Waziri wa afya Mh. Prof. David Mwakyusa akiwasili katika viwanja vya hospitali ya mkoa wa Dododma ili kupokea wodi na vifaa vilivivyotolewa na Benki ya CRDB, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Charles Kimei, Naibu Waziri wa Afya Mh.Dr. Aisha Kigoda na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh.James Msekela.
Waziri wa Afya Mh.David Mwakyusa akikata utepe kufungua rasmi wodi ya kinamama ya hospitali ya mkoa wa Dodoma iliyokarabatiwa kwa msaada wa Benki ya CRDB.
Mh. Waziri akiongea na kinamama waliolazwa hospitali ya mkoa wa Dodoma iliyokarabatiwa kwa msaada wa Benki ya CRDB. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dk. Kimei
Waziri wa Afya Mh.David Mwakyusa, akifurahi vitanda vipya vilivyotolewa na Benki ya CRDB huku akishuhudiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei na Mkurugenzi wa Masoko Bi.Tully Mwambapa.
Sehemu ya wodi ya hospitali ya mkoa wa Dodoma iliyokarabatiwa na CRDB






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2010

    kwa rasirimali tulizo nazo Tanzania hatuhitaji kusubiri mabank yatusaidie na hivi ndivyo kila kata inatakiwa kuwa na hospitali/zahati zenye mazingira mazuri bila kusahau kitanda kimoja mgonjwa mmoja. Hongereni CRDB,hongera Dk. Kimei lakin pia nyie serikali msiishie kufungua tu . hao wanawasunta na chukulieni km changamoto mkajadiri kwenye vikao vyenu huku bungeni,baraza la mawaziri na kukwingineko kwa mustakabali bora wa watanzania na si kukalia ufisadi. sasa hii usiweeke we michuzi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2010

    Asanteni CRDB bank, kwa msaada. Ila kwa mtazamo wangu naomba msiandike majina kwenye shuka mgonjwa anaweza asipate nafuu. Kwa mfano unaenda benki ya CRDB kufuatilia malipo yako huku nyumbani umeacha wadeni wanakusubiri, kufika benk hela haijaingia, au chek haijaklia. Ghafla pressure inapanda ama kushuka maru pu chini. Unachukuliwa hadi hospital, kufika unapata huduma ya kwanza, unazinduka, ghafla pembeni unaona tena CRDB , nahisi utazimia tena maana akili inarudi kule kule benki.... Sijui lakini wadau mnasemaje, au andikeni kwenye ufito ili ikitandikwa maandishi hayaonekani, au mnataka mileage kiana?

    Vipi huko nyumbani jamani? Nimetamani Mbege ( hata "Ngera" nikipata nakunywa)

    Mdau Kiwoso
    Ukerewe

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2010

    Mdau wa Ukerewe Kiwoso una macho kama mimi, kwakweli branding mbovu, wangeweka kalogo kadogo au hata wangeweka kwenye label ya shuka au wanaogopa zitaibiwa but still sijapenda Kama wa marketing au Pr wanaona fanyeni lirekebisheni hili next time

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2010

    Hee hebu waacheni wakitoa zawadi lazima waandike watakavyo..

    Mimiombi langu ni hao wafanyakazi waweze kumainain usafi huo kama ilivyosasa ni jana tu nilikuwa na mwanangu ER nikawanaangalia kulivyo kusafi na nikajiuliza kwanini wenzetu waweze kutunza hivi na siye tunashindwa/

    Ukiwapa miezi mitatu hayo mashuka yote yamehamia kwa who knows who...utayakuta tu mtoni yanafuliwa na watu wanyumbani wameshajiibia tayari...

    Poor Us

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2010

    Dah mdau wa UKWEREWENI NOMA. Umenichekesha sana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2010

    mdau wa ukerewe hujatulia nimecheka kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...