Katibu mkuu wa Ashanti United Haji Bechina

Klabu ya Ashanti United ya jijini Dar kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wamepanga kuwaombea duwa marehemu wote waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo itakayofanyika katika shule ya msingi ya Ilala Boma.

Katibu Mkuu wa Ashanbti Bw. Haji Bechina aliwataja watakaosomewa duwa hiyo kuwa ni pamoja aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyekuwa Mlezi wao Rajabu Mgodo, Athumani Nobi waliokuwa makatibu katika vipindi tofauti na Mzee Mwalimu Kinyogori ambaye alikuwa mwenyekiti.

Bechina alisema kuwa klabu zote za mpira wa miguu zilizopo jijini Dar es salaam pamoja na wadau wa mchezo wa soka wamepewa mialiko kwa kushiliki duwa hiyo itakayofanyika jumapili hii ya Julai 25.

Aidha klabu hiyo imepanga kuisuka upya timu ya soka ya Ashanti United baada ya kupoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni. Mbali na soka Ashanti pia hujishughulisha na uinuaji wa vipaji vya mchezo wa ngumi kupitia kocha wake Rajabu Mhamila a.k.a Super D.

Bechina aliongeza kuwa wanajivunia timu hiyo ya ngumi ambapo mchezaji wao Joseph Richard, alimpiga kwa KO ya raundi ya pili Kijepa Omari katika pambano la utangulizi kabla ya Rashidi Matumla na Mada Maugo kwenye ukumbi wa P.T.A Ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2010

    Vizuri kaka Bechina.
    Wapi Chosta?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...