Juu na chini: Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah akipokea msaada wa Komputa 18 zenye thamani ya zaidi ya million 20 toka kwa Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Young – Hoon Kim. Komputa hizo zimetolewa na Ubolozi huo nchini kusaidia matumizi mbalimbali kwa waheshimiwa na watumishi wa Ofisi ya Bunge. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Young – Hoon Kim akimweleza katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashililah namna nchi hiyo inavyokusudia kusaidia Bunge la Tanzania katika maswala ya Teknolojia ya mawasiliano mara baada ya kukabidhi msaada wa Komputa 18 zenye thamani ya zaidi ya million 20 katika Ofisi ndogo ya Bunge Dar es salaam jana. Waliosimama toka kulia ni Mkurugenzi wa Mipango na ICT wa Bunge ndg. Siegfied Kuwite na Msaidi wa Katibu wa Bunge Emanuel Mpanda. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mdau, BlooomsburyJuly 08, 2010

    Sasa tutaingiliwa hadi uvunguni!!
    Yaani hadi BUNGE linapewa msaada! Tena wa milioni 20!


    Je, hizo kompyuta zimefanyiwa uchunguzi wa virusi na programu nyingine za kunasa taarifa?

    Najua kuna watakaosema Tanzania ni taifa dogo sana kwa Korea ya Kusini kutaka kuchunguza chini chini lakini ni bora kuwa waangalifu.

    Hizo kompyuta zitolewe kwenye shule

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 08, 2010

    Siyo msaada Watanzania.

    Hakuna mwanaume yeyote amanyeweza kuto mali yake hivi hivi.

    Wenzetu wajanja, wanajua pa kurudishia, si tutawachekea nakufurahia? Watatulazimisha tununue magari yao au, si tuna kilimo kwanza, watatuletea mbegu za mpunga badala ya kununua kilo moja kwa shs 250 tutanunua kwa shs 250,000.00 Mtu mweupe mtu!!

    ReplyDelete
  3. Ninyi serikali ya Afrika, muache mambo ya omba omba, ninyi munaomba mupaka computer, nyinyi hakuna hata aibu, mufanya kazi mununue, siyo kuomba.

    kama munatoka hapo, munawapa zawadi sa shimo ya dhaabu, mujinga sana

    Mujomba Paulo Kamau
    Nakuru Kenya

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2010

    Halafu mutumie hizo computer kwenye mambo ya muhimu ..mtashangaa na roho yenu na kukuta kila kitu kinasomwa na wenye computer zao..


    Kamau nipo na wewe kwa hili...kasumba mbaya sana hii. Tumezoea kutembezza mabakuli halafu hela zetu tunatumia kwenye party na semina zisizoisha. Million ishiniri tulishindwa kweli kununua peke yetu au maubongo yetu yamedata tu. Walikuja wakakuta hatuna hizo pc wakaopna watuletee kumbe wala wanaohusika walikua hawajui umuhimu wa kuwa na hizo ....

    Wakiendaga kutembelea mabunge ya wenetu sijui wanaangaliaga na kuiga nini huko.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2010

    Aibu tupu. Kwa bei ya shangingi moja wabunge wangeweza kujinunulia computer zao. Uendelezaji huu wa omba omba ndio unaoturudisha nyuma. Aibu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 09, 2010

    Nilizani ntakua wa kwanza kuona tatizo la misaada. Asavali kuna walionitangulia kuliona hilo.

    Kuna vitu vinavonifanya nichukie kuitwa mtanzania. Mojawapo ni hili la misaada. Tuone aibu jamani ndugu zangu watanzania. Duh!!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 09, 2010

    trojan horses na madudu mengine utayakuta ndani yake, kwa uwezo mdogo wa Tanzania ata kama ukizi-scann zote hautakuta kitu bali wamejificha ndani yake na wanakuwa activated after few months after you switched them on.

    Mambo ya espionage hayo!

    dah! Tanzania yangu inaelekea wapi!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 09, 2010

    hata kama hizo komputer ni bora kiasi gani. bei yake haitaweza kuzidi milioni 13.5

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...