Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Huduma ya maji kwa Jamii Mhandisi Frida Rweyemamu(watatu kushoto) akitoa maelezo ya mradi wa maji jana wakati Rais Jakaya kikwete(katikati) alipokagua bwawa kubwa la maji katika mji wa Mugumu wilayani Serengeti jana.Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.Rais Kikwete ameshauri mradi wa ufugaji samaki na uvuvi ufanyike katika bwawa hilo. JK akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mji wa Mugumu waliojitokea kumlaki wakati wa ufunguzi wa mradi wa maji mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti.
JK na Waziri wa Maji profesa Mark Mwandosya na Mbunge wa Serengeti Dr.Wanyancha wakijadiliana jambo wakati wa ufunguzi wa mradi wa maji katika Mji wa Mugumu,wilayani Serengeti
JK akiwapongeza vijana wadogo wawili Brittany Scalciewicz(10) na kaka yake Joey Scalciewicz kutoka jimbo la California nchini Marekani ambao wako nchini Tanzania kwa utalii na walifanikiwa kupanda na kufika kilele cha mlima Kilimanjaro hivi karibuni.Vijana hao wadogo pamoja na wazazi wao wanaitembelea mbuga maarufu ya Serengeti ma walikutana na Rais Kikwete katika uwanja wa ndege wa Seronera,wilayani Serengeti wakati Rais Kikwete alipokwenda kuzindua mradi mkubwa wa maji katika mji wa Mugumu jana
JK akikagua moja wa faru weusi(black rhino) waliorejeshwa nchini kutokea Afrika ya Kusini hivi karibuni katika makazi yao ya muda huko mbuga ya Serengeti.Faru hao baadaye wataachiliwa na kuishi katika mazingira ya asili.Rais Kikwete aliwakagua faru hao wakati alipokuwa njiani akitokea mji wa Mugumu wilayani Serengeti ambapo alizindua mradi mkubwa wa maji na kuongea na wananchi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2010

    Tajiri mmoja wa kimarekani ka-donate hao faru 40 toka south Africa to Tanzania, na si kwamba walishakuepo Tanzania, wakapelekwa S.Africa na sasa wamerejeshwa HAPANA, tumeshazoea vyakupewa, hili nalo ni moja wapo.,..tunashindwa zuia ujangili ili wazaliane tunasubiri majangili wamalize ili tupewe, haya sasa na hao 40 tutawalindaje na majangili? Selikali tafadhali chukueni hatua, sisi tunalipa kodi tukitegemea mtatuulindia urithi wetu huo wa asili na si vinginevyo.

    REMSI,IRINGA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2010

    Hao watoto watakavyokwenda kuhadithia huko kwao? That is nice picha moja hiyo itaengeza watalii 50 form those kids....

    Thumb up for this Mr president

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2010

    Jamani JK chonde chonde Kiboko si Mbuzi jamani hivi akibumburuka hapo hiyo shuhuli yake si itakuwa balaa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2010

    au mimi sijui kiswahili!! kwanini mnatumia raisi kukagua kitu fulani kwa mtazamo wangu mimi mtu anayekagua lazima ajue kitu hicho kwa undani au katika ukamilifu kinatakiwaje sasa ina maana rais yeye anajua kila kitu maana kila kitu huwa anakagua naomba labda muwe mnatumia rais akiangalia asante

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2010

    Hilo coat lilipelekwa bagamoyo nini au na yeye ana mengi ya rangi moja kama yule mtangazaji aliyejitetea juzi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2010

    RAIS AKIWAANGALIA VIFARU SI KUKAGUWA KWANI YEYE NI MTAALAMU WA WANYAMA? HE IS NOT A VETERINARY OFFICER

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2010

    Wewe Obama akienda kwenye mitambo ya solar power system, wind power system, jana kwenye mitambo ya broadband internet speed na kuikagua na kufafanua juu ya fund wanayoitaka kuianzisha kwa ajili ya kuzidisha internet speed USA anajua mambo hayo yote? Mbona hayo husemi? Acha kizabina zabina na kiherehere give credit when its due....Mimi sio CCM na wala siipendi kabisa lakini mahali panaoneka panaukweli tuache umbeya. Ndio tunajua fika kuwa mengi yanayofanyika siku hizi ni kutokana na uchaguzi ujao lakini better late than nothing all politicians are the same toka enzi za Julius kaisari ..

    K

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 05, 2010

    aliyesema wewe ni ccm nani?
    wewe ndo unakizabina zabina
    hata huyo obama nae alikuwa akiangalia huyo mitambo ya intanet
    akague kwani yeye ni mhandisi wa tehama?
    hata hao wamarekani kama walitangaza kuwa obama alikagua nao walikosea

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 05, 2010

    watoto wadogo ivo wamefika kileleni?haaaa basi na mimi nitaweza kumbe ebu nile tizi ndog

    JK na faru

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2010

    OBAMA HAKWENDA KUKAGUWA MITAMBO ALITEMBELA MITAMBO KUPATA UFAFANUZI ZAIDI WA KITU KINACHOENDELEA, SASA SWALA CREDIT LINATOKEA WAP HAPA, TUMPE CREDIT KWA VIPI, YAANI KUTMBELEA VIFARU APEWE CREDIT! FOR ME THAT IS CHEAP AND SIMPLE POLITICS,HAKUNA MTU HAPA AMESEMA HAFANYI KAZI NZURI, AFTER ALL THAT IS AMONG ONE OF HIS DUTIES. KILICHOJADILIWA HAPA NI LUGHA SI UTENDAJI WA RAIS. IF YOU SEE THINGA AT THAT NARROW ANGLE BASI KUNA KAZI NDO MAANA WABUNGE WABOVU WANAENDELEA KUCHAGULIWA YEAS AFTER YEARS THE SAME MAN KIASI KWAMBA WANACHUKUWA FOR GRANTED KUWA NAFASI HIZO NI ZAO NA WANAGEUZA POLITICS AS JOB FOR LIFE NA KUFANYA NDO CAREER YAO KIASI KWAMBA MAWAQZO MSETO NDO YANATAKIWA KULETA MSUGUWANO WA MAENDELEO, MBUNGE AKIGAWA PIPI NA KUTEMBELEA VILABU VYA POMBE BASI TUMPE CREDIT NA TUMCHAGUWE KIPINDI KIJACHO CHA UCHAGUZI, MMMM SI HIVYO JAMANI

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2010

    Heheehheee! Halooo! Mtajibeba mwaka huu! Na bado.

    JK uko juu kama mukungu gwa ndizi, hao si watoto wa makwabela hao ni watoto wa mamilionea, inaonyesha safari zako za US zimeleta watalii mamilionea Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...