Hellow wadau, natumaini ni wazima wa afya na mnaendelea poa na ujenzi wa taifa. Napenda kuwafahamisha kwamba nimejiunga katika medani ya WANABLOGU tafadhali naomba mnipokee kwa mikono miwili na kunipa ushirikiano.. Blogu yangu inajulikana kama
www.mamapipiro.blogspot.com.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
Wenu Dina Ismail.
----------------------------------
Globu ya Jamii inatoa pongezi nyingi kwa Da' Dina Ismail kwa kujichovya kwenye ulimwengu wa libeneke. Tunamtakia kila la heri na mafanikio katika hili na kumtaka asikate tamaa kwani mwanzo mara nyingi huwa mgumu. Tunatoa changamoto kwa kinadada na kinamama kuiga mfano wa wana libeneke wanawake ambao kwa sasa inatia moyo kuona wanavyozidi kuchangamka - Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    This is good...sijapenda hiyo rangi nyekundu lakini nimependa habari zako...

    Na pia hebu jaribu kuangalia hiyo picha uliyoiweka hapo juu...labda uipunguze pixels manake sijui umetengenezea kwenye screen ya ukubwa gani...Kumbuka watu wanaoaingia kwenye blog yako hawatakua na screen size sawa..Mimi humu naona picha iko kulia habari zipo kushoto...Then ukishuka chini ndio mambo yanaeleweka na kulingana

    Ni hayo tu keep up with your good work and I will be back for more

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2010

    Madam, tafadhali cheki formatting au layout ya hiyo globu yako. Nimejaribu kuifungua kwenye browser tofauti (IE, Firefox na Chrome) kote haidisplay vizuri. Sentensi ziko wima badala ya kwenda from left to right.

    Laptop display yangu ni 1600 x 900.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2010

    Dada Kama alivyosema Anony aliyetangulia, jaribu kufanyaa uchaguzi wa rangi upya, maana rangi uliyoweka kidogo ina mapungufu. Omba msaada kwa watu wanaoweza kukusaidia kudesign graphics. Pia kuhusu size kama alivyosema mdau aliyetangualia ni tatizo.Binafsi nasoma blog kwenye laptop ya 17' lakini kinachotokea ni kuwa picha zote ulizoweka zinajipanga moja chini ya nyingine na maelezo yake yanakaa kushoto yakitengeneza mstari mrefu sana kwenda chini maana mstari ni herifu moja kwenda chini. I wish ningetumia image uone jinsi inasotokea. Kwa hiyo jaribu kufanya marekebisho katika hilo. Kwa ujumla ni kazi nzuri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2010

    suali dada, hivi uliifanyia test yeyote blog yako kabla ya kuiweka hewani?

    Mbona sentensi ziko kiajabu ajabu au ndio style yako? ni nani mwenye muda wa kukaa na kusoma blog namna hiyo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...