Katika mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania,mojawapo ya mambo ambayo tumedhamiria hapa www.bongocelebrity.com ni pamoja na kuvipa vyama vyote kisiasa nchini Tanzania, nafasi ya kunadi sera zao kwa watanzania walio ndani na nje ya nchi,kuwasiliana nao kupitia hapa, kufikisha ujumbe wao kwa wadau wa michakato ya kidemokrasia ulimwenguni nk.

Hivi karibuni tutafungua msururu wa mahojiano na baadhi ya waliokwisha kutangaza nia ya kugombea nafasi za kisiasa iwe ni Urais au Ubunge ili wananchi,wapiga kura wa leo na kesho,wajue kwa undani sera na ushawishi uliopelekea mtu fulani kujitokeza kama mgombea na hivyo,kama atachaguliwa,atakuwa kiongozi wao katika mapambano ya kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali kwa miaka mitano ijayo. Kama wewe ni mgombea na ungependa habari zako,sera zako nk ziwekwe hapa,unaweza kuwasiliana nasi kwa kupitia barua pepe;
au
www.bongocelebrity@gmail.com

Sasa ili kupata mahojiano yaliyo bora na yenye usawa,tumekuwa tukipitia katika tovuti rasmi za vyama ili kutizama kwa makini sera,historia na habari kuhusu wagombea mbalimbali kupitia vyama hivyo ili kupata habari za uhakika,zilizopitishwa na vyama husika na hivyo kuboresha uwazi na usawa tunaojaribu kuuzingatia.

Kwa bahati mbaya, katika chambua chambua yetu mtandaoni,bado hatujafanikiwa kuziona tovuti za vyama vya Tanzania Labor Party(TLP) na Chama Cha Wananchi-CUF(Civic United Front).
Juhudi zetu za kuwasiliana na vyama hivyo kupitia anuani za barua pepe ambazo tulifanikiwa kuzipata kupitia mtandaoni,hazikuzaa matunda kwani barua pepe zote ziliturudia zikiashiria kutokuwepo hewani kwa anuani hizo!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2010

    So what?!!!! Kwa nini unapublish kitu kama hiki??? Mtandao au email ni moja ya njia tu kupelekea mawasiliano, kuna nyingine nyingi. Kama umekwama kwa njia hizo basi fika kwenye ofisi husika watakupa habari unayotaka, au?! Na kama una nia nzuri na lengo lako kwa nchi, kwa nini unaanzisha mgogoro kati yako na vyama hivi?? BE PROACTIVE, NOT REACTIVE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2010

    MNASHANGAZA SANA, YAANI HATA 'GOOLE SEARCH' TU HAMUWEZI? AU NI CAMPAIGN CHAFU? KWA SUALA SERIOUS KAMA HILO, MNASHINDWA HATA KUTUMA MTU TU TENA KWA MGUU OFISINI KWAO? KWA KUWASIDIA WEBSITE YA CUF NI

    http://hakinaumma.wordpress.com/

    M.W.IS

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2010

    Kama ni kweli hivi vyama havina website basi kweli nchi imeliwa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2010

    yaani ina maana chama cha CUF kinatumia free platform badala ya kuwa na tovuti kamili.Mdau mimi nadhani labda hiyo hapo juu ni blogu yao na sio website rasmi na TLP je?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2010

    Official Website ya CUF ni www.cuf.or.tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...