AZIZ katika kipindi cha pili na MILALA aliokoa jahazi katika dakika za majeruhi.
Kwa kuwa kila timu ilijiamini kuwa ni bora na mshindi kukosekana, inafikiriwa kuandaliwa mechi ingine na wadau waliopo nchi za jirani na hata nchi za mbali wanaalikwa kwenda kushuhudia pambano hilo la marudiano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2010

    Ndio ALLY AMIR AKIDA kama nakuona unelishika duara la wazee nakufananisha na ALLY MAUMBA.
    Mdau
    Kisiju pwani

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2010

    naimiss umangani. Kumbe uwanja wa Faliro bado upo? Nausudu sana sistimu yenu bab kubwa.endeleeni hivyo hivyo na sisi ingawa hatupo huko lakini tupo nanyi kwa moyo wote

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2010

    sawa shalamar bado unaweka mwili safi waonyeshe vijana messina line ulivyokuwa ukifanya mavitu yako enzi hizo mitaa ya magomeni ninaimani wawekukubali..mwambie kassa asijifiche tumemuona. mdau kondoa street magomeni

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2010

    Tupeni majina ya hao wadau - Sabri yumo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...