Na Alfonso E. Lenhardt
ZANZIBAR INAWEZA KUWA MLANGONI MWA ZAMA MPYA NA BORA:
Barua ya wazi ya kuunga mkono kazi ya "Kamati ya watu sita" ya Baraza la Wawakilishi.
**************************************
Matukio ya hivi karibuni yamenipa matumaini makubwa sana kuhusu mustakabali wa Zanzibar. Inawezekana kuwa visiwa hivi sasa vinaingia katika zama mpya na iliyo bora zaidi. Katika mazungumzo yangu na Wazanzibari nimebaini kuwepo kwa utambuzi wa pamoja miongoni mwao kwamba wakati sasa umefika wa kusahau yaliyopita na kujenga Zanzibar mpya ikiwa na msingi imara kwa ustawi na maendeleo ya jamii, mageuzi ya kidemokrasia, kujenga mazingira mapya ya kisiasa kwa misingi ya kuheshimiana, na kukubali ukweli kuhusu hali na vipindi vigumu ambavyo Zanzibar imepitia katika historia yake, kujenga imani ya wafuasi wa vyama vyote vya siasa kuhusu taasisi zinazosimamia uchaguzi na kutafuta njia ya kuondokana na mfumo unaowagawa watu wa kutoa madaraka yote kwa chama kilichoshinda uchaguzi na kuwa na mfumo wa kisiasa unaojumuisha pande zote kuu mbili za kisiasa visiwani Zanzibar.
Nimepata heshima ya kukutana na wagombea wakuu wa Urais visiwani Zanzibar. Wote ni watu wenye maono, nia njema na wasio na msimamo mkali. Kwa yeyote atakayekuwa amepata kura nyingi zaidi kuliko mwingine najua ni nani atakayekuwa ameshinda: ni Watu wa Zanzibar. Ninaamini kuwa viongozi hawa wana dhamira ya kweli ya kushirikiana katika kuiinua Zanzibar.
Chaguzi za vyama vingi visiwani Zanzibar, tangu nyakati za mwisho za ukoloni, mara nyingi zimekuwa zikihusisha kambi kuu mbili za kisiasa zikiwa na karibu idadi sawa ya wafuasi. Kuufanya upande ulioshindwa uchaguzi kutokuwa na sauti yoyote katika serikali husababisha hali ya kukata tamaa, utengano na mazingira ya kisiasa yenye uhasama. Mivutano na uhasama wa kisiasa hukwaza maendeleo. Aidha, machafuko ya kisiasa yanaharibu sifa nzuri ya Tanzania kimataifa na kwa kukwaza utalii na uwekezaji, yanaharibu pia uchumi.
Kama nilivyosema miezi michache iliyopita - rai yangu ni kwamba tuufanye mwaka 2010 uwe mwaka wa maridhiano ya Zanzibar! Kwa uongozi imara, ustahimilivu na nia njema kutoka kwa watu wote, uendeshaji wa chaguzi za mwaka 2010 uwe ni ule utakaowafanya raia wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuona fahari.
kama alivyosisitiza Rais Obama katika hotuba yake ya Ghana mwaka jana, sera zetu zinajengwa katika msingi kwamba "Mustakabali wa Afrika upo mikononi mwa Waafrika wenyewe.” Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Balozi Johnnie Carson aliwekea msisitizo wazo hili pale aliposema: " Bila kuwepo kwa dhamira ya dhati kutoka kwa viongozi wa Afrika ya kuweka na kutekeleza kikamilifu mageuzi na sera zinazohitajika kuleta mabadiliko ya kweli, hatuwezi kutarajia kufikia malengo yetu ya pamoja ya kuwa na Afrika yenye amani, ustawi na uhuru zaidi."
Wazanzibari kwa kupitia wawakilishi wao katika Baraza la Wawakilishi wameamua kuchukua hatua kubwa na muhimu ya kutafuta suluhu ya Kizanzibari kwa matatizo ya Zanzibar. Baraza hili limeunda kamati ya watu sita ambayo jukumu lake kubwa litakuwa ni kutekeleza Azimio la Baraza la Wawakilishi la kuendesha zoezi la kura za maoni lililo huru na la haki ili kuwawezesha wananchi kuamua aina ya serikali wanayoitaka.
Napenda kutoa pongezi na heshima zangu za dhati kwa wajumbe wa Kamati hii. Mola awajaalie busara ya kuweza kuongoza vyema shughuli hii kwa kusaidia kujenga mfumo utakaowezesha kufanyika kwa uchaguzi ulio huru, wa haki na amani na kuanzishwa kwa serikali inayosikiliza sauti za Wazanzibari wote. Dua zangu zi pamoja nanyi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...