Warembo 18 wanaoshiriki mashindano ya kumtafuta mlimbwende wa Kanda ya Ilala, watatembelea vyumba vya habari vya magazeti mbalimbali kujifunza jinsi magazeti yanavyotengenezwa na kukutana na waandishi wa Habari na wahariri ambao wamekuwa wakiwasikia tu au kuwasoma bila kuwajua.

Afisa wa Redds Miss Ilala amesema: "Sisi tunajitahidi kuwafundisha warembo wetu kuwaona waandishi wa habari kama marafiki na watu wa kushirikiana nao na wala si maadui kwa kudhani kuwa watawaandika vibaya".

Saa nne Alhamisi walikuwa magazeti ya serikali Dailynews na habari leo, saa tano, Jambo Leo halafu wakaenda Business times na kumalizia Mwananchi Communications. Leo wataendelea na ziara hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2010

    OK, mmependeza. OMBI: Mmeshakuwa watu maarufu, umaarufu usiwaleweshe mkajisahau na kuja kufanya mambo ya ajabu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2010

    Jamani utamaduni wetu emebadilika sana,nadhani niliondoka bongo zamani sana. Mbona sioni hapo hata mmoja mwenye miguu ya chupa ya bia? sioni hata mmoja aliye jaziajazia? wote wamepigwa pasi kiaina,ndio beauty ideal za siku hizi hizo?

    Enzi zetu ukikosa demu aliyejazajaza ndio unachukua hao,halafu uwe tayari kutaniwa na washkaji eti mshkaji demu wake ana miwa!;);)LOL.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...